2915; Nenda kauze.
Kwako rafiki yangu mpendwa unayekabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaisha na biashara kwa ujumla.
Kuna njia moja ya uhakika ya kuondoka kwenye changamoto zote zinazokukabili hata kama ni kubwa kiasi gani.
Njia hiyo ni kufanya mauzo zaidi.
Karibu kila changamoto inayokukabili sasa, inaweza kutatuliwa vizuri kabisa kwa kuongeza mauzo zaidi.
Nenda kauze, ndiyo kauli utakayoisikia kwangu mara nyingi kuliko kauli nyingine zote.
Kwa sababu ni hapo kwenye mauzo ndipo penye ukombozi wako.
Kila matatizo na changamoto unazokutana nazo, anza na swali hili; nini nahitaji kuuza zaidi ili kuondokana na hili?
Kaa mahali tulivu ukiwa na kalamu na karatasi na usiondoke mpaka umepata majibu ya uhakika ya swali hilo, majibu ambayo unaweza kwenda kuyafanyia kazi mara moja.
Kinachofanya wengi kushindwa pale wanapokutana na magumu au changamoto ni kusubiri mambo mazuri yatokee.
Nisikilize rafiki yangu, hakuna mambo mazuri yanayotokea yenyewe.
Mambo mazuri yote huwa yanasababishwa.
Unapaswa kuchukua hatua ndiyo mambo mazuri yatokee.
Na hatua za uhakika unazoweza kuchukua zikakuletea matokeo bora kabisa ni kwenda kuuza zaidi.
Mauzo ndiyo silaha yako ya mwisho na ya uhakika pale unapojikuta kwenye magumu.
Hivyo ni silaha unayopaswa kuinoa kila mara, maana inakuchomoa kwenye mengi magumu utakayokuwa umenasa.
Nenda kauze, hakuna gumu ambalo huwezi kulitatua kwa mauzo zaidi.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe