SheriaYaLeo (351/366); Kukikaribia kifo.

Watu wengi huendesha maisha yao kwa mazoea na kupoteza muda kwenye mambo yasiyokuwa na tija.
Ni mpaka pale wanapokutana na hatari ya kifo ndiyo wanayabadili maisha na kuishi kwa tija.

Inaweza kuwa ni kwenye ajali ambayo mtu amenusurika kufa au kupata ugonjwa ambao hawezi kupona.
Katika hali za aina hiyo, mtu anaiona thamani ya maisha ambayo alikuwa anayaishi kwa mazoea.

Unaweza usikutane na hatari hiyo ya kukikaribia kifo, lakini ukiangalia uhalisia wa maisha, wakati wote unatembea na kifo.
Unaweza kukutana na kifo muda wowote, hivyo hilo linapaswa kukufanya uthamini muda uliobakiwa nao hapa duniani.

Usisibiri mpaka unusurike kufa ndiyo uyathamini maisha yako.
Anza kuyathamini sasa, ukijua muda wowote unaweza kuyakosa.

Sheria ya leo; Yaishi maisha yako kama vile umeshakutana na kifo na kunusurika. Kwa njia hiyo utayathamini na kuishi kwa tija.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji