2979; Hofu ya mafanikio.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwa kipindi kirefu ambacho nimekuwa najifunza kuhusu mafanikio, nimekuwa na kutana na sababu mbalimbali zinazowazuia watu kufanikiwa.
Moja ya sababu hizo ni hofu ya mafanikio.
Nilikuwa sielewi iweje mtu anayeyataka mafanikio awe pia anayahofia mafanikio?
Sikuwa nalipa sana uzito hilo kwenye sababu za watu kutokufanikiwa.
Ni mpaka pale nilipokutana na mifano halisi ndipo nilipoelewa maana ya hofu ya mafanikio kuwa kikwazo cha kupata mafanikio makubwa.
Tulipoanza programu ya kukuza zaidi mauzo, kuna watu walikuwa hawapo tayari kufanya zoezi la kutafuta wateja wapya kwa wingi.
Nilidhani kinachowakwamisha ni ugumu wa zoezi zima.
Lakini baada ya kufuatilia kina, ndipo nikaanza kupata majibu tofauti, baadhi walikuwa hawafanyi zoezi hilo kwa sababu waliona kama watapata wateja wapya wengi basi watashindwa kuwahudumia vizuri.
Na hapo ndipo nikaielewa ile sababu ya watu kutokufanikiwa kwa sababu ya hofu ya mafanikio.
Kinachojidhihirisha hapo siyo kwamba watu wanakwepa zoezi hilo kwa hofu ya kushindwa (japo hiyo pia ipo), ila kwa sababu ya hofu ya kufanikiwa.
Kwamba iwapo watatafuta wateja wapya na wakafanikiwa kuwapata, basi watashindwa kuwahudumia vizuri.
Unaanza kupata picha hapo na unaanza kuona jinsi ambavyo wewe mwenyewe umekuwa unajizuia kufanikiwa kwa kuhofia kufanikiwa.
Unaweza kumcheka anayekwama kutafuta wateja wapya kwa kujiambia wewe unawatafuta kwa wingi bila kujali, lakini je vipi kwenye kutoza gharama?
Watu wengi wanakwama kuwatoza wateja wao gharama kubwa siyo kwa sababu wanahofia wateja watashindwa kulipa, bali wanahofia kama wateja hao watakubali kulipa gharama kubwa watakuwa pia na matarajio makubwa ambayo hawataweza kuyatimiza.
Unaona tena hapo jinsi hofu ya mafanikio ilivyo kiini cha kushindwa?
Bado haijakufikia? Kuna ambao wanakwepa kuajiri siyo kwa sababu watashindwa kupata watu sahihi wa kuwaajiri, bali kwa sababu wanaona ni kazi ya ziada kuanza kuwafundisha watu, halafu tena kuwasimamia na bado wakosee.
Wapo waliojaribu kuajiri na walipokutana na hayo wakaamua kuachana na zoezi hilo, yote hayo yanatokana na hofu ya kufanikiwa.
Unaweza kujiambia wewe unataka sana mafanikio na hukwamishwi na hofu ya kufanikiwa.
Lakini nataka nikuambie, ukijitafakari kwa ndani, utaona wazi jinsi ambavyo hofu ya kufanikiwa unayo na imekuwa kikwazo kwako.
Nakuambia hivyo kwa uzoefu ambao nimeupata kupitia kufanya kazi na watu wengi, kila mmoja ninapofanya naye kazi kwa karibu, hofu hiyo inajitokeza.
Kuna hata zile fikra za kawaida tu za vipi kama nikiuza zaidi na nikatakiwa kulipa kodi kubwa zaidi ya mapato? Kwa hiyo? Unaona bora uwe masikini na ulipe kodi kidogo kuliko kuwa tajiri na ulipe kodi kubwa?
Au vipi kama nikipata utajiri na watu wakaanza kuniwinda? Ndiyo maana utajiri unakuja na wajibu wake mkubwa, ikiwepo kujilinda kwa gharama kubwa zaidi.
Au kali kabisa, mafanikio yatabadili sana maisha yangu na kuvunja baadhi ya mahusiano yangu. Huwezi kuwa tajiri na kuendelea kuwa na mahusiano mengi uliyokuwa nayo wakati ukiwa masikini. Kitendo tu cha kufanikiwa kitawapoteza wengi wa karibu yako ambao hawajafanikiwa.
Na kubwa kuliko ni zile fikra kwamba, hata hivyo matajiri hawana furaha kama masikini.
Hapo kwanza nicheke, halafu hii tuipeleke kwenye uzembe zaidi kuliko kwenye mafanikio.
Rafiki, imani yangu ni umeipata picha kamili ya jinsi hofu ya mafanikio inavyokuzuia kufanikiwa.
Hatua ya kuchukua hapa ni kuchimba hofu zote za mafanikio zilizo ndani yako na kuhakikisha unaziondoa zisiwe kikwazo kwako kufikia mafanikio makubwa unayoyataka.
Maana bila ya kushughulikia hizo hofu, utakwama licha ya juhudi kubwa unazoweka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ahsante kocha
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Penye hofu kuna mkwamo, haijalishi nijuhudi kubwa kiasi gani inawekwa pale.
LikeLike
Tuivuke hofu kujikwamua.
LikeLike
Kweli mara nyengine khofu yako ndio kikwazo kwako. Nitahakikisha naondoa khofu ili niweze kypata mafanikio
LikeLike
Tusiipe hofu nafasi ya kututawala.
LikeLike
Nashughulikia hofu yangu ya kuogopa kushinda, hasa kuogopa kufanikiwa kupata wateja wengi au wateja wakubwa.
Kuanzia Leo, SIOGOPI TENA MAFANIKIO Bali najifunza jinsi ya kulipa GHARAMA ya kubaki na mafanikio na WAJIBU WA KUTUNZA UTAJIRI.
Hahhaa na Mimi nicheke kwanza matajiri hawana furaha kama masikini nicheke Tena
Kauli za sungura sizitaki mbichi hizi…
Utajiri ndio furaha ya kweli na hakuna masikini mwenye furaha anajitia tuu moyo.
Utajiri siyo dhambi na umaskini siyo utakatifu.
Tutafute utajiri maana umaskini hauhitaji mipango unakuja wenyewe.
LikeLike
Umesema mengi na ya muhimu sana kwenye ujumbe huu.
Tuyazingatie.
LikeLike
Hofu ndio changamoto kubwa kwa wakati wote ndio imefanya kuleta mkwamo mkubwa katika yale ambayo tunayafanya katika ukuaji wetu..
LikeLike
Tuivuke hofu ili kuyafikia mafanikio makubwa.
LikeLike
Hofu ni kikwazo.
LikeLike
Na tusikikubali.
LikeLike
Limenigusa ili Ctoogopa MAFANIKIO
LikeLike
Tuyapende ili tuweze kuyaendea.
LikeLike
Hofu,hofu,hofu, nitaendelea kujifunza zaidi ya kuendelea kikabiliana na hizi.
LikeLike
Vizuri sana, tusiipe hofu ushindi.
LikeLike
Naanza kuchimba hofu zote za mafanikio nilizokuwa nazo,na kiziweka pembeni. Asante sana Kocha.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Huwezi kuwa tajiri na bado ukawa na mahusiano na wengi kama ulivyokua masikini.
LikeLike
Kupanga ni kuchagua.
LikeLike
Nitapambana na hofu zote zinazonizuia kufikia mafanikio yangu!
LikeLike
Vizuri sana, usiruhusu chochote kuwa kikwazo.
LikeLike
Hatua ya kuchukua hapa ni kuchimba hofu zote za mafanikio zilizo ndani yako na kuhakikisha unaziondoa zisiwe kikwazo kwako kufikia mafanikio makubwa unayoyataka.
LikeLike
Hakika, hofu nyingi zimejificha ndani, bila ya kuzichimba huwezi kuzifikia.
LikeLike
Hiki ndicho nakiona kwa wafanyabiashara wengi pale ninapowaeleza kuhusu mfumo wa biashara.Wanakuwa na hofu kuwa itawapasa kuajiri hivyo kutengeneza mwanya wa kuibiwa.
LikeLike
Wanahofia kuibiwa, wanaishia kujiibia wao wenyewe.
Hofu ni mbaya sana na kikwazo kikubwa kwenye safari ya mafanikio.
LikeLike
Hofu ni adui mkubwa wa mafanikio yangu
Napambana kuzishinda hizi hofu ili niweze kufika kwenye mafanikio makubwa ninayotaka kwenye maisha yangu.
LikeLike
Kweli hofu ya kufanikiwa ni kikwazo kikubwa.
LikeLike