2783; Haina matumizi.

Kitu chochote kikishakosa matumizi, kinaanza kuharibika.

Angalia majengo mazuri ambayo hayatumiki, huwa yanaanza kuharibika vibaya.

Kadhalika kwenye vifaa mbalimbali tunavyotumia, kama kifaa hakitumiki kinaanza kuharibika.

Tunapata funzo kubwa sana hapa kuhusu maisha ya mafanikio.
Kama kuna kitu tunakosa au kushindwa kutumia, inasababishwa na sisi kukosa matumizi na kitu hicho.

Unapokuwa na muda wa siku ambao hujaupangilia, unaishia kupotea bila hata kujua umepoteaje. Unashangaa siku inaisha, umechoka kweli kweli, ila ukiangalia hakuna chochote kikubwa ulichokamilisha.

Kadhalika kwenye fedha. Kwa maisha yako yote, kuna fedha nyingi sana ambazo zinapita kwenye mikono yako.
Lakini mwisho wa siku unaishia kujikuta hakuna akiba wala uwekezaji umefanya.
Hiyo yote inasababishwa na kukosa matumizi yaliyopangiliwa kwenye kitu chochote kile.

Kwa chochote ambacho hakipo sawa kwa upande wako, anza kwa kuangalia umepanga na kusimamiaje kwenye eneo hilo.

Hatua ya kuchukua;
Angalia kila unachofanya na matokeo unayoyapata. Angalia mipango uliyonayo kwenye kila eneo.
Utagundua maeneo yote ambayo huna mipango na usimamizi mzuri ndiyo ambayo unapata matokeo mabovu.

Tafakari;
Asili inaheshimu vitu vinavyopangwa na kusimamiwa vizuri. Hiyo ndiyo hatua muhimu ya kuanza nayo, pangilia vizuri kila kitu kwenye maisha yako na simamia kile ulichopanga.
Utashangaa jinsi ambavyo mambo yatakwenda vizuri kuliko awali.

#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed