#SheriaYaLeo (272/366); Pangilia mpaka mwisho.

Hatari nyingi kwenye maisha, ambazo zipo mbele yetu, huwa zinaweza kuepukika kama tukiwa na mipango mizuri mpaka mwisho.

Mara nyingi huwa tunachukua hatua ya kutatua tatizo dogo, lakini tunaishia kuzalisha tatizo kubwa zaidi.

Kwenye mamlaka, nguvu kubwa ipo kwenye vitu unavyoacha kufanya kuliko vile unavyovifanya.
Hatua za kijinga unazojizuia kuzichukua kabla hujaingia kwenye matatizo zaidi.

Ni vyema kuweka mipango ya kina kabla ya kuanza. Pangilia kitu mpaka mwisho wake kabla hata hujaanza kukifanya.
Usikubali mipango ya hovyo ikuingize kwenye matatizo makubwa zaidi.

Mwisho mbaya ni mwingi kulilo mwisho mzuri na wenye furaha.
Usipotezwe na mwisho mzuri unaoweza kuwa nao kwenye fikra zako.
Badala yake pangilia kila kitu mpaka mwisho ili kujua kama ni kitu sahihi kwako kufanya au la.

Sheria ya leo; Kwa kila hatua unayopanga kuchukua jiulize; Je hatua hii itakuwa na matokeo tofauti na ninavyotegemea? Je nitaishia kutengeneza maadui wapya? Je kuna ambao watanufaika zaidi na nguvu zangu?
Pangilia kila kitu mpaka mwisho ili uweze kujua kama ni sahihi kwako kufanya kabla hata hujakifanya.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji