2804; Hakuna kushindwa.

Watu wengi hudhani pale wanapokutana na changamoto na vikwazo mbalimbali basi wameshindwa.

Kwenye safari ya mafanikio, kushindwa ni pale unapokuwa umekata tamaa na kuacha kufanya.
Hapo ndiyo unakuwa umeshindwa kwa sababu kama umeacha kufanya, umeondoa nafasi zote za kuweza kupata matokeo mazuri.

Lakini kama unaendelea kufanya licha ya kukutana na magumu na changamoto mbalimbali, hapo hujashindwa. Kwa sababu kupitia kufanya huko unajiweka kwenye nafasi ya kupata matokeo mazuri.

Futa kabisa msamiati wa kushindwa kwenye fikra zako.
Kila unalopitia chukulia ni somo muhimu la kukujengea uwezo wa kupata kile unachotaka.

Kadiri unavyokaa kwenye kitu kwa muda mrefu, huku ukikazana kuendelea kuwa bora zaidi, ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi kubwa ya kufanikiwa.
Lakini kama haupo kabisa kwenye mchezo, nafasi ya kushinda kwako ni sifuri.

Hatua za kuchukua;
Leo pitia historia yako kwenye ufanyaji wa mambo mbalimbali. Ni mangapi ambayo uliishia njiani badala ya kuendelea kama ulivyokuwa umepanga?
Sasa ondoa kabisa hilo kwenye maisha yako. Ukishaamua unachotaka, unapaswa kukaa kwenye mchakato mpaka ukipate.

Tafakari;
Mafanikio yangekuwa rahisi kila mtu angekuwa nayo. Siyo rahisi ndiyo maana wachache pekee ndiyo wanaofanikiwa.
Unapowaangalia wale waliofanikiwa unagundua hawatofautuani sana na ambao hawajafanikiwa.
Ni maamuzi yao ya kuyataka mafanikio kweli na kutokukubali kuyumbishwa na kingine chochote.

#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed