#SheriaYaLeo (325/366); Fokasi na vipaumbele.

Baadhi ya mambo unayofanya ni upotevu wa muda wako.
Baadhi ya watu unaojihusisha nao ni wa hadhi ya chini, ambao watakuvuta urudi chini.
Unapaswa kuepuka mambo na watu hao kama ukoma ili kutumia muda wako vizuri.

Macho yako yanapaswa kuwa kwenye malengo yako makuu na hayo ndiyo yanapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza kwako na kuyapa umakini mkubwa.

Jiruhusu kuzunguka na kuchagua kwa ubunifu, lakini mara zote fanya hayo kwa kusudi, ukijua vilaumbele vyako na kuvipa hivyo umakini mkubwa.

Sheria ya leo; Kwenye dunia iliyojaa kila aina ya usumbufu, unapaswa kufokasi na kuwa na vipaumbe sahihi.

#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji