#SheriaYaLeo (330/366); Geuza upendo binafsi kuwa huruma.

Huwa tunadhani tunawaelewa vizuri watu tunaojihusisha nao.
Maisha yanaweza kuwa magumu na tuna majukumu mengi ya kukamilisha.
Pia tu wavivu na tunapendelea kuwahukumu watu kwa mazoea.

Lakini hayo yote siyo sahihi. Mafanikio yetu kwenye maisha yanategemea sana uwezo wetu wa kuwasoma na kuwaelewa watu vizuri.
Huwa hatuelewi hilo kwa sababu tunashindwa kuona jinsi matatizo tunayokutana nayo kwenye maisha yanavyotokana na kushindwa kuwaelewa watu.
Hilo pia limekuwa linatukosesha fursa nyingi na nzuri maishani.

Hatua ya kwanza ya kuvuka hili ni kutumia silaha kuu ambayo tunayo, ambayo ni huruma.
Ili kuweza kutumia silaha hiyo kwa manufaa, unapaswa kuacha kujiangalia wewe mwenyewe tu na kuanza kuwaangalia wengine.

Isome saikolojia ya watu wengine.
Jua nini kinawasukuma kufanya yale wanayofanya.
Jaribu kuelewa mtazamo wao kwa kuvaa viatu vyao.
Hilo litakuingiza kwenye ulimwengu wa tofauti na kuweza kuzielewa tabia nyingi za watu ambazo hukuwa unaziona.

Sheria ya leo; Ni asili yetu binadamu kujipenda na kujijali sisi wenyewe kuliko wengine. Lengo letu kwenye maisha ni kugeuza mapenzi haya binafsi kuwa huruma ili tuweze kuwaelewa wengine, maana hilo linatusaidia kuchangamana nao vizuri.

#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji