2764; Wimbo unaoupenda sana.
Rafiki, hebu fikiria wimbo mmoja ambao unaupenda sana.
Tena hebu uimbe kidogo wimbo huo.
Unaujua kwa hakika mashairi yake yote.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwa baadhi ya matangazo ya biashara.
Kuna baadhi ya matangazo ambayo umekuwa unayapenda sana na unayajua maelezo yake yote.
Sasa nina swali dogo kwako, je umewahi kutenga muda ili kukariri kwa nguvu wimbo au tangazo unalopenda?
Je umewahi kujifungia ili kusoma na kuandika neno kwa neno ndiyo ukumbuke mistari au maneno ya wimbo na tangazo unalopenda?
Majibu ni hapana.
Umekariri wimbo na tangazo unalopenda siyo kwa kutumia nguvu, bali kwa kujirudia rudia kwa muda mrefu.
Umekuwa unasikiliza wimbo na tangazo kwa muda mrefu na kwa kujirudia rudia mpaka imekuwa sehemu yako.
Hiyo inaonyesha nguvu ya marudio kwenye fikra zetu.
Chochote ambacho tunakirudia rudia kwa muda mrefu, kinakuwa sehemu yetu.
Hatua ya kuchukua;
Leo na kila siku nenda katumie nguvu ya kujirudia rudia ili kuweza kujenga fikra sahihi kwako na zitakazokupa matokeo makubwa.
Hapa kuna #Kauli10Chanya za kujiambia kila siku, jirekodi kwenye simu yako ukiwa unajiambia kauli hizo kisha sikiliza rekodi yako mara kwa mara mpaka iwe sehemu yako.
💥Kauli 🔟 chanya za kujiambia kila siku.
1️⃣Mimi …… (majina kamili) ni bilionea na muuzaji bora kuwahi kutokea.
2️⃣Hii ni siku bora na ya kipekee sana kwangu kufanya makubwa.
3️⃣Mimi ni msikilizaji makini na ninayejali.
4️⃣Nina shauku kubwa ya kuwahudumia wateja wangu.
5️⃣Napenda sana kuwapigia simu wateja wangu.
6️⃣Napenda sana kuwatembelea na kukutana na wateja wangu.
7️⃣Napenda sana kuwahudumia wateja wangu na kuwapa thamani.
8️⃣Napenda sana kuwafuatilia wateja wangu baada ya kuwauzia na kwenye ahadi zao.
9️⃣Mimi ni mkamilishaji bora wa mauzo.
🔟Leo ninakamilisha mauzo ya tsh …..
🔹️ Jirekodi kwa sauti ukijiambia kauli hizi kwa hisia kali kisha sikiliza siyo chini ya mara 10 kwa siku kila siku.
Poa ziandike kauli hizo anbalau mara 3 kwa siku.
Na pia endelea kuzitafakari kwenye muda wako mwingi wa siku.
#Tafakari;
Unakuwa kile unachofikiri kwa muda mrefu. Jilazimishe kufikiri mambo yenye tija ili uweze kuwa mtu bora kwa namna unavyotaka.
#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed