2988; Una machaguo matatu.
Rafiki yangu mpendwa,
Inapokuja kwenye kuajiri kwenye biashara, una machaguo matatu.
Chaguo la kwanza ni kutafuta wafanyakazi ambao tayari ni bora kabisa kisha kuwaajiri hao na wakakupa matokeo makubwa na mazuri sana.
Changamoto ya chaguo hili ni uhaba na gharama, wafanyakazi walio bora ni adimu sana kupatikana na hata wakipatikana huwa wanataka kulipwa mshahara mkubwa, kitu ambacho kitaongeza sana gharama za biashara.
Hili siyo chaguo sahihi kwa biashara ambazo ndiyo zinakua.
Chaguo la pili ni kuajiri watu ambao wana uwezo wa kuwa bora ndani yao, kisha kuwaendeleza ili kuweza kufikia ubora wa hali ya juu na kuzalisha matokeo bora.
Changamoto ya chaguo hili ni kuweza kuwajua wenye uwezo wa kuwa bora na kuwa na uvumilivu wakati wa kuwafanya kuwa bora.
Watu wenye uwezo wa kuwa bora ndani yao ni wale ambao ni wanyenyekevu, wapo tayari kujifunza, ni waaminifu, wachapa kazi na wenye ung’ang’anizi.
Ili chaguo hili lifanye kazi vizuri, lazima uwe na mfumo bora wa kutoa mafunzo endelevu kwa wafanyakazi wako.
Ni lazima uwekeze muda kwenye kuwajenga watu kuwa bora.
Chaguo la tatu ni sala.
Kwenye chaguo hili unaajiri yeyote anayepatikana kwa urahisi, ambaye hana cha kufanya, halafu unasali kwamba unatumaini watu hao watafanya kazi nzuri.
Kwenye chaguo hili unakuwa huchagui walio bora kwa sababu huwezu kumudu na wala huwaendelezi kuwa bora kwa sababu huna mpango wowote wa mafunzo.
Unachukua yeyote rahisi kupatikana na kwenda naye hivyo hivyo bila kufanya mafunzo yoyote.
Matokeo ya chaguo hili huwa ni kuwa na wafanyakazi wasiojiweza, wasiozalisha matokeo na ambao pia hawakai kwa muda mrefu.
Swali ni je wewe umekuwa unatumia chaguo gani kati ya hayo matatu?
Kwa walio wengi, hasa biashara ndogo na za kati, chagua namba tatu ndiyo linatumika sana.
Na hilo ndiyo chanzo cha matatizo na changamoto zote za wafanyakazi kwenye biashara.
Wafanyabiashara wanakuwa hawapo tayari kuwekeza fedha kupata wafanyakazi walio bora au kuwekeza muda kutengeneza walio bora kwa kuwa na mpango wa mafunzo endelevu.
Matokeo yake ni kujikuta wanabaki na wafanyakazi wasiojiweza kwa lolote na wanaokuwa mzigo mkubwa kwa biashara na kuizuia isikue.
Wewe chagua namba mbili, ajiri watu wenye uwezo wa kuwa bora kwa sifa za tofauti walizonazo, kisha wekeza gharama na muda kuyatengeneza kuwa bora kwa mafunzo endelevu utakayokuwa unawapatia.
Kama unataka biashara yako iwe bora, lazima uwe na watu ambao ni bora pia.
Kama huwezi kumudu kuwaajiri ambao tayari ni bora, huna budi kuajiri wenye uwezo wa kuwa bora na kuwatengeneza kuwa bora.
Kamwe usitumie mkakati wa sala na matumaini.
Vitu huwa haviwi vizuri vyenyewe, bali vinatengenezwa kuwa vigumu.
Kama umeajiri ndugu yako ambaye hana kazi ya kufanya halafu huna mpango wowote wa mafunzo kwake, unajua nini biashara yako inakwenda kupata, majanga makubwa.
Mara nyingi changamoto za biashara kuwa ngumu na timu kutokuzalisha vizuri ni za kujitakia kulingana na chaguo tulilofanya.
Kwa vyovyote vile, chaguo namba tatu halifai kwa yeyote makini anayetaka kujenga biashara yenye mafanikio.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Uzuri wa mtu wa familia ni urahisi wa kumpata ila hatari yake ni ubovu wa utendaji na uzalishaji.
LikeLike
Watu wa kuajiri ni wanyenyekevu, walio tayari kujifunza, waaminifu, wachapa kazi na wenye ung’ang’anizi.
LikeLike
Asante kocha kwa somo
LikeLike
Vizuri
LikeLike
vitu huwa haviwi bora vyenyewe bali kwa kutengenezwa kwa gharama
LikeLike
Dah Kocha nimecheka sana chaguo la 3 ambalo wengi wanafanya. Kwa kweli nimekuwa na msimamo wa chaguo la 2.
LikeLike
Nakubali gharama,naajiri watu ambao ni waaminifu ,wavumilivu na ambao wapo tayari kujifunza
LikeLike
Asante sana Kocha Dr. Makirita Amani
LikeLike
Karibu
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Katika machaguo matatu, nitachagua namba mbili. Namba moja ni adimu na wa gharama kubwa. Lakini chaguo namba tatu, sala si sahihi, biashara itadumaa na oengine kufa.
LikeLike
Vizuri, namba mbili ndiyo mpango mzima.
LikeLike
Huwa nachagua namba 2
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante Kwa somo nzuri kuhusu ajira Kwa wafanyakazi wetu
LikeLike
Karibu
LikeLike
Asante Kocha, kiukweli mimi binafsi nilikuwa natafuta wafanyakazi wa chagu la tatu : Sala nikiwa na dhana ya kwamba kazi zangu nyingi niza kutumia nguvu wengi wenye level flani za eleimu hawapendi / hawapo tayari kuzifanya lakini kwa sasa nimekuwa na vitengo tofauti ktk kampuni yangu nimeanza kuajiri wafanyakazi kwa njia ya usahili ( mpaka sasa ninesha fanya usahili mara mbili ) kwa hiyo, ninakuwa kibiashara kwa kuwa na chaguo namba mbili kwani nikisha waajiri ( probation- matazamio ) ni lazima kwa kila anayefanya kazi na mimi awe na kitabu cha Chuo Cha Mauzo cha Kocha Makirita Amani pia nawaingiza staff hao kwenye mafunzo ya chuo cha mauzo na kushiriki ktk semina mbalimbali za Kocha. Mwisho, ninepanga kwa interview ya 3 kuangalia wafanyakazi wazoefu na wanaojua biashara ninayoifanya kwa kina ili niweze kufanya vizuri zaidi.
LikeLike
Vizuri sana, bila kubadilika biashara zetu haziwezi kukua.
LikeLike
Kuajiri walio tayari kujifunza na kuwaendeleza.
LikeLike
Ndiyo mpango mzima
LikeLike
Mtego wa namba tatu(3) ni mrahisi Kuingia, namba mbili(2) ndio chagua bora sana kwa kukuza biashara namba moja(1) yaweza kutumika baadae biashara zikiwa kubwa sana kwa nafasi mahususi.
kwa sasa nakomaa na namba mbili(2)
LikeLike
Sahihi kabisa.
LikeLike
Ktk machaguo matatu,chaguo langu ni namba mbili.asante kocha kwa maelezo haya.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante kocha,nitajitahidi kwenye uchaguzi wa wafanyakazi ambao ni bora sio chaguo namba tatu.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Sahihi katika hili na ni somo zuri sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
Asante Kocha.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Asante Kocha,ngoja nikomae na chaguo no 2.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Chaguo Namba tatu halifai .
Ili kupata mafanikio ni kujitahidi kupata watu toka katika chakuo Namba moja au chaguo Namba mbili.
Asante kocha
LikeLike
Sahihi.
LikeLike
Mie nimeajiri chaguo la tatu. Kuanzia sasahv ndugu zangu ntawafukuza wakafanye wapendacho wao nianze kuajiri level 1 na level2.
Nitajitahidi kuwekeza ili nipate matokeo Bora m makubwa kwenye biashara
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kama umeajiri ndugu yako ambaye hana kazi ya kufanya halafu huna mpango wowote wa mafunzo kwake, unajua nini biashara yako inakwenda kupata, majanga makubwa
LikeLike
Hilo halina ubishi.
LikeLike
Chaguo namba Tatu ni changamoto, kwa sababu ni rahisi na rahisi inaua.
LikeLike
Rahisi haijawahi kumwacha yeyote salama.
LikeLike
Mimi chaguao langu ni namba 2
Asante
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante kocha nitaajiri namba 2.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Hakuna miujiza katika kupata mfanyakazi bora, kumuajiri aliye bora au kutengeneza mfanyakazi mwenye uelekeo wa kuwa bora, zaidi ya hapo ni majanga.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hii ni changamoto kwa wengi. Wengi huenda na chaguo la tatu kwa sababu ya kutojua matokeo yake. Nadhani hapa machaguo ni mawili tu : la kwanza au la pili. Hili la tatu halipaswi kabisa kuwa mojawapo ya chaguo kwa mtu aliye makini.
LikeLike
Hilo la tatu ni chaguo hatari.
LikeLike
Kama nataka biashara yangu iwe bora, lazima niwe na watu ambao ni bora pia.
Nachagua namba 2.
Ahsante sana Kocha.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
kutokana na kuhusisha vitu vingi na dini namba tatu imekuwa ikichukua nafasi kubwa kwenye jamii zetu. Naenda na namba mbili kuchukua hatua zaidi
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante Kocha, hii makala nayo ina ukweli mtupt,
Jibu la Swali hapo juu kibinafsi na kiukweli nilikuwa naajili halafu nawaombea wafanye vizuri.
Lakini kwa sasa nimewaingiza kwenye mafunzo ya mauzo na ninachokiona ndani ya kwa sasa hata MITAZAMO yao IMEANZA KUBADILIKA japo kidogo,
Kwa kuwa lengo langu ni KUJENGA BIASHARA na si KUFANYA BIASHARA basi baada ya muda nitaweza kuajili watu wenye uwezo wa kuwa bora na baadaye wale wa chaguo la kwanza ambao ni bora kabisa,
Asante
LikeLike
Mkakati wa sala umekuwa mwiba kwa wengi. Tunautokomeza kabisa.
LikeLike
Ahsante sana kocha ni kweli tumeboronga sana kwa kuchukua wale wa sala hawa hata utumie mbinu gani hawatakuletea matokeo ni sala tu ili mungu awabadilishe ila kwa sasa ni nachukua no 2 ambao nikiwapa mafunzo wanakuja kwenye no 1 na tena kwa garama ndogo
LikeLike
Kabisa yani,
Hiyo ndiyo kanuni yetu ya BM na CHUO CHA MAUZO, tunachukua namba 2, tunakaa nao na kuwapa mafunzo ya uhakika na wanakuwa namba 1.
Tunatumia gharama ndogo huku pia tukijenga uaminifu mkubwa.
LikeLike
Ukiona vyaelea, vimeundwa, nachagua namba 2.
LikeLike
Vizuri, tufanye uwekezaji kwa watu.
LikeLike