#SheriaYaLeo (261/366); Linganisha matokeo na njia.
Majenerali wote bora huwa wanaanza kwa kuangalia njia walizonazo kisha kutengeneza mkakati wa kuweza kuzitumia vyema ili kupata matokeo wanayoyataka.
Wanaanza kwa kufikiria uhalisia ulivyo, kwa upande wao na wa maadui pamoja na mambo mengine yote yanauohusika kwenye mapambano.
Kufanya hivyo kunawapa msingi sahihi wa kupangilia mashambulizi yao na kupata matokeo wanayoyataka.
Wanaepuka kunasa kwenye mapambano kwa kuwa tayari kubadili matokeo yaendane na njia zilizopo.
Pale unapokuwa na kampeni au changamoto yoyote jaribu zoezi hili; usifikirie kuhusu malengo yako au ndoto ulizonazo na wala usiweke mkakati wako kwenye karatasi.
Badala yake fikiria kwa kina nini ulichonacho – zana na rasilimali utakazofanyanazo kazi.
Usizame kwenye ndoto ulizonazo bali zama kwenye uhalisia ulivyo. Fikiria ujuzi ulionao au chochote kinachokuweka kwenye nafasi nzuri zaidi na uweze kutumia vyote kupata matokeo matokeo mazuri.
Kuanza na ndoto ulizonazo kisha kutafuta njia za kuzifikia ni njia ambayo itakuchosha, kukupoteza na kufanya ushindwe.
Anza na njia ulizonazo kisha zitumie vizuri kupata matokeo bora.
Sheria ya leo; Mara zote linganisha matokeo na njia; unaweza kuwa na mpango bora wa kufikia matokeo fulani, lakini kama huna njia sahihi ya kufikia matokeo hayo, mpango wako hauna maana.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji