2812; Kwanza umefanya?
Hakuna kitu kinashangaza kama pale mtu anajua anachopaswa kufanya, ila hakifanyi, halafu analalamika kwa kukosa matokeo aliyotegemea.
Hakuna namna matokeo yoyote yatakuja kimiujiza kwako bila ya kuchukua hatua na kufanya.
Ukiangalia kila matokeo ambayo unayapata kwenye maisha yako, yanaendana kabisa na hatua ambazo ulichukua huko nyuma.
Kama kuna matokeo umekuwa unataka sana kuyapata ila hupati, mahali pa kuanzia ni kwenye hatua unazochukua. Kwanza umefanya? Maana kama hujafanya, haina hata haja ya kujiuliza kwa nini hupati matokeo.
Jifunze na jenga msingi wako kwenye ufanyaji, katika jambo lolote, jiulize nini umefanya au hukufanya na kikachangia kwenye matokeo ambayo umepata.
Ukijua unachopaswa kufanya na ukakifanya kweli, unakuwa na haki ya kungojea matokeo unayotaka. Lakini kama hujafanya, kusubiri matokeo bora ni kujidanganya.
Kufanya kuna nguvu ya kubadili hali yoyote ile. Hivyo wewe kuwa mfanyaji, itakuweka kwenye nafasi ya kupata matokeo bora.
Hatua ya kuchukua;
Kwenye kila hali unayotaka kuibadili kwenye maisha yako, jiulize unapaswa kufanya nini, kisha kifanye. Usitegemee mambo yabadilike yenyewe, badala yake chukua hatua za makusudi katika kuyabadili. Kuna vitu ukifanya vinabadili kabisa matokeo unayopata, vifanye hivyo.
Tafakari;
Huwezi kutegemea matokeo ya tofauti kama hakuna kitu cha tofauti ambacho umekifanya. Jenga msingi wako kwenye ufanyaji na utaweza kubadili chochote kwenye maisha yako. Kufanya kunashinda kila aina ya maneno.
#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed
Kila ninachotaka kubadili nitaanza na kujiukiza nini nifanye hili kiitokeee
LikeLike