#SheriaYaLeo (308/366); Ongeza muda wa kujibu.

Hii ni nguvu inayojengwa kwa mazoezi na marudio.
Pale jambo kinapokutaka ujibu, jifunze kusubiri kwanza kabla ya kukimbilia kujibu.

Unaweza kufanya hivyo kwa kuondoka eneo la tukio na kwenda eneo jingine ambapo utakuwa peke yako.
Au unaweza kuandika majibu yako lakini usiyatume.

Unajipa muda kwanza kabla hujatoa majibu yako. Katika muda huo hufanyi chochote kinachohusiana na hisia unazokuwa nazo.

Kila unapojikuta unasukumwa na hisia kusema au kufanya jambo fulani, jipe muda kwanza kabla hujafanya hivyo.

Tuliza hisia zako. Kadiri unavyosubiri muda mrefu bila kuchukua hatua, ndivyo unavyopata uelewa mzuri juu ya jambo husika.

Sheria ya leo; Kadiri unavyojizuia usikibilie kujibu, ndivyo unavyopata nafasi ya kuelewa zaidi na ndivyo akili yako inavyozidi kuwa imara.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji