2936; Safisha kwanza.
Rafiki yangu mpendwa,
Kama unataka kutumia kikokotozi kukokotoa hesabu fulani na ukakuta kikokotozi hicho tayari kina hesabu nyingine, unasafisha kwanza ndipo unaweka hesabu mpya.
Kwa kuchanganya hesabu mpya na za zamani, unapata majibu yasiyo sahihi.
Kabla hujapanda mazao kwenye shamba, unalisafisha kwanza kuondoa magugu. Ukipanda mazao kwenye magugu, hayawezi kuota na kuzalisha vizuri.
Ubao ambao tayari umeshaandikwa inabidi ufutwe kwanza kama unataka kuandika vitu vingine.
Na kama una kikombe kilichojaa maji na unataka maziwa, inabidi ukisafishe kwanza.
Mifano yote hiyo ya asili, inaonyesha jinsi ambavyo kitu chochote kipya hakiwezi kupata nafasi kama kinachanganywa na vitu vya zamani.
Na hilo linaonyesha kwa nini umekuwa hupati matokeo mazuri kwenye hatua mbalimbali unazochukua.
Ni kwa sababu kabla ya kuanza kitu husafishi kwanza.
Unaweka vitu vipya kwenye vitu vya zamani na hapo matokeo yanakuwa magumu kuonekana.
Hii ni kujifunza vitu vipya wakati bado umebeba vya zamani. Maarifa unayojifunza yanakuwa mazuri, lakini yale ya zamani yanakuwa kikwazo kwako kutumia hayo mapya.
Ili unufaike na vitu vipya unavyojifunza futa vile vya zamani unavyojua, kwa kuchukulia kama unaanza upya.
Ni kubaki kwenye mazoea licha ya kujifunza njia mpya bora za kufanya vitu.
Kama bado unaamini njia za zamani ndiyo bora, mpya hazitapata nafasi.
Ili uweze kutumia njia mpya unazojifunza, acha kuamini kwamba njia za zamani ndiyo bora zaidi.
Na pia ni kuajiri wafanyakazi wapya na kuwachanganya na wafanyakazi wa zamani. Mwanzo wataanza kwa kasi kubwa na mabadiliko, lakini baadaye wataishia kuwa kama hao wa zamani.
Unapoajiri watu wapya, waepushe na watu wa zamani au hakikisha watu wa zamani wanakuwa bora kwanza ili wasiwaharibu hao wapya.
Chochote kipya kinachokupa changamoto kwenye maisha ni kwa sababu hukusafisha kwanza kabla ya kukifanya.
Jijengee tabia hii ya kusafisha kwanza na utaweza kuleta mabadiliko yenye tija kwenye maisha yako.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ni kweli kabisa, huwezi kuendelea kusoma kurasa za mbele kwenye kitabu kama bado unasoma ukurasa wa kwanza.
LikeLike
Ni kweli kocha mazoea ya zaman yamekuwa kikwazo sana kwetu kupiga hatua mbalimbali,.
LikeLike
01/01/2024 nitasafisha!!!!!!!! Huwezi kuamini
LikeLike
Mbona mbali sana,
Kwa nini usianze kusafisha mapema?
LikeLike
Shamba kweli lazima lisafishwe kabla ya kuweka mazao Mapya, ndiyo maana kila mwaka tunafunga na kufungua kwa semina,na kweli wengi wao wanaohudhuria semina wanakuwa na kitu cha ziada.
Asante Sana kocha.
LikeLike