#SheriaYaLeo (258/366); Usitaharuki.
Huwa ni kawaida yetu sisi binadamu kutaharuki pale tunapokutana na mambo makubwa na ya tofauti na tulivyozoea.
Lakini kutaharuki huko huwa hakuna msaada wowote, zaidi ya kutufanya tuwe dhaifu zaidi na kuwa kwenye hali ya kushindwa.
Jambo lolote linalotokea, hata liwe kubwa na la tofauti kiasi gani, hatupaswi kutaharuki.
Badala yake tunapaswa kuwa na utulivu mkubwa ndani yetu, tukichukulia jambo hilo kama kile kitu ambacho tayari tumebobea kwenye kukifanya.
Unapokuwa na utulivu ndiyo unaweza kufikiri vyema na kuchukua hatua ambazo ni sahihi.
Hata maadui zako, huwa wanakuweka kwenye hali ambayo utataharuki ndiyo waweze kunufaika na wewe.
Kama utajizuia kutaharuki, utakuwa na utulivu mkubwa sana ambao utawafanya maadui zako wakuogope kwa kuwa hawajui ni hatua zipi utakazochukua na madhara ya hatua hizo.
Jidhibiti sana usiwe mtu wa kuibuka na hisia kirahisi. Kwani hilo linaweka wazi udhaifu wako ambao wengine wanaweza kuutumia kwa manufaa yao.
Jijengee utulivu mkubwa wa ndani na huo utakupa fursa ya kuona mambo kwa usahihi na hatua bora unazopaswa kuchukua.
Sheria ya leo; Jijengee udhibiti mkubwa kwa kulazimisha fikra zako kulenga kwenye eneo moja ambalo tayari una ubobezi nalo. Zoezi hilo litakupa utulivu mkubwa ambao utakuwezesha kuona kitu kwa uhalisia wake na kuchukua hatua sahihi bila ya kutaharuki.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
Shukurani kocha kwa uwezo wa mungu nafanyanyia kazi maarifa haya
LikeLike