#SheriaYaLeo (310/366); Jijue wewe mwenyewe kiundani.

Unaendeshwa na hisia pale unapokuwa hujitambui wewe mwenyewe.
Pale unapojitambua, hisia zinakosa nguvu ya kukutawala.
Unaweza kuzidhibiti na kuzuia zisiwe kikwazo kwako.

Hivyo hatua ya kwanza unayopaswa kuchukua ili kuwa mtu wa mantiki na busara ni kujitambua wewe mwenyewe.
Unapaswa kujikamata pale hisia zinapokuwa zinataka kukutawala.

Unapaswa kutambua jinsi unavyofanya kazi unapokuwa na msongo.
Ni udhaifu gani unaokuwa unahonyesha kwenye nyakati kama hizo?

Yatafakari maamuzi yote ambayo umekuwa unayafanya, hasa yale ambayo hayakuwa sahihi. Je unaweza kuona makosa uliyokuwa unafanya kwenye kufikia maamuzi hayo?

Tafakari uimara ulionao, kile kinachokutofautisha wewe na watu wengine. Hiyo itakusaidia kuchagua malengo yanayoendana na wewe na ya yenye manufaa ya muda mrefu kwako.

Kwa kutambua na kuthamini kile kinachokutofautisha wewe na wengine, utaweza kuepuka kuvutwa na kuingia kwenye mkumbo.

Sheria ya leo; Je unaweza kujiangalia wewe mwenyewe kama mtu baki na kuona jinsi hisia zinavyokuwa kikwazo kwako?

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji