3004; Malengo na sababu.
Rafiki yangu mpendwa,
Huwa tunachukulia wanaoshindwa kwenye maisha kama watu ambao hawana malengo yoyote.
Na wanaofanikiwa kwenye maisha tunaona ndiyo wenye malengo.
Kwa kifupi tunachodhani ni tofauti ya wanaoshindwa na wanaofanikiwa ni malengo.
Lakini huo siyo ukweli, karibu kila mtu ana malengo fulani.
Malengo hayo yanaweza kuwa madogo au makubwa, lakini yanakuwepo.
Ukweli ni kwamba, kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa siyo malengo bali ni sababu.
Wanaofanikiwa ni wale wanaokuwa na sababu kubwa na nyingi za kufanya kile wanachopaswa kufanya.
Ni sababu hizo ndiyo zinazowawezesha kuendelea na safari hata pale wanapokutana na magumu au changamoto mbalimbali.
Japokuwa watu wote wanakuwa na malengo, msukumo wa kufikia malengo hayo haufanani kwa watu wote, hata waliopo kwenye eneo moja na wanafanya kitu kimoja.
Sababu za kwa nini mtu afanye kitu zina maana na mchango mkubwa kwa watu kuweza kuyafikia malengo yao.
Nietzche aliwahi kunukuliwa akisema; mtu mwenye kwa nini kubwa kwa kile anachotaka anaweza kukabiliana na changamoto yoyote anayokutana nayo.
Ni zile sababu za msingi ulizonazo ndizo zinazokusukuma kufikia malengo yako.
Sababu pia zinakupa nguvu ya kuweza kuyapambania malengo uliyonayo.
Nikikuambia ubebe mfuko wa sementi wenye kilo 50 na ukimbie nao kwa umbali fulani utaona hilo ni zoezi gumu na usiloweza.
Lakini ikitokea mtu wa karibu yako, mwenye kilo 50 anaumwa na anatakiwa kuwahishwa mahali kwa haraka, utakuwa tayari kumbeba na kukimbia naye.
Hapa tunaona jinsi ambavyo sababu inakupa nguvu za kuweza kuvuka magumu yote.
Watu wanaoweka malengo na kushindwa kuyafanyia kazi, siyo kwa sababu malengo hayo siyo sahihi, ila ni kwa sababu wanakosa sababu za kuwasukuma.
Chukua mfano wa zoezi la kuwapigia simu wateja. Watu wengi huwa wanaleta visingizio mbalimbali kwa nini zoezi hilo haliwezekani.
Lakini kama kuna kitu wanakipata moja kwa moja kwa kuchukua hatua, wanapata msukumo wa kuchukua hatua.
Zipi sababu zako wewe kufikia malengo yako?
Kama ambavyo tumeona, malengo kila mtu anayo. Ila sababu za kufikia malengo hayo ndiyo zinatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa.
Swali ni je wewe ni sababu gani zinazokusukuma kwenye malengo yako makubwa?
Nini kinakufanya uwe tayarj kuteseka katika kuyafikia malengo yako?
Shirikisha kwenye sehemu ya maoni hapo chini.
Watu wanaweza kufundishwa na kusaidiwa jinsi ya kuweka malengo yoyote makubwa waliyonayo.
Lakini hakuna mtu anaweza kupewa sababu za kwa nini afikie malengo fulani.
Sababu huwa zinaanzia ndani ya mtu mwenyewe.
Na kama ndani hakuna sababu za msingi kwa mtu kupambania malengo yake, hakuna namna ataweza kuyafikia.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ahsante sana kocha, napata msukumo wa kupambania malengo yangu ni kwasababu nauchukia sana umasikini
LikeLike
Kinachotofautisha waliofanikiwa na wasiofanikiwa ni Ile sababu ya kufanya. Waliofanikiwa wanayo sababu kubwa na tamaa ya kupata zaidi.
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike
Pambana sana, kila unapotaka kukata tamaa jikumbushe jinsi umasikini unavyotesa bila ya huruma.
LikeLike
Napata msukumo wa kufikia malengo yangu kwa sababu ya alama ninayotaka kuacha duniani
LikeLike
Safi sana,
Kila unapotaka kukata tamaa kumbuka alama kubwa unayotaka kuacha hapa duniani.
LikeLike
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani, sababu kubwa ya kuendelea kujisukuma ni kuwasaidia watu kupitia kile nachofanya ili kuifanya dunia kuwa sehemu bora na salama ya kuishi kwa kila mmoja wetu.
LikeLike
Vizuri sana,
Kila ukitaka kukata tamaa angalia ni watu wengi kiasi gani utakuwa umewaangusha.
LikeLike
Napata sababu ya kupambania malengo yangu yangu kwa sababu ni kupitia kufikia malengo ndio naweza kutoa mchango chanya kwa wengine.
LikeLike
Vizuri sana, kumbuka jinsi wengine wanavyotegemea unachofanya ili usikate tamaa.
LikeLike
Ahsante sana kocha.
Malengo ninayoweka Kila siku ni Kwa ajili ya kufikia SABABU yangu kubwa ya kuvunja umasikini wa familia yetu. Hichi kitu kinanifanya nijione sitakuwa na thamani ikiwa tu nitashindwa kukifanya.
👏👏👏
LikeLike
Safi sana, kumbuka umasikini usivyo na huruma na hilo likusukume kuendelea na mapambano.
LikeLike
Nataka kufikia malengo yangu ya kuwa Bilionea Kwa sababu zifuatazo.
Kupata uhuru Wa fedha na muda niweze kumudu chochote ninachokitaka Kwa muda wowote ninaoutaka bila kuwa na kikwazo Cha muda Wala fedha.
Nahitaji kuwasaidia wengi, kutoa thamani kubwa Kwa wengi na kuacha alama kubwa duniani.
nataka kufikia ndoto zangu Kubwa na kuonesha Dunia inawezekana kupambania ndoto na kuzifikia.
LikeLike
Vizuri sana, jikumbushe haya kila mara ili usije kukata tamaa na kuishia njiani.
LikeLike
Sababu kubwa niliyo nayo kwenye kile nninachokifanya
-Nikufikia uhuru wa kifedha kwa kufikia hatua ya kuzalisha bidhaa zangu mwenyewe.
-Nauchukia umaskini sana mana umaskini unakosesha raha na unadhalilisha.
-Nataka kupitia ninachokifanya niweze kubadili maisha ya watu wengine kuwa bora na yenye maana.
-Nataka kufanikiwa ili kuwaonyesha wengine hakuna mtu aliezaliwa kuwa maskini kila mtu ni tajiri kama akiamua kuwa tajiri.
LikeLike
Safi sana, sababu hizi ziwe kwenye fikra zako muda wote ili mawazo ya kukata tamaa yasikujie.
LikeLike
Kwa nini kubwa niliyonayo itanisaidia kufanikisha malengo makubwa niliyonayo.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Niko tayari kuteseka kwa sababu nataka kufikia uhuru wa kifedha na muda na pia kutoa mchango wangu kwa wengine ili nao wafikie uhuru wa kifedha na muda
LikeLike
Vizuri sana, jikumbushe hili kila mara ili uweze kuendelea na safari.
LikeLike
Asante Kocha,
Sababu ya Kupambana kufikia malengo yangu ni Uhuru wa kipato, nisiwe tegemezi kwa wengine nguvu zikiniishia.
LikeLike
Safi sana, jikumbushe hili mara zote ili upambane zaidi.
LikeLike
Sababu kuwa ya kuwa Bilionea ni uhuru wa kifedha, kuwa na uhakika wa kipato Ata kama sifanyi kazi, kutoa kwa wengine ili kuleta maana ya maisha na Kuwaonyesha Watu wengi kwenye jamii wanaomaini na mitazamo hadi kuwa haiwezekani.
LikeLike
Vizuri, kumbuka haya kila mara ili usikate tamaa.
LikeLike
Sababu kubwa ya Mimi kufikia malengo yangu makubwa ni kuacha Alama hapa duniani
Asante
LikeLike
Vizuri,
Hakikisha alama unaiacha kweli.
LikeLike
Asante sana kocha, nitaendelea kuwa na kwa nini kubwa,maana hadi sasa natambua nakuelewa maana ya kuwa na kwanini kubwa ktk kuzitimiza ndoto zangu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Sababu kubwa ya mimi kufikia malengo yangu makubwa ni kuwasaidia wengine na kuwashuhudia kuwa inawezekana.
LikeLike
Vizuri, ukitaka kukata tamaa, angalia wengi watakaokosa msaada wako.
LikeLike
Sababu ya Mimi kufikia malengo yangu makubwa baada ya kujua kusudi langu na Kwa Kwa nini Nipo hapa duniani ni kuacha Alama
Asante
LikeLike
Sababu kubwa ni moja tu kwa Ajili ya wengine
LikeLike
Vizuri, waangalie wengine kabla hujaacha.
LikeLike
Sababu kubwa nilizonazo ni
1. Nauchukia Sana Umasikini maana ni dhambi kubwa
2. Nataka Uhuru wa Kifedha niweze kufanya Mambo mengine ya kijamii bila Hofu ya kipato.
3. Nataka maisha yangu yawe na Thamani na maana kwa kusudi la kuumbwa kwangu.
Nausaka Ubilionea Kama pumzi au uhai.
LikeLike
Safi sana,
Tumia adha ya umasikini kama msukumo mkubwa kwako kufanya.
LikeLike
Sababu nzuri zinatupatia nguvu ya kufanya yale yaliyobora sana, unazo sababu za kukaa kwenye mchakato wa BM.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ahsante sana Kocha Dr. Makirita Amani.
Sababu zangu mimi ni;
Kusaidia wengine kuwa na maisha bora kupitia ninachofanya.
Kuwa na uhuru wa kifedha.
LikeLike
Vizuri sana, watumie hao wengine kama msukumo wa kuendelea kufanya.
LikeLike
Asante Kocha,sababu kubwa ya mimi kuteseka ni kutaka kufanya makubwa,na kuonyesha wengine kuwa inawezekana.
LikeLike
Vizuri, kabla hujakata tamaa jiulize wangapi utawakatisha tamaa.
LikeLike
Asante Kocha kwa makala nzuri.
Malengo kila mtu anayo ila sababu za kufikia malengo hayo ndio zinamtofautisha aliyefanikiwa na aliyeshindwa.
Nitaweka sababu kubwa ili niweze kufanikiwa katika malengo yangu.
Asante
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ninapata msukumo wa kuyapambania Marengo yangu kwa sababu ninaamini kabisa ninauwezo wa kuyafikia na nitafikia. Asante Sana kocha kwa makala Bora kabisa.
LikeLike
Vizuri sana na kila la kheri.
LikeLike
Jinsi kwanini kubwa inavyomsukuma mtu kufanya makubwa.
LikeLike
Kwa nini yako kubwa ni ipi?
LikeLike
Nafanyia kazi malengo yangu mpaka kieleweke. Uwezo ninao na sababu kkubwa za kunisukuma zipo
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike