#SheriaYaLeo (278/366); Chambua, chunguza na hoji.
Ili kujenga uwezo mkubwa wa ndani unaoweza kufanya maamuzi sahihi, unapaswa kutafuta njia ya kutawala hisia zako.
Hisia huwa zinatuondoa kwenye uwezo wetu mkubwa wa kufikiri.
Hisia hizo zinatuteka na kuathiri mtazamo tunaokuwa nao.
Tunapokuwa tumetawaliwa na hisia, hatuvioni vitu kama vilivyo kwa uhalisia wake, bali tunaviona kulingana na hisia tulizonazo.
Unapaswa kujifunza kujizuia kufanya maamuzi wakati unapokuwa umetawaliwa na hisia kali.
Unachotakiwa kufanya kwenye hali hiyo ya kutawaliwa na hisia kali ni kichambua, kuchunguza na kuhiji usahihi na uhalali wa hisia unazokuwa nazo.
Kwa kufanya hivyo ndiyo unagundua kwamba hisia unazokuwa nazo siyo sahihi wala muhimu.
Hapo ndipo unaweza kuzitelekeza hisia hizo na kurudi kwenye uwezo mkubwa wa ndani wa kufikiri na kufanya maamuzi.
Kuna wakati utahitajika kukaa peke yako kwa muda mrefu ambapo utazituliza hasia na kurudi kwenye uwezo wako mkubwa wa ndani.
Sheria ya leo; Ziangalie hisia zote ambazo zinaathiri fikra zako na maamuzi unayofanya. Jifunze kuchambua, kuchunguza na kujihoji juu ya hisia zozote unazokuwa nazo, kujua sababu ya hisia hizo na kinachozichochea. Ni kwa njia hiyo ndiyo unaweza kuzivuka na kwenda kwenye uwezo mkubwa wa ndani.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji