3003; Piga makofi tafadhali.
Rafiki yangu mpendwa,
Wengi wetu tumelelewa kwenye mazingira ambayo hatujafundishwa kutambua, kuthamini na kusifia juhudi na hatua wanazopiga wengine.
Pale tunapoona kuna wengine wamefanikiwa kuliko sisi kwenye jambo lolote lile, tunatafuta sababu ya kubeza uwezo ambao mtu ametumia kupata alichopata.
Na hapo ndipo chuki zote dhidi ya watu waliofanikiwa zinapoanzia.
Watu hutafuta kila namna ya kujifariji kwamba kutokufanikiwa kwao hakutokani na uzembe na uvivu wao, bali mambo ya nje.
Inapoonekana kuna wengine kwenye hali kama zao wamefanikiwa, wanatafuta cha kuonyesha kwa watu hao ambacho siyo sawa.
Utasikia mabaya mengi ya wale waliofanikiwa yakisemwa na wasiofanikiwa.
Sehemu kubwa ya mabaya yanayosemwa huwa hata siyo ya kweli au sahihi.
Yanakuwa ni sehemu tu ya wale walioshindwa kujifariji.
Ukweli ni kwamba, kama kuna mtu amepiga hatua ambazo wewe hujapiga, unapaswa kuwa mnyenyekevu na kujifunza kutoka kwa watu hao.
Unapaswa kuweka pembeni yote yanayosemwa kuhusu watu hao na wewe kuwa na mtazamo chanya wa kujifunza na kuchukua hatua.
Unapokutana na mtu ambaye amefanikiwa kuliko wewe kwenye jambo lolote, unapaswa kupiga makofi na kufurahia kwamba unapata fursa ya kwenda kujifunza vitu ambavyo hukuwa unavijua hapo awali.
Na kama tayari ulikuwa unavijua, bado hujavifanyia kazi kwa uhakika.
Hivyo kukutana na aliyefanyia kazi, inakuwa fursa kubwa na nzuri kwako kujifunza.
Umekutana na mtu ambaye ana utajiri mkubwa kuliko wewe, simama na upige makofi. Kisha jiulize amewezaje kupata utajiri huo?
Achana na hadithi za kwenye jamii kwamba amerithi utajiri, au ametumia njia zisizo halali.
Hata kama kweli hayo yapo, mbona kuna wengine wengi ambao wamepitia hali kama hizo na hawajawa na utajiri?
Lazima ufike mahali ukubali kwamba kuna uwezo wa tofauti ambao mtu anakuwa nao na kuutumia katika kupata matokeo bora.
Umekutana na mtu ambaye amejenga biashara inayojiendesha vizuri na kwa faida, simama na upige makofi. Kisha jiulize amewezaje kupiga hatua hizo.
Kutakuwa na hadithi nyingi kuhusu mtu huyo, kwamba alipata bahati fulani au kuna njia zisizo sahihi ambazo ametumia.
Hata kama hayo yana ukweli fulani, turudi kwenye msingi, kwamba wapo wengi ambao wamepitia hali kama hizo lakini hawajaweza kupiga hatua za aina hiyo.
Hivyo kuna mengi ya kujifunza kwa yeyote aliyepiga hatua kubwa.
Mwisho simama na ujipigie makofi wewe mwenyewe.
Kuna hatua ambazo umeshaweza kupiga mpaka sasa, hatua ambazo wapo wengine wengi waliozishindwa.
Lakini pia kuna magumu na changamoto mbalimbali ambazo umeshapitia, lakini hujakubali ziwe kikwazo kwako kuendelea kuyapambania mafanikio yako.
Kwa hatua hizo ambazo umeshapiga, ni ushahidi dhahiri kwamba utazidi kupata mafanikio makubwa kama utaendelea kukaa kwenye mchakato.
Mafanikio ya aina yoyote ile ni magumu.
Unapokutana na yeyote aliyepiga hatua za mafanikio, kubali, thamini na sifia hatua hizo.
Kisha kuwa mnyenyekevu na jifunze kwa mtu huyo na ukachukue hatua kwa yale unayojifunza.
Kwa kufanya hivyo utaweza kuona fursa zaidi na namna ya kuzitumia kupiga hatua kubwa zaidi.
Je ni jambo gani kwako binafsi unalojikubali na kujisifia kwa hatua ulizopiga kwenye hii safari ya mafanikio?
Tushirikishe kwenye maoni hapo chini ili tuweze kukupigia makofi na kujifunza zaidi kutoka kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nimejifunza kuelewa mchakato wa mafanikio siyo rahisi yanipasa kujitoa na kulipa gharama ili kufikia malengo ninayoyahitaji
LikeLike
Hongera sana Mr Kangalawe
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Jambo ambalo najivunia na nimepiga hatua ni kufanya kazi zangu kwa uaminifu ambao kwenye mazingira yetu ya Tanzania inawashangaza sana wateja wetu.
LikeLike
Hongera sana wakili Zake, mchina wa Mwanza nimekupigia makofi yakutosha
LikeLike
👏👏
Kaa humo, unaweza usipate manufaa makubwa sasa, lakini baadaye yatakuja kwa wingi mno.
LikeLike
Asante sana kocha naomba nikupigie makofi kwanza wewe kwa kuendelea kutupa mafunzo haya ya msingi na bora sana kwenye maisha yetu hongera sana.
Jambo nalojipongeza nalo mpaka sasa japo si kwamba nimefanikiwa sana la hasha ila ni swala la kukaa kwenye mchakato wa mauzo hasa kuwapigia simu wateja amabo hata hawanijui ni kitu ambacho sikuwahi kukifanya kwneye maisha yangu ila sasa nakifanya na ninaona matokeo yake na nayaona matokeo makubwa sana siku zijazo na kinanifanaya najiamini katika kuzungumza na watu nisiowafahamu.
LikeLike
Hongera sana Notbruga
LikeLike
✌️✌️
👏👏
Endelea kukaa kwenye mchakato,
Mambo mazuri yanakuja.
LikeLike
Asante kocha,Jambo kubwa ninalojivunia ni kuweka biashara kwenye mfumo na kukaa kwenye mchakato bila kuyumba.
LikeLike
Hongera sana Mwombeki
LikeLike
👏👏
Endelea kukaa kwenye mchakato bila kuyumba.
LikeLike
Makofi tafadhali kwako wewe mwenyewe Kocha Dr Makirita Amani kwa kuendelea kukaa kwenye mchakato wa Bilionea Mafunzoni.
Kitu ambacho najivunia nacho ni kuendelea kukaa kwenye mchakato wa kuandika tokea nianze mwaka 2016
LikeLike
Hongera sana Mwl Deo..moto hauzimi na ni unaendelea kuuwasha kweli kweli tena kwa shauku kubwa
LikeLike
✌️✌️
👏👏
Tuendelee kukaa kwenye mchakato.
Hakuna namna nyingine.
LikeLike
Ahsante sana Kocha kwa makala Bomba na safi ya Leo,
Mpaka Sasa nimefanikiwa katika kujiwekea AKIBA Kila siku Kwa msimamo bila kuacha.
LikeLike
Hongera sana Mr kandugu, akiba ni eneo ambalo wengi limewashinda kabisa
LikeLike
👏👏
Endelea na hilo bila kuacha.
LikeLike
Kadiri mtu atakapechelewa kuridhika na mafanikio madogo ndivyo atavyopata makubwa jambo ambalo wengi hatuwezi
LikeLike
Nimeielewa vizuri sentensi hii Mr Hassan, hongera sana
LikeLike
Kipi unachojipigia nacho makofi?
LikeLike
Asante sana kocha,jambo Jambo kubwa kwangu ambalo naweza kujivunia kwanza ni kukushkr wewe kuniwezesha kuanzisha biashara na kuniwezesha kukaa kwenye mchakato ,pili kunifanya niuone umuhimu wa kujifunza kila iitwayo Leo,kila siku.
LikeLike
Hongera sana Mr Rwitana
LikeLike
✌️✌️
👏👏
Endelea kukaa kwenye mchakato.
LikeLike
Nimeweza kuvuka liziko la mafanikio kidogo..Leo nina kampuni nayaona matunda.
##Ukweli ni kwamba, kama kuna mtu amepiga hatua ambazo wewe hujapiga, unapaswa kuwa mnyenyekevu na kujifunza kutoka kwa watu hao.
Unapaswa kuweka pembeni yote yanayosemwa kuhusu watu hao na wewe kuwa na mtazamo chanya wa kujifunza na kuchukua hatua.
#Najifunza mengi kutoka kwa wana BM wenzagu
LikeLike
👏👏
Safari ndiyo kwanza imeanza.
LikeLike
Jambo niinalo jivunia ni kufabya kazi kwa viwango, kuna wateja wenye kiu ya viwango vya juu, lakini kwa mazingira yetu wengi wa wale wanao ahidi hawatekelezi viango hivyo.
LikeLike
👏👏
Usishushe viwango vyako kwa ajili ya wengine.
Endelea kusimamia viwango hivyo.
LikeLike
Asante Kocha,
Nimejijengea tabia bora sana kuweza kuamka mapema na kuingia kulala mapema pia. Hii imenifanya masaa yangu 24 yawe na tija kubwa. Ninatumia muda wangu kwa ufanisi mkubwa.
LikeLike
👏👏
Endelea na utaratibu huu.
LikeLike
Jambo ninalojivunia ni kutumia muda wangu karibu wote kwenye mambo ya msingi na kuepuka kufuata mkumbo.
Najifunza kwa yeyote aliyenizidi kwa chochote.
LikeLike
👏👏
Endelea kujali sana muda, ndiyo maisha yenyewe.
LikeLike
Ninajikubali kwa Hatua hii ya kuweka akiba na kuwekeza kwa msimamo bila kuacha.
LikeLike
👏👏
Endelea na msimamo huo.
LikeLike
Kujifunza kutoka Kwa waliofanikiwa ni fursa nzuri ya wewe kufanikiwa
Asante
LikeLike
Makofi yako unajipigia kwenye nini?
LikeLike
Asante Kocha, jambo la kwanza najivunia kuwa na Kocha ambaye anapenda kufanya kazi zake kwa ubora wa hali ya juu hongera sana Kocha. Nashukuru Kocha umeniwezesha na kunijengea hamu ya kupenda kusoma na kuandika kila siku kwa sasa nina mwaka moja tangu nianze kuandika kwenye blog. Na pia nimeweza kusoma vitabu kadhaa ambapo hapo mwanzoni singeweza kusoma nikiwa peke yangu bila Kocha. Na pia muhimu ni jambo la uwekezaji,kuamka mapema na kukaa kwenye mchakato. Asante sana Kocha nitaendelea kukaa kwenye mchakato bila kuacha.
LikeLike
✌️✌️
👏👏
Endelea kukaa kwenye mchakato.
LikeLike
Gharama muhimu katika kufikia mafanikio yeyote makubwa
LikeLike
Makofi unajipigia kwenye nini?
LikeLike
Asante sana kocha kwa makala hii nzuri ya kusimama na kupiga makopfi.
Ni kweli kuwa watu waliofanikiwa huwa wanasemwa vibaya na watu wasiofanikiwa kuhusu mafanikio yako, Mimi nitasimama daima na kuwapigia makofi katika mafanikio yao na kutaka kujifunza zaidi kutoka kwao.
Kwa sasa naweza simama na kujipigia makofi kwa kuwa na mtazamo chanya wa kuanzisha na kujenga biashara yangu mwenyewe kupitia maarifa ninayoyapata kwenye kisima cha maarifa,
Asante sana kocha
LikeLike
👏👏
Endelea kusimama imara katika kujenga na kukuza biashara.
LikeLike
Jambo ambalo ninajivunia katika maisha yangu ni kuwa na kiongozi anayeniongoza kupata mafanikio na kiukweli kama siyo yeye kuniwezesha kukaa kwenye mchakato ningekua kama tu wauzaji wengine na kwa kukaa kwenye mchakato nimekua naamka usiku na kutembelea watejal Mimi najivunia sana
LikeLike
👏👏
Endelea kukaa kwenye mchakato.
LikeLike
👏👏👏👏 mengi kwako Kocha. Umekuwa rafiki na Kocha bora sana kwangu.
Mimi najipigia makofi kwa kuendelea kukaa kwenye Mchakato Kamili Wa Bilionea Mafunzoni Kwa Msimamo.
LikeLike
✌️✌️
👏👏
Endelea kukaa kwenye mchakato.
LikeLike
Kumsifia aliefanikiwa ni ngumu kama hauna mtazamo chanya.
LikeLike
Na ndiyo maana wengi hawafanikiwi, maana chuki zao kwa waliofanikiwa zinayakimbiza mafanikio.
LikeLike
Jambo ambalo ninaweza kujivunia na kujipigia makofi .
Kuwa na kocha pia kuendelea kukaa katika mchakato
Utakaonifikisha kwenye uhuru wa fedha pia uhuru wa mda.
LikeLike
👏👏
Endelea kukaa kwenye mchakato.
LikeLike
Makofi kwa kocha kwa Makala Mfululizo unazoandika na kushirikisha Maarifa bila kuchoka na kuhimiza watu kukaa kwenye mchakato na kutuvumilia pale tunapojisahau. Makofi kwangu kwa kuweza kuwezeka UTT kwa kila kipato ninachopata na kuweza kununua HISA za CRDB kila wiki zisipungua za 50000 kwa mwaka wa pili mfululizo.
LikeLike
✌️✌️
👏👏
Endelea na mpango huo wa uwekezaji.
LikeLike
Najivunia kwamba nimeweza kuandika vitabu zaidi ya 15 ambavyo watu wengi wanabaki kuniuliza nimewezaje kuviandika
LikeLike
👏👏
Endelea kuandika.
LikeLike
Asante Kocha,
Kwanza nakupigia makofi wewe kwa kufanya vizuri kwenye nidhamu na kuweka kazi.
Najipigia makofi kwa kuweza kutambua kitu kimoja muhimu cha kufanya katika uhai wangu. Kuwaambia watu kuhusu uwezo wao na kuwasaidia ili wauumshe kuweza kuishi maisha wanayostahili
LikeLike
✌️✌️
👏👏
Endelea kuamsha uwezo mkubwa uliolala ndani ya watu.
LikeLike
Jambo ambalo najivunia ni kuwa na Uvumilivu wa changamoto ninazopitia na kuwa kwenye Jamii ya Wana Kisima Cha Maarifa ambao wanaamini katika kazi, kujituma, ubunifu na kuheshimiana.
Ni fursa nzuri ya kukua kiakili na fikra kubwa.
LikeLike
👏👏
Endelea na mapambano, kukata tamaa ni mwiko.
LikeLike
Kuendelea na Biashara pamoja na magumu ninayopitia
LikeLike
Safi sana, mapambano lazima yaendelee.
LikeLike
👏👏👏 Makofi kwako Kocha kwa kuendelea kutusimamia kwa ukaribu sana katika mchakato wa BM na KCM bila kuchoka. Kila siku unakuja na ubunifu mpya, hali inayopelekea BM , Chuo cha mauzo na KCM kisizoeleke wala kupoa na kuboa.
👏👏👏Kwa upande wangu nijipongeze, nimefanya mengi chini ya usimamizi wako, hasa kwenye uandishi wa vitabu.
Asante
LikeLike
✌️✌️
👏👏
Endelea kukaa kwenye mchakato.
LikeLike
Kwanza nikupigie makofi wewe mwenyewe Kocha,kuwa na nidhamu kali ya kutenda.Umekuwa mfano bora kwangu kupita kiasi na natamani nijaliwe angalau robo ya nidhamu uliyokuwa nayo. Binafsi najishukuru kwa kufanya uwekezaji katika kilimo cha Mkonge kumiliki karibia heka 100 nilizopanda kwa kipindi. kifupi tangu 2019,bila KCM nisingeweza kufanya kazi hii isiyofurahisha na iliyojaa jasho na damu.
LikeLike
✌️✌️
👏👏
Endelea na uwekezaji.
LikeLike
Kwanza nikupigie makofi wewe mwenyewe Kocha,kuwa na nidhamu kali ya kutenda.Umekuwa mfano bora kwangu kupita kiasi na natamani nijaliwe angalau robo ya nidhamu uliyokuwa nayo. Binafsi najishukuru kwa kufanya uwekezaji katika kilimo cha Mkonge kumiliki karibia heka 100 nilizopanda kwa kipindi. kifupi tangu 2019,bila KCM nisingeweza kufanya kazi hii isiyofurahisha na iliyojaa jasho na damu.
LikeLike
Kocha , mimi nakupigia makofi mengi sana kwa kuwa msomaji na mwandishi bora wa vitabu.
Kwa upande wangu, nipigieni makofi kwa kuwa mwandishi wa vitabu licha ya kubanwa na majukumu ya kikazi. Watumishi wengi wa serikali wa level yangu hawana muda wa kusoma na kuandika vitabu. Mimi ni mmoja wa watumishi wa serikali wachache Tanzania waliofanikiwa kuandika vitabu sita hadi sasa.
LikeLike
✌️✌️
👏👏
Endelea na uandishi.
LikeLike
Jambo kubwa nililofanikiwa ni kuvunja tabia ambazo hazikuwa sahihi Kwa mafanikio yangu.
LikeLike
👏👏
Endelea kukaa kwenye tabia mpya kwa msimamo.
LikeLike
Asante kocha kwa makala hii nzuri na hongera kwa mafunzo unayotupatia kila siku. Kwa upande wangu najipongeza kwa Kukaa kwenye mchakato na kuweka akiba UTT kiasi kisichopungua laki moja kila mwezi.
LikeLike
✌️✌️
👏👏
Vizuri sana, endelea kukaa kwenye huo mchakato.
LikeLike