2983; Ongeza kasi ili kuwa imara.
Rafiki yangu mpendwa,
Kama umewahi kuendesha baiskeli unajua kitu kimoja, kama inayumba yumba, ili kuifanya iwe na mwendo imara na wa utulivu, unapaswa kuongeza kasi zaidi.
Ndiyo kwa kuiweka baiskeli kwenye mwendo wa kasi kubwa, unaipa utulivu na uimara mkubwa kwenye mwendo wake.
Hivyo pia ndivyo kwenye maeneo mengi ya maisha yetu, kama tunataka uimara, tunapaswa kuongeza kasi zaidi.
Chukua mfano wa biashara, kinachofanya biashara ziwe na changamoto nyingi na hata kufa ni kasi ndogo inayokuwepo kwenye biashara hizo.
Kwa kasi hiyo ndogo, wamiliki wa biashara hizo hujikuta wanasumbuliwa na usumbufu mwingi hivyo kuondoa umakini wao kwenye biashara hizo.
Hilo linatoa mwanya kwa biashara hizo kualika changamoto nyingi na hata kupelekea anguko.
Hata ushindani kwenye biashara, huwa unakuwa mkali kwenye biashara zinazoendeshwa kwa kasi ndogo.
Kasi inapokuwa kubwa, wale wasio imara huwa wanakimbia wenyewe na hivyo kupunguza ushindani.
Lakini pia hilo linaenda mpaka kwenye ukuaji wa timu. Biashara zisizokuwa na timu au ambazo timu yake ni ndogo huwa zinakuwa dhaifu na kwenye hatari ya kushindwa.
Lakini biashara zenye timu kubwa na nzuri, inayofanya kazi kwa mfumo sahihi, inakuwa imara na kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Kinachofanya kasi ilete uimara ni umakini mkubwa ambao mtu anauweka kwenye kitu pale kasi inapokuwa kubwa.
Kasi inapokuwa ndogo, umakini unagawanyika na usumbufu kuingilia.
Lakini kasi inapokuwa kubwa, umakini unakusanywa na usumbufu unawekwa pembeni.
Chochote ambacho siyo imara kwenye maisha yako, jiulize ni kasi gani unayoweza kuiongeza kwenye kitu hicho ili kukifanya imara zaidi.
Ongeza kasi bila kuhofia, kwa sababu kasi hiyo inajenga uimara mkubwa unaochangia ukuaji mkubwa pia.
Kwenye biashara;
Ongeza kasi ya ukuaji,
Ongeza kasi ya kujifunza,
Ongeza kasi ya malengo,
Ongeza kasi ya kuchukua hatua mpya,
Ongeza kasi ya kuajiri,
Ongeza kasi ya kuwahudumia wateja,
Ongeza kasi ya kutafuta wateja wapya,
Ongeza kasi ya kufuatilia wateja,
Ongeza kasi ya kujaribu vitu vipya,
Ongeza kasi ya kuitangaza biashara.
Kasi ni nguvu inayohitajika sana ili kufanya vitu kuwa na uimara mkubwa wa asili.
Wengi huhifia kwamba kasi inakuwa na hatari ya anguko.
Lakini hiyo itatokana na kasi ya kiholela.
Ongeza kasi iliyopangiliwa na utaweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yako.
Kila umapokuwa njia panda na hujui nini cha kufanya, anza kwa kuongeza kasi, itakufanya ujue kwa haraka unachopaswa kufanya na hivyo kuendelea au kubadilika kulingana na hali inayokuwepo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nitaongeza kasi ya biashara ili kuimarisha biashara yangu.
LikeLike
Kasi zaidi inahitajika.
LikeLike
ongezeko la kasi kwenye biashara ni kitu kinachotakiwa sana kwenye biashara kwasasa maana
wateja wana haraka mno kwa kile wanachokuwa wanakihitaji.
hapa ndo nawekeza nguvu kutoa huduma bora na kwa uharaka
asante kocha.
LikeLike
Hasa biashara yako, watu hawana muda wa kuzungushana, ongeza kasi uwapate kwa uhakika.
LikeLike
Ongeza kasi kwenye mauzo nk. Asante Kocha. Kwa ukweli kuna maeneo nimekuwa na kasi ndogo sana hasa kwenye kuajiri nina kila haja ya kuongeza kasi.
LikeLike
Kasi ndogo ni kujichelewesha kwenye hizi zama
LikeLike
Asante kocha,nitaongeza kasi na kukaa kwenye mchakato ili niweze kufikia malengo.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kila umapokuwa njia panda na hujui nini cha kufanya, anza kwa kuongeza kasi, itakufanya ujue kwa haraka unachopaswa kufanya na hivyo kuendelea au kubadilika kulingana na hali inayokuwepo.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Hata kama ni kupotea, bora upotee haraka kuliko taratibu.
LikeLike
Ahsante sana Kocha Dr Makirita Amani kwa makala hii muhimu sana kwenye biashara yangu.
#Naenda kuongeza KASI
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante Kocha, kasi kubwa inazaa umakini mkubwa. Na matunda yake ni uimara.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante sana Kocha
Nitaongeza kasi zote ulizoziainisha kwenye makala hii, bado nipo kwenye kuyumba, sijaridhika na kasi yangu.
LikeLike
Kasi zaidi itapunguza kuyumba.
LikeLike
Asante sana Kocha
Nitaongeza kasi zote ulizoziainisha kwenye makala hii
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Naongeza kasi ya kujifunza,kuweka malengo, kuajiri, kuwahudumia wateja,kutafuta wateja wapya, kufuatilia wateja, kujaribu vitu vipya naweka nidhamu na kuwa mgumu kwangu.
LikeLike
Yatimize yote haya na utapiga hatua kubwa mno.
LikeLike
Kasi zaidi inahitajika kuhakikisha safari inakuwa imara.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
ahsante kocha, nitaongeza kasi zaidi
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ahsante sana kocha nitaongez kasi zaidi ya ukuaji wa biashara yangu
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kinachofanya kasi ilete uimara ni umakini mkubwa ambao mtu anauweka kwenye kitu pale kasi inapokuwa kubwa.
Kasi inapokuwa ndogo, umakini unagawanyika na usumbufu kuingilia.
Lakini kasi inapokuwa kubwa, umakini unakusanywa na usumbufu unawekwa pembeni.
Ahsante sana Kocha.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kasi ndio kitu muhimu zaidi katika ukuaji wa biashara zetu
Asante
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Kasi ni muhimu sana kwenye mchakato wa kibiashara Asante sana kicha nimejifunza zaidi.
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Nimegundua kila kinapoyumba kwenye chochote Ni kutokana na Kasi kupungua. Hivyo nitaongeza Kasi kwenye chochote ninachoweka umakini wangu ili kuwa na utulivu na kuzalisha matokeo Bora.
LikeLike
Nikushukuru sana kocha sasa naenda kuongeza kasi maeneo muhimu yote na kuweza kukua kwa haraka sana
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike