#SheriaYaLeo (329/366); Kaa kwenye kundi sahihi.
Dhumuni la makundi mbalimbali ni kukamilisha majukumu, kufanya kazi, kutatua matatizo.
Makundi yanakuwa na rasilimali muhimu ambazo zikitumika vizuri zinakuwa na tija kubwa.
Lakini pia ndani ya kundi huwa kuna ushindani baina ya watu, ambao unaweza kuwasukuma watu kufanya zaidi.
Kundi lenye afya huwa linaweka msisitizo kwenye kazi inayopaswa kufanyika. Linahakikisha rasilimali zilizopo zinatumika vizuri na kwa tija. Kundi la aina hii linaepuka kupoteza muda kwenye michezo ya kisiasa isiyokuwa na tija.
Kundi la aina hii lina uwezo wa kukamilisha mara kumi zaidi kuliko kundi lisilokuwa na afya.
Linatumia vizuri kila kilicho ndani ya watu wake kwa manufaa makubwa.
Unapaswa kuwa kwenye kundi lenye afya, kundi ambalo linatumia vizuri uwezo wako na kufanya makubwa.
Epuka makundi ambayo yanakudidimiza na kaa kwenye makundi ambayo yanakuinua zaidi.
Sheria ya leo; Unapaswa kuelewa kwa kina madhara ya kifikra na kihisia ambayo kundi ulilopo linayasababisha kwako. Kwa kuwa na uelewa huo, utaweza kuchagua kujiunga na kundi linalokuinua zaidi.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji