#SheriaYaLeo (276/366); Hakuna chenye nguvu kuzidi asili ya mwanadamu.
Watu wengi hudhani ujuzi wa asili ya binadamu umepitwa na wakati.
Huona kwa maendeleo ya teknolojia tuliyonayo, tunepiga hatua kuondoka kwenye asili yetu binadamu na kuwa bora zaidi.
Lakini hilo siyo kweli.
Pamoja na mabadiliko makubwa ambayo yameendelea kwenye kila eneo la maisha, asili yetu sisi binadamu haijabadilika, bado iko vile vile.
Na zaidi, asili yetu binadamu imepata nguvu zaidi kwenye mabadiliko yanayoendelea.
Chukua mfano wa mitandao ya kijamii.
Kupitia mitandao hiyo, asili ya binadamu imepata nguvu zaidi.
Ona jinsi ambavyo watu wanaoneana wivu na kujilinganisha kupitia mitandao hiyo.
Ona jinsi ambavyo wenye nia fulani wameweza kuitumia kuwagawa watu na kupata kile wanachotaka.
Yote hayo yamewezekana kutokana na nguvu ya asili yetu binadamu, nguvy ambayo imekuwa haibadiliki kwa namna yoyote ile.
Ukweli ni kwamba asili ya binadamu ina nguvu kuliko vitu vingine vyote. Asili hiyo ndiyo inayoamua jinsi ambavyo maisha ya mtu yanakuwa.
Hivyo ni muhimu sana kujifunza kuhusu asili ya binadamu na kutumia maarifa hayo kuwa bora zaidi.
Sheria ya leo; Kukataa kukubali ukuu wa asili ya binadamu ni kuchagua kuwa na maisha magumu na yenye mvurugiko. Ielewe kwa kina asili ya binadamu ili kuweza kuitumia vyema kuwa na maisha bora.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji