2824; Hakuna kushindwa.

Kitu kinachoitwa kwenye maisha hakipo kiuhalisia.
Bali ni msamiati ulitengenezwa na jamii ili kuwadhibiti watu.

Tunapoiangalia asili kwa namna inavyofanya kazi, tunaona wazi kabisa kushindwa hakupo.

Kwenye eneo moja, panda mbegu za papai na embe.
Siku chache mbegu za papai zitakuwa zimeota, ila mbegu za embe zitakuwa bado. Je embe limeshindwa?

Miezi michache inayofuata, papai litakuwa na matunda, ila embe ndiyo kwanza linaota. Je embe limeshindwa?

Miaka michache baadaye, papai litakuwa linakufa, wakati embe ndiyo kwanza linaanza kuzaa. Je papai limeshindwa?

Rafiki, naamini unaipata dhana ninayotaka uipate hapa.

Tuendelee na mfano kama bado hujaelewa vyema.

Ni saa saba mchana, jua kali lilikuwa linawaka na umeanika vitu vyako. Ghafla linatanda wingu na mwanga wa jua unakuwa hafifu kiasi cha kushindwa kukausha vitu vyako. Je jua limeshindwa?

Rafiki, unajionea mwenyewe hapo jinsi ambavyo msamiati wa kushindwa haupo kabisa kwenye uhalisia.

Hatua ya kuchukua;
Futa neno kushindwa kwenye maisha yako. Wajibu wako ni mmoja tu, kukaa kwenye mchakato.

Tafakari;
Mambo mengi uliyojazwa na kuaminishwa na jamii siyo ya kweli na yamegeuka kuwa kikwazo kwako.
Hoji kila ulichoaminishwa na jamii kwa kuangalia kwenye asili.
Kama hakiendani na asili, ni uongo. Upuuze mara moja na ishi uhalisia.

#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed