2818; Mwenza, roho mbaya au utegemezi.

Kuanzisha biashara na kuikuza mpaka ifikie mafanikio makubwa ni kitu kigumu sana kufanya, lakini ambacho kinawezekana kwa uhakika.

Hatari kubwa na ya kwanza kwenye biashara ni kufa.
Takwimu zinaonyesha biashara nyingi sana huwa zinakufa kwenye hatua ya uchanga.
Zaidi ya asilimia 80 ya biashara mpya huwa zinakufa ndani ya miaka 2 tangu kuanzishwa kwake.

Ni takwimu za kusikitisha na kuumiza, lakini ndivyo ukweli ulivyo.
Cha kushangaza, bado wengi wanaendelea kuanzisha biashara zinazoendelea kufa, bila ya kujifunza kuhusu takwimu hizo na kutafuta njia ya kuzikwepa.
Kwa kifupi, watu wanajipeleka kwenye kifo cha biashara zao wenyewe.

Tafiti zinaonyesha kwamba, katika biashara zinazoanzishwa na kufa, zinazokufa zaidi ni zile ambazo mwanzilishi anakuwa mtu mmoja ambaye anajikuta akifanya karibu kila kitu peke yake.
Watu hawa huwa wanaishia kuelemewa na mzigo wa kisaikolojia wa kuendesha biashara, kitu kinachopelekea wakate tamaa na kuishia njiani.

Ili kuondokana na hilo, kuna njia tatu za kutumia.
Njia tatu za kuanzisha biashara ambayo haiwezi kufa haraka.

Njia ya kwanza ni kuwa na mwanzilishi mwenza, ambaye mnashirikiana kwenye mambo mengi ya mwanzoni mwa biashara. Hilo linasaidia kwenye kubeba mzigo wa kihisia na kuvuka bila kukata tamaa.

Njia ya pili ni kuwa na roho mbaya, yaani uwe tayari kujitesa wewe mwenyewe bila ya kuwa na huruma. Uwe unafurahia mateso, maana awali utayapitia mateso mengi, kama huwezi kuyahimili, hutafika mbali.

Njia ya tatu ni utegemezi, kuwa na watu wanaokuunga mkono na kuwa pamoja na wewe kwenye safari yako hiyo. Hawa ni watu wanaokuelewa na kukukubali kwa ndoto ulizonazo na wanaokupa moyo uzipambanie bila kukata tamaa.

Njia ya kwanza ya mwenza unaweza kuishindwa, kwa sababu hupati mtu mwenye maono makubwa kama wewe.
Njia ya pili ya roho mbaya unaweza kuishindwa kwa sababu hakuna anayependa kujitesa.
Njia ya tatu ya utegemezi ndiyo unaipata hapa kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Unapata fursa ya kuzungukwa na watu ambao wanakuunga mkono kwa ndoto kubwa ulizonazo na kukutia moyo uzipambanie. Wanakushauri vyema pale unapokutana na changamoto mbalimbali.

Hatua ya kuchukua;
Kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA, kushiriki mikutano ya klabu na programu ya Billionaires In Training ni fursa ya kipekee kabisa kwako kuweza kutoboa kwenye huu ulimwengu wenye changamoto za kila aina.
Kaa hapa, tekeleza unachopaswa na tumia rasilimali hizi kuhakikisha unafanikiwa kufikia ndoto zako kubwa.

Tafakari;
Jamii zetu zimejaa wakatishaji tamaa wakubwa. Watu ambao ukiwaambia ndoto zako kubwa wanakubeza na ukishindwa wanafurahia. Ni vigumu sana kufanikiwa kwenye jamii za aina hii. Bila ya kukaa kwenye jamii ya tofauti, mafanikio yatakuwa magumu sana kwako. Uzuri umeshaipata jamii ya tofauti, ishikilie ili usiipoteze.

#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed