#SheriaYaLeo (267/366); Tumia machale yako.

Mara nyingi sana utahitajika kufanya maamuzi ya haraka kabla hujawa na taarifa za kutosha.

Ni kwenye hali za aina hiyo ndiyo unapaswa kuyatumia vizuri machale yako.
Kutumia hisia za ndani yako katika kufanya maamuzi sahihi.

Kabla ya kutumia machale yako, lazima kwanza uyaendeleze.

Na njia bora ya kuyaendeleza machale yako ni kujua kwa kina kile unachofanya.
Unapaswa kujijengea ubobezi mkubwa kwenye kile unachofanya kwa kujua taarifa nyingi kuhusu kitu hicho.

Ni taarifa hizo nyingi unazokuwa nazo ndizo zinazokuwezesha kufanya maamuzi ya haraka pale unapohitajika kufanya hivyo.

Huwezi kusubiri mpaka wakati wa maamuzi ndiyo ujifunze kitu kwa undani.
Badala yake unapaswa kukijua kitu kwa undani kabla ili unapohitajika kufanya maamuzi ya haraka, unatumia ujuzi wote ulionao kufanya maamuzi sahihi.

Sheria ya leo; Ijenge akili yako kuweza kufanya maamuzi ya haraka kwa kutumia machale yako. Na unapaswa kuyajenga machale yako kwa kuwa na uelewa wa kina kwa kile unachofanya.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji