#SheriaYaLeo (333/366); Jifunze kwenye zama zilizopita.
Vile tunavyoishi sasa ni matokeo ya mambo yaliyotokea kipindi cha nyuma.
Mabadiliko yote ambayo binadamu tumeyapitia tangu enzi na enzi, ndiyo yamezalisha yote tuliyonayo sasa.
Huwa tuna tabia ya kubeza zama zilizopita, kwa kuona zimepitwa na wakati.
Kufanya hivyo kunatuzuia tusijifunze.
Lakini pia ni kujitenganisha na mizizi mikuu inayotufanya sisi kuwa binadamu tuliostaarabika.
Unapaswa kujifunza kutoka kwenye zama zilizopita.
Kuwa na mtazamo ambao watu walikuwa nao kipindi hicho.
Na kuiona dunia kwa namna ambayo waliona wao pia.
Hilo litakupa funzo kubwa na kuweza kuyaelewa na kuyathamini mengi yanayoendelea sasa.
Unaweza kufanya hilo kwa kusoma vitabu vya historia na kujenga taswira ya mambo yalivyokuwa kipindi hicho.
Pia unaweza kusoma riwaya za miaka zaidi ya 100 iliyopita na kuipata picha ya kipindi hicho.
Usipoteze mizizi yako ambayo ndiyo inakupa uimara wa kusimama kama mwanadamu. Jifunze kwenye zama zilizopita na utumie vizuri zama tulizopo sasa.
Sheria ya leo; Kuna mengi ya kujifunza kwenye zama zilizopita ambayo yatakufanya uwe bora kwenye zama hizi. Chukua nafasi ya kufanya hivyo.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji