#SheriaYaLeo (283/366); Nguvu ya ushirikiano.
Sisi binadamu huwa tunaathiriwa sana na fikra na hisia za watu ambao tunashirikiana nao.
Huwa tunaishia kuwa kama wale ambao tunakaa nao kwa muda mrefu.
Wale waliotawaliwa na hisia hasi, wasio na furaha na wenye kisirani huwa wana nguvu kubwa ya kushwishi kwa sababu hisia zao huwa ni kali.
Huwa wanajionyesha kama watu wasio na hatia, wakilalamika kwamba wameonewa au wana bahati mbaya. Hilo linafanya iwe vigumu kuona jinsi ambavyo wametengeneza wenyewe hali wanazopitia.
Kwa kushirikiana na watu wa aina hiyo, unajikuta na wewe una matatizo kama yao, wanakuwa wamekuambukiza.
Elewa kwamba watu unaoshirikiana nao wana ushawishi mkubwa kwako. Mara nyingi unaishia kuwa kama wao na pale utakapotaka kuachana nao, inakuwa vigumu sana.
Wanakufanya ujisikie vibaya kuwaacha katika hali zao, hivyo unajikuta ukizidi kukaa kwenye matatizo yao ambayo yanakuathiri sana.
Sheria ya leo; Kuwa makini na nguvu ya ushawishi ya wale ambao unashirikiana nao. Ni rahisi sana kuambukizwa matatizo waliyonayo wengine.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji