#SheriaYaLeo (311/366); Nani alaumiwe?

Pale mambo yanapokwenda vibaya, ni asili ya binadamu kutafuta mtu wa kumlaumu.
Tunaamini watu wengine ndiyo waliosababisha mambo hayo kwenda vibaya.

Waache wengine wahangaike na huo ujinga, wakiongozwa na pua zao, wakiona kile tu kinachoonekana na macho.
Wewe unaona vitu kwa utofauti.

Pale mambo yanapokwenda vibaya, iwe ni kwenye kazi, biashara, maisha au siasa, unarudi kwenye sera ambayo imepelekea makosa hayo kutokea.

Hiyo ina maana kwamba wewe mwenyewe ndiye chanzo cha mambo yote mabaya yanayotokea kwako.
Kama ungekuwa makini zaidi, ukiwa na sera bora na maono makubwa, ungeweza kuepuka hatari ulizoingia.

Hivyo pale mambo yanapokwenda vibaya, jiangalie ndani yako, siyo kwa hisia na kujilaumu au kujutia, bali kwa mantiki ili kujipanga vyema wakati mwingine usirudie makosa yale yale.

Sheria ya leo; Ona mchango wako kwenye kila ambalo umeshindwa, mara zote huwa una mchango kwenye mabaya yanayokukuta.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji