2811; Kinachohitajika ni furaha.
Tunahangaika na mambo mengi kwenye maisha yetu.
Lakini mwisho wa siku kinachohitajika ni furaha.
Huenda hatujui moja kwa moja, lakini kila tunachofanya, msingi wake ni furaha.
Sasa kwa kutokujua chanzo sahihi cha furaha, tunajikuta tunajaribu kila aina ya kutu kuona kama kitatupa furaha.
Kubahatisha furaha imekuwa chanzo cha matatizo mengi ambayo watu wanapitia kwenye maisha.
Watu kudhani kupata fedha nyingi kutawapa furaha, au kustarehe kutawapa furaha.
Lakini hivyo huishia kutoa furaha ya muda mfupi tu.
Vitu vya kupata huwa haviwezi kumpa mtu furaha ya muda mrefu.
Furaha ya muda mrefu inatokana na ule mchango unaotoa kwa ajili ya wengine.
Kile unachofanya, ambacho kina manufaa mazuri kwa wengine, ndiyo chanzo bora cha furaha kwako.
Na hata kupitia hicho, bado furaha haitakuja kwa kuitafuta.
Badala yake furaha inakuwa ni tunda unalopata baada ya kutekeleza vyema wajibu wako.
Hiyo ina maana kwamba unapofanya kitu ili kupata furaha, unaishia kutokuipata.
Lakini ukisahau kuhusu wewe na kuzama kweli kwenye kile unachofanya, furaha inakuwa sehemu ya maisha yako.
Hatua ya kuchukua;
Acha kuhangaika sana na furaha, jua kile unachoweza kufanya vizuri na chenye mchango mzuri kwa wengine.
Ukishajua hicho zama kwa undani katika kukifanya na sahau kabisa kuhusu mengine.
Utashangaa jinsi matokeo unayozalisha yatakupa furaha kubwa.
Tafakari;
Furaha ndiyo lengo kuu la kila mtu, lakini hakuna ambaye ameshaweza kujua anawezaje kuipata kwa uhakika na ikadumu kwake.
Furaha imekuwa kama kipepeo, ukikikimbilia na chenyewe kinakimbia.
Hivyo unapokaa chini na kusema nafanya hiki ili nipate furaha, huipati.
Lakini unapozama kwenye kitu na kukifanya vizuri, furaha ni moja ya matokeo utakayoyapata.
#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed
Asante kocha
LikeLike