#SheriaYaLeo (251/366); Gawa ili kushinda.

Pale tunapokabiliana na kitu chochote kikubwa, iwe ni adui, jukumu au changamoto, huwa tunahofia.
Ukubwa wa kile kinachotukabili unatuogopesha kwa kuona hatuwezi kukishinda.

Lakini huo siyo ukweli, hakuna chochote kikubwa ambacho hatuwezi kukishinda kama tutatumia njia sahihi.

Na moja ya njia bora kabisa ya kushinda kitu chochote kinachokukabili ni kukigawa.
Igawe nguvu ya adui kwenye sehemu ndogo ndogo na hapo utaweza kumkabili na kumshinda.
Ligawe jukumu kubwa kwenye sehemu ndogo ndogo ambazo unaweza kuzifanyia kazi mara moja.
Na hata kwa changamoto, igawe kwenye sehemu ndogo ndogo ndiyo uanze kuitatua.

Hakuna chochote kikubwa ambacho huwezi kukigawa kwenye sehemu ndogo na ukakishinda.
Kugawa kitu kikubwa kwenye sehemu ndogo ndogo ni mkakati ambao unakupa ushindi kwenye jambo lolote lile.

Sheria ya leo; Kila kikubwa unachokabiliana nacho kigawe kwenye sehemu ndogo ndogo kisha anza kukabiliana na kimoja baada ya kingine.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji