2803; Usitafute fursa, jitafute wewe.
Kama bado unatafuta fursa, tatizo siyo fursa hazipatikani, tatizo ni wewe bado hujajijua vizuri.
Na kama umeshajijua basi hujajitumia ipasavyo.
Fursa hazitafutwi, maana hazijawahi kupotea, wala hazijajificha.
Fursa zinajidhihirisha, pale unapokuwa mtu sahihi, kwenye eneo sahihi na wakati sahihi.
Hivyo kama bado hujapata fursa nzuri kwako, basi hujawa mtu sahihi, au haupo eneo sahihi au wakati siyo sahihi.
Hilo linamaanisha kwamba badala ya kukimbizana na kila aina ya fursa, kazana kwanza kuwa mtu sahihi, kwenye eneo sahihi na kwa wakati sahihi.
Swali litakuja, nitajuaje nimekuwa mtu sahihi, kwenye eneo sahihi na kwa wakati sahihi?
Jibu ni kwa kujisikiliza wewe mwenyewe, kujitambua, kujua kusudi lako, kuwa na ndoto kubwa na kuziendea muda wote.
Ukishakaa kwenye huo mchakato, mengine yote yanajipanga yenyewe.
Hatua ya kuchukua;
Unajiona bado hujapata fursa sahihi kwako? Kaa chini na jiulize wewe ni nani, kwa nini upo hapa duniani na ukiondoka unataka uache alama gani? Jipe majibu ya maswali hayo manne na ukae kwenye mchakato wa majibu hayo na utashangaa jinsi fursa nyingi zitakavyofunguka kwako.
Tafakari;
Ingekuwa fursa ni kitu kipo mahali fulani pekee, kila mtu angeenda hapo akaipate. Lakini sivyo fursa zilivyo, fursa hazipo mahali, bali zipo ndani ya mtu. Kama bado hujapata fursa sahihi kwako, pakutafuta siyo nje bali ndani.
#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed