#SheriaYaLeo (277/366); Uwezo Mkubwa Wa Ndani.
Kila binadamu huwa ana kitu anachokiabudu. Huwa kuna kitu cha juu ambacho mtu anakijeshimu na kukitukuza zaidi.
Kwa baadhi ya watu ni ufahari wao wa ndani. Wengine ni familia zao, dini zao au jamii zao.
Wanafalsafa wa kale waliamini na kuabudu uwezo mkubwa ulio ndani ya kila mtu.
Ni uwezo huo ndiyo unaompa mtu akili ya kuweza kukabiliana na mambo mbalimbali anayokutana nayo kwenye maisha.
Uwezo huo wa ndani ambao kila mtu anao, ndiyo unaowapa watu akili ya kuweza kufanya makubwa zaidi.
Ni sauti inayowajia watu katika nyakati wanazokuwa wanapitia magumu.
Ni uwezo huo wa ndani ndiyo unawapa watu uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi badala tu ya kusukumwa na hisia.
Kwa kuwa mara nyingi sisi binadamu tumekuwa tunasukumwa kufanya maamuzi kwa hisia na mihemko, kwa kujua na kutumia uwezo mkubwa wa ndani tutaweza kufanya mambo makubwa na ya tofauti.
Ili uweze kufikia uwezo huo wa ndani na kuutumia, lazima uweze kuzivuka hisia zinazokutawala kwa muda mrefu.
Sheria ya leo; Endeleza uwezo wako mkubwa ulio ndani yako na uabudu huo. Kwa njia hiyo utaweza kufanya maamuzi kwa mantiki badala ya hisia, kitu ambacho kinapelekea uweze kufanya maamuzi bora kabisa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji