#SheriaYaLeo (257/366); Fikiria matokeo yasiyotegemewa.
Sisi binadamu, huwa tunafikiri kwa uvivu na urahisi.
Huwa tunaona kama vile matokeo yanafuatana.
Kwamba baada ya A ni B, kisha C na kuendekea, sivyo mambo yanavyokuwa kwenye uhalisia.
Unapaswa kujua kwamba kila jambo hapa duniani lina ugumu na utata.
Kuna mambo yatahusishwa ambayo hayakutegemewa kabisa.
Huwezi kujua kabla au kutabiri kwa uhakika jinsi ambavyo mambo yatakwenda.
Ndiyo maana ni muhimu sana kwenye kila jambo unalojihusisha nalo kufikiria pia matokeo yasiyotegemewa kutokea.
Chochote kile kinachoweza kutokea kinaweza kutokea hata kama uwezekano wake ni mdogo.
Kuyafikiria matokeo yasiyotarajiwa kunakufanya uwe na maandalizi bora ya chochote kinachoweza kutokea, hata kama ni cha tofauti kabisa.
Unapaswa kulifikiri kila jambo kwa kina kuliko ambavyo imezoeleka.
Na hapo utakuwa tayari kukabiliana na chochote kinachoweza kujitokeza.
Sheria ya leo; Kwa kila mkakati unaokuwa nao, fikiria matokeo yote yanayoweza kutokana na mkakati huo kisha kuwa na maandalizi sahihi kwa matokeo yoyote yanayoweza kutokea na siyo yale tu unayotegemea.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
Asante kocha kwa maarifa haya mungu akubariki sana
LikeLike