#SheriaYaLeo (289/366); Epuka nguvu ya kubadilishwa na kundi.
Sisi binadamu ni viumbe wa kijamii, huwa tunapenda sana kuwa ndani ya makundi ya watu wengine.
Lakini makundi hayo huwa yana nguvu kubwa ya kutubadili kwa namna tunavyofikiri, kusema na kufanya.
Ndani ya kundi tunajikuta tukijilinganisha na wengine na kujali wanatuchukuliaje.
Bila ya kujua unajikuta ukiwa unabadilika ili ukubalike na wale wanaokuzunguka.
Unawaiga wengine kwa mwonekano, kufikiri, kuongea na kufanya.
Ndani ya kundi asili iliyo ndani yetu inaibuliwa na kujikuta tukifanya vitu ambavyo peke yetu tusingeweza kufanya.
Kuepuka nguvu hii ya mabadiliko iliyo ndani ya makundi mbalimbali, unapaswa kwenda kinyume na mazoea na msukumo wa ndani.
Unapaswa kukubali jinsi kundi lilivyo na nguvu ya kukusukuma ubadilike. Kisha kuhakikisha nguvu hiyo haikufanyi wewe pia ufuate mkumbo.
Badala yake kuendelea kufikiri, kusema na kufanya kwa namna tunavyoona ni sahihi kwetu na siyo kufanya kwa sababu wengine pia wanafanya.
Ni lazima uweze kushinda nguvu ya kubadilishwa na kundi na kusimama kuwa wewe mara zote.
Huwezi kufanikiwa kwa kuiga wengine, bali unafanikiwa kwa kuwa wewe.
Kataa kufuata mkumbo na simama kuwa wewe hata kama watu wote wanakupinga.
Sheria ya leo; Kuwa mkweli kwako mwenyewe ili uweze kufanya yake sahihi kwako. Jiulize kila unachofikiri, kusema na kufanya kimetoka ndani yao kweli au umeiga kutoka kwa wengine? Mafanikio yapo kwenye kuwa wewe na kuacha kufuata mkopo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UdadisiUpekeeUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji