#SheriaYaLeo (298/366); Jua hujui.
Huwa tunapenda kuwabeza watu wa zama zilizopita jinsi ambavyo hawakuwa wanajua yale ambayo tunajua sasa.
Tunaona kama walikuwa watu wajinga na walioshindwa kujua yale ya msingi.
Hebu fikiria ni kwa namna gani watu wa vizazi vijavyo watatushangaa na kutubeza kwa mambo tunayofanya sasa.
Kuna mengi tunajua, kuamini na kufanya sasa, ambayo siku zijazo yatagundulika siyo sahihi.
Watu wa kipindi hicho watashangaa sana jinsi ambavyo tuliyaamini mambo hayo.
Kitu kimoja unachopaswa kujua ni kwamba hujui.
Mengi unayojua na kuamini sasa siyo sahihi.
Kadiri muda unavyokwenda, ndivyo mengi zaidi yanajulikana na hapo utajionea dhahiri jinsi ambavyo hujui.
Kujua hujui kunakufanya uwe mnyenyekevu na kuwa tayari kujifunza.
Kunakuondolea kiburi ambacho ndiyo huwa kinaleta anguko kwa wengi.
Unyenyekevu na kuwa tayari kujifunza vitakusaidia sana uweze kujifunza na kuendelea kuwa bora kadiri siku zinavyokwenda.
Inakufanya usiwe mgando kama walivyo wengine wengi.
Sheria ya leo; Inapokuja kwenye mawazo na maoni unayoshikilia, yachukulie kama vitu unavyochezea. Baadhi utayatunza, baadhi utaachana nayo lakoni nafsi yako itabaki. Jua kuna mengi hujui hivyo mara zote kuwa tayari kujifunza.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji