2773; Usichokitaka.
Kama kuna kitu ambacho hukitaki kwenye maisha yako, dawa yake ni kukipuuza.
Hapaswi kupambana na chochote ambacho hukitaki.
Kwa sababu kwenye kupambana na kitu, unakipa nguvu zaidi na hivyo kuishia kushindwa.
Njia ya uhakika na ya ushindi ni kupuuza kile ambacho hukitaki.
Kuchukulia kama vile hakipo na hukihitaji kabisa.
Kama kitu hukihitaji, wewe kipuuze kabisa. Kwenye fikra zako kufute na usijisumbue nacho kwa namna yoyote ile.
Hiyo ndiyo njia ya uhakika ya kuachana na mambo yasiyokuwa na tija na kupeleka umakini wako kwenye mambo muhimu.
Mambo usiyoyataka ni mengi, ukisema ujihangaishe nayo yote utakosa nguvu na umakini wa kushughulikia yale ambayo ni muhimu zaidi.
Kwa kupuuza na kuchukulia mambo kama vile hayapo kabisa au siyo muhimu kunakupa wewe nguvu na mamlaka makubwa ya kufanya maamuzi sahihi na yenye tija kwako.
Hatua ya kuchukua;
Ni vitu gani ambavyo huvitaki kwenye maisha yako na hivyo kuwa unapambana navyo?
Achana na hilo mara moja, kupambana na kitu unakipa nguvu zaidi na hivyo kukusumbua.
Chochote usichotaka, kipuuze kabisa. Kifute kabisa kwenye fikra zako na utakuwa umekinyima nguvu za kukusumbua.
Tafakari;
Kupuuza kuna nguvu kubwa.
Unapokipuuza kitu, unakiondolea nguvu ambayo kitu hicho kilikuwa nayo juu yako.
Hupaswi kuruhusu kitu chochote kikusumbue, wewe ndiye unayeweza kufanya watu au vitu vikusumbue au visikusumbue.
Fanya maamuzi sahihi ambayo yatakuacha wewe kwenye utulivu mzuri wa kuweza kufanya maamuzi bora zaidi kwa mwendelezo.
#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed