#SheriaYaLeo (356/366); Tumia kifo kuziondoa tofauti.
Kifo ni moja ya vitu vinavyotuleta mahali pamoja wote.
Ni kitu kinachotufanya wote kuwa sawa kwa sababu mwisho wa siku wote tutakufa.
Haijalishi tofauti zetu kwenye maisha, wote njia yetu ni moja, kifo.
Yote tunayobaguana nayo hayana tofauti kwenye kifo.
Kwa kujua hatima hii ambayo inatukabili wote, tunapaswa kuziondoa tofauti zetu na kuwa kitu kimoja.
Tunapaswa kupendana, kuheshimiana na kushirikiana kwa muda huu mfupi ambao tunao hapa duniani.
Kwa kujua wote tutakufa, unapaswa kuwa na huruma kwa wengine badala ya kiburi na majigambo.
Sheria ya leo; tumia uwepo wa kifo kwa wote kama njia ya kuwapenda, kuwathamini na kushirikiana vyema na wengine.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji