2932; Ndiyo maana unapaswa kufanya.
Rafiki yangu mpendwa,
Pata picha umemwajiri mtu afanye kazi fulani.
Baada ya kumpa majukumu hayo ya kazi, anakuambia hii kazi ni ngumu sana.
Hiyo ni kweli, kazi hiyo itakuwa ngumu ndiyo maana ukatafuta mtu wa kuifanya.
Maana kama ingekuwa rahisi, ungeifanya wewe mwenyewe.
Upande wa pili wa hili ni wewe kulalamika kwamba mchakato wa safari ya mafanikio ni mgumu sana.
Ni kweli, mchakato wa safari ya mafanikio ni mgumu, ndiyo maana ni wachache sana waliofanikiwa.
Na kama unataka kuwa miongoni mwa hao wachache waliofanikiwa, unapaswa kupokea ugumu huo na kuufanyia kazi.
Kupanda mlima ni kazi ngumu, lakini unapofika kwenye kilele, unapata hewa safi, unaona mbali zaidi na hakuna msongamano wa watu wengi.
Mara nyingi vitu tunavyolalamikia, ndiyo sababu tunapaswa kuvifanya. Yaani malalamiko yetu juu ya kitu chochote kile, ndiyo sababu ya kufanya kitu hicho.
Mkwamo wowote unaokutana nao kwenye njia yako, ndiyo njia yenyewe.
Badala ya kukata tamaa na kuacha, unapaswa kusonga mbele na kuvuka mkwamo huo.
Maana huo mkwamo ndiyo sababu ya wewe kufanya.
Na pale unapompa mtu jukumu la kufanya na akalalamika ni gumu, jua hapo hauna mtu sahihi. Tafuta mtu sahihi atakayelipokea jukumu hilo pamoja na ugumu wake na kukupa matokeo unayoyataka.
Watu tunaowabembeleza huwa wanaishia kutukwamisha sana kwenye mambo muhimu kwetu.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ni sababu tosha ya Mimi kufanya kwa msimamo ili kuwa miongoni mwa watu wachache waliifanikiwa.
LikeLike