#SheriaYaLeo (266/366); Wavuruge wasiweze kukusoma.

Nguvu ya maadui zako ipo kwenye uwezo wao wa kukusoma na kujua nia na mipango uliyonayo.

Lengo la mikakati yako linapaswa kuwa ni kuwazuia maadui wasiweze kukusoma.

Utaweza kukamilisha hilo kwa kuwavuruga maadui zako, kuwafanya wahangaike na mambo yasiyokuwa sahihi.

Unachofanya ni kuigiza unafanya kitu fulani au kwenda kwenye njia fulani na hapo maadui wanadhani wameshajua nia na mipango yako.
Kumbe hiyo ni hadaa tu, unakuwa umewapoteza kwa kuwafanya wahangaike na kile kisichokuwa sahihi kuhusu wewe.

Sheria ya leo; Kadiri unavyovunja uwezo wa watu kukusoma na kukuelewa, ndivyo unavyowavuruga na kuwafanya washindwe kukudhuru.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji