2827; Ung’ang’anizi na upinzani.
Hakuna chochote unachokitaka kwenye maisha yako ambacho utakipata kwa urahisi.
Chochote kile unachokitaka, dunia itakuwekea upinzani mkali kwenye kukipata.
Dunia itahakikisha inakuwekea kila aina ya kikwazo, mradi tu usipate unachotaka.
Njia pekee ya kuvuka upinzani wa dunia ni kuwa na ung’ang’anizi usiokuwa na kikomo.
Unapaswa kuwa na ung’ang’anizi mkubwa kuliko upinzani unaokutana nao.
Hata kama umekutana na ugumu kiasi gani, wewe endelea kupambania kile unachokitaka bila ya kukata tamaa.
Kwenye maisha, wanaofanikiwa ni wale wenye ung’ang’anizi mkali kuliko upinzani wowote wanaokutana nao.
Kama ni rahisi kukata tamaa pale unapokutana na upinzani, jua wazi hutaweza kufanya chochote kikubwa.
Hatua ya kuchukua;
Kwa chochote ulichochagua kufanya, jua wazi kabisa kwamba dunia itakuwekea upinzani wa kila aina. Wajibu wako ni kuwa na ung’ang’anizi mkubwa kuliko upinzani wowote unaokutana nao. Ni ung’ang’anizi huo ndiyo utakaokuwezesha kupata chochote unachotaka.
Tafakari;
Mara zote jiambie; nina ung’ang’anizi mkubwa kuliko upinzani wowote ninaokutana nao. Kisha ng’ang’ana kweli kweli. Ukishaamua nini hasa unachotaka, komaa nacho mpaka ukipate kweli, usikubali kuishia njiani.
#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed