#SheriaYaLeo (360/366); Hili nalo litapita.

Sisi binadamu huwa tunapenda sana uhakika wa mambo.
Hilo ndiyo limekuwa linasababisha tukae kwenye mazoea.
Huwa tunataka mambo na hali ziendelee kuwa vile ambavyo zimekuwa.
Ndiyo maana mara nyingi huwa tunasema afadhali ya jana.

Ukweli ni kwamba, kila kitu kinabadilika. Hakuna kitu chochote ambacho hakibadiliki hapa duniani.
Kila dakika inayopita, mambo yanabadilika.
Na hata sisi wenyewe tunabadilika.
Iwe ni mazuri au mabaya, yote yanabadilika.

Mabadiliko ni kanuni ya asili.
Ukiangalia kipindi chote ambacho dunia imepitia, kumekuwa na mabadiliko mengi makubwa.
Lakini tukiangalia muda wetu mfupi hapa duniani, tunaona kama mambo yako vile vile na yataendelea kuwa hivyo hivyo.

Mabadiliko yapo na yataendelea kuwepo. Tuyapokee na kwenda nayo kwa manufaa yetu sote.

Sheria ya leo; Achana na yaliyopita na jisikie ukipelekwa na mkondo wa maisha ambao unabadilika kila wakati. Mabadiliko hayo yanatupa nguvu ya kuweza kufanya makubwa zaidi.

#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji#SheriaYaLeo (360/366); Hili nalo litapita.

#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji