AMKA CONSULTANTS ni kampuni inayotoa ushauri elekezi na mafunzo kwenye biashara. Kampuni imejikita kuziwezesha biashara ndogo na za kati kujiendesha kwa mfumo na kufanya mauzo makubwa zaidi.

Kampuni inatoa mafunzo bora ya mauzo kwa biashara na wafanyakazi wa biashara ambayo yanapelekea biashara kukuza zaidi mauzo yake.

Kupitia kufanya kazi na wafanyabiashara wengi wadogo na wa kati, changamoto kubwa imeonekana ni kukosekana kwa watu wazuri wa mauzo. Biashara nyingi zimekufa na nyingi kushindwa kukua kwa sababu hazina watu sahihi wa mauzo, wenye msukumo na shauku ya kufanya mauzo makubwa.

Ni kwa sababu hiyo, AMKA CONSULTANTS imechukua hatua ya kutafuta watu wazuri wa mauzo ambao wana kiu, msukumo na shauku kubwa na kuwaunganisha na biashara ambazo zina uhitaji mkubwa wa watu hao.

Kama wewe ni mtu ambaye unajiona ukiweza kufanya vizuri kazi ya mauzo basi kuna nafasi nzuri ya wewe kupata kazi. Chukua hatua ya kujaza fomu ambayo link yake iko hapo chini na utapewa maelekezo zaidi baada ya hapo.

Ieleweke wazi kwamba siyo AMKA CONSULTANTS inayoajiri na wala AMKA CONSULTANTS siyo wakala wa kuajiri. Sisi AMKA CONSULTANTS tumeona ombwe la ukosefu wa watu sahihi wa mauzo kwa wateja wetu na tunaamini kuna watu wazuri wa mauzo wapo, ila hawajui kuhusu uwepo wa nafasi zinazopatikana. Hivyo sisi AMKA CONSULTANTS tunachofanya ni kuwaunganisha pamoja wenye uhitaji wa watu wa mauzo na wenye uhitaji wa kazi za mauzo kisha mchakato wa makubaliano ya kazi unaendelea baina yenu.

Kitu pekee ambacho AMKA CONSULTANTS itaendelea kufanya ni kutoa mafunzo endelevu ya MAUZO kwa wale watakaopata kazi za mauzo kwa wateja wetu, gharama ambazo zitalipiwa na biashara husika na siyo mfanyakazi.

Sifa kuu zinazohitajika kwenye kazi hizi za mauzo ni tatu;

Sifa ya kwanza ni uwe na tabia njema. Tunaamini tabia ni kitu ambacho mtu hawezi kufundishwa, ni kitu kilicho ndani ya mtu. Na pia tunaipa tabia uzito mkubwa. Hivyo unapoomba nafasi hizi, hakikisha una tabia njema. Tabia huwa haijifichi na pia haitavumiliwa pale inapoathiri biashara. Sifa kuu ya kazi ya mauzo ni kuwafanya wateja wajisikie vizuri, kama una tabia yoyote inayowafanya wateja wasijisikie vizuri pale wanapojihusisha na wewe hilo litakunyima sifa ya kazi.

Sifa ya pili ni upende kazi na kujituma. Tunaamini sana kwenye kazi na kukaa kwenye mchakato sahihi wa mauzo ambao utafundishwa. Mchakato huo unahusisha kutafuta wateja, kuwashawishi kununua na kuwafuatilia baada ya kununua. Muda wa kufanya kazi utakuwa masaa ya kawaida, lakini ufanisi utapimwa kwa majukumu ambayo mtu anayakamilisha kwenye muda wake wa kazi.

Sifa ya tatu ni kupenda kujifunza endelevu. Tunaamini kwenye kujifunza kila siku kama njia ya kuwa bora na kupiga hatua binafsi na hata kwenye kazi na biashara. Hivyo mtu anayeomba kazi hizi anapaswa kupenda kujifunza endelevu kupitia kusoma vitabu, kujiunga na kozi mbalimbali na njia nyingine za kujifunza ili kuwa bora kwenye mauzo. Pia kutakuwa na programu endelevu ya kujifunza kila siku na kujibu maswali ya quiz. Sehemu hii ya kujifunza kila siku na kujibu quiz ni ya lazima kama utapata kazi ya mauzo.

Sifa kuu ni hizo tatu tu, nyingine kama elimu, umri, kabila, jinsia hazina uzito. Hizo tatu zikiwepo kwa uhakika hizo nyingine zinakuwa za ziada tu.

Kwa watakaopata kazi, mafunzo ya kina ya mauzo yatatolewa mwanzoni na kwa uendelevu ili mtu kuweza kubobea kwenye mauzo.

Mfumo wa malipo.

Mfumo wa malipo kwenye kazi hizi za mauzo utakuwa wa fedha ya kujikimu na kamisheni.

Utakapopata kazi ya mauzo kutoka kwa wateja wetu, utalipwa mshahara wa kima cha chini kama sehemu ya kuweza kujikimu kimaisha.

Halafu sehemu kubwa ya malipo itatokana na kamisheni ambayo utaipata kulingana na kiwango cha mauzo unachofanya.

Kwa msingi huu, kiasi cha malipo hakina ukomo, kadiri unavyouza zaidi ndivyo unavyolipwa zaidi. Na kwa kuwa unaendelea kupata mafunzo ya mauzo, unakuwa na fursa ya kuingiza kipato kikubwa utakavyo.

Jaza fomu.

Ili kupata taarifa zako na kuweza kukuunganisha na wafanyabiashara wenye uhitaji wa watu wa mauzo, unapaswa kujaza fomu hii yenye maswali ya msingi kuhusu wewe.

Kujaza fomu fungua kiungo hiki; https://forms.gle/d6mXn4fVpYBJwUNQ6

Hitimisho.

AMKA CONSULTANTS tunaamini mauzo ndiyo moyo wa biashara, ambao unasukuma damu kwenye biashara ambayo ni fedha. Bila ya mauzo hakuna fedha na bila ya fedha hakuna biashara.

Tunaamini kila mfanyakazi aliye ndani ya biashara anapaswa kuchangia kwenye mauzo. Hivyo kila mfanyakazi wa biashara anapaswa kuwa na mafunzo sahihi ya mauzo.

Hivyo tunaendelea kufanya kazi kwa karibu na wafanyabiashara wadogo na wa kati ili kuwawezesha kujenga timu bora za mauzo zitakazowezesha biashara kufanya mauzo makubwa na kufanikiwa.

Kama wewe ni mfanyabiashara na ungependa kupata huduma ya mafunzo ya mauzo kwa wafanyakazi wako au ungependa kupata wafanyakazi bora wa mauzo tuwasiliane kwa email; amkaconsultants@gmail.com

Kwa waombaji wa kazi za mauzo jaza fomu kwa kufungua link hii; https://forms.gle/d6mXn4fVpYBJwUNQ6

Kwa wafanyabiashara tuwasiliane moja kwa moja kwa email; amkaconsultants@gmail.com

Karibuni sana.

Kocha Dr Makirita Amani.

www.amkaconsultants.co.tz