3011; Unaweza kufanya zaidi.
Rafiki yangu mpendwa,
Ukiwa ardhini na ukatazama angani, unaona anga au mawingu kama ndiyo ukomo.
Lakini ukipata njia ya kupanda juu zaidi, unagundua ukomo ulioona ukiwa chini siyo mwisho, bali unaweza kwenda zaidi na zaidi.
Hivyo ndivyo ilivyo kwenye mambo mengi ya maisha, ukomo unaokuwa unauona siyo halisi, unaweza kwenda zaidi ya ukomo huo.
Pale unapoona umefika mwisho wa ufanyaji, tambua kwamba unaweza kufanya zaidi.
Pale unapojiona umechoka kufanya kile unachofanya, bado unaweza kuendelea kufanya zaidi.
Asili huwa haina uhaba wala ukomo.
Ukomo wowote tunaouona ni wa kufikirika, yaani umeanzia kwenye fikra zetu wenyewe.
Hatua ya kwanza ya kuweza kufanya makubwa kwenye maisha yako ni kuamini bila ya shaka yoyote kwamba unaweza kufanya zaidi.
Haijalishi kwa sasa unafanya kwa kiasi gani, jua unaweza kufanya zaidi.
Haijalishi ni juu kiasi gani umeshafika, jua unaweza kwenda juu zaidi.
Pale unapokuwa umechoka na kuona umefika mwisho, jua hapo ndiyo kwanza unaanza.
Ukiwa tayari kwenda hatua ya ziada bila ya kukubaliana na ukomo wowote, utaweza kufanya makubwa.
Dunia imejengwa na wale waliokataa kukubaliana na ukomo unaowazuia wengi. Ni wale wanaokuwa na picha ya tofauti na kung’ang’ana nayo bila kukubali kushindwa ndiyo wanaoweza kufikia picha hiyo.
Ipo kauli maarufu inayosema; ‘Watu wa kawaida huwa wanaenda na dunia inavyoenda, watu wasio wa kawaida huwa wanailazimisha dunia iende vile wanavyotaka wao. Hivyo basi, maendeleo yote hapa duniani yanatokana na watu wasio wa kawaida.’
Usikubali kufuata mkumbo kwenye maisha, utajikwamisha kwa mengi sana unayotaka kufikia.
Jua kabisa ya mwamba;
Ndoto zozote kubwa ulizonazo zinawezekana.
Hatua zozote ambazo umeshapiga mpaka sasa unaweza kupiga
Na chochote ambacho umeshafanya, unaweza kufanya zaidi.
Kwa kifupi ni kwamba hakuna ukomo wala kikwazo chochote kinachoweza kukuzuia kupata kile unachotaka.
Ukomo pekee wenye nguvu ya kukuzuia wewe usipate matokeo unayotaka ni wa ndani yako mwenyewe na siyo nje.
Kama kuna vitu unataka kupata ila hujakipata mpaka sasa, jua ni wewe mwenyewe unajizuia.
Anza kwa kuvunja ukomo uliojiwekea mwenyewe ili uweze kufanya makubwa zaidi.
Haijalishi umefika ngazi gani, unaweza kufanya zaidi na kupiga hatua kubwa zaidi.
Chochote unachotaka kipo ndani ya uwezo wako kukipata.
Ni kuamini bila ya shaka yoyote kwamba unakipata,
Kisha kuchukua hatua stahiki ili kuweza kukipata.
Mara zote nenda hatua ya ziada ili uweze kupata kile unachotaka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
usikubali kufuata mkumbo utajikwamisha kwa mengi unayotaka kuyafikia.
Dunia hii unahitaji kuwa mtu ambaye si wa kawaida unaeweza kuipeleka dunia vile unavyotaka wewe.
LikeLike
Mara zote nitaenda hatua za ziada ili niweze kupata ninachokitaka, kwani hakuna ukomo.
LikeLike
Asili huwa haina uhaba wala ukomo.
Ukomo wowote tunaouona ni wa kufikirika, yaani umeanzia kwenye fikra zetu wenyewe.
LikeLike
Ninaweza kufikia ndoto zangu. Hakuna kinachoweza kunizuia mimi kufanya hilo
LikeLike
Hakuna ukomo kwenye jambo lolote lile, ukomo ni pale utakaposhindwa kwenda zaidi na kutokutuma uwezo wako wa ndani vizuri.
LikeLike
Dunia haina uhaba. Uhaba uko kwenye fikra zetu. Tutafute taarifa na maarifa sahihi, kwayo tutatimiza ndoto zetu kubwa tulizojiwekea.
LikeLike
Chochote ninachotaka kiko ndani ya uwezo wangu.
LikeLike
Hakuna ukomo katika kufikia ndoto ninazotaka
LikeLike
ahsante kocha.
fikira ndio kila kitu. chochote unachokiona kilianza kutokea kwenye fikira ndio kikatokea kwenye uhalisia.
AFANDEA SELE ALIWAI KUSEMA ” ALIWAZALO MJINGA NDILO LINALO MTOKEA”
LikeLike
Unaweza kupata chochote unachotaka kama utakwenda hatua za juu zaidi
Asante
LikeLike
Asili ina utele usio na kikomo.
LikeLike
Naamini bila ya shaka yoyote kuwa, chochote ninachokitaka kipo ndani ya uwezo wangu na naweza kukipata.
LikeLike
Kinachotakiwa ni kuamini bila wasiwasi wowote kuwa naweza kukipata na kisha kuchukuwa hatua zinazotakiwa ili kuweza kukipata.
Natakiwa kwenda hatua ya ziada ili kupata ninachotaka maana kipo ndani ya uwezo wangu.
LikeLike
Mara zote nitaenda hatua ya ziada ili kupata kile ninachokitaka
LikeLike
Naondoa ukomo ili nipige hatua zaidi
LikeLike
Chochote unachotaka kipo ndani ya uwezo wako kukipata.
Ni kuamini bila ya shaka yoyote kwamba unakipata,
Kisha kuchukua hatua stahiki ili kuweza kukipata.
Mara zote nenda hatua ya ziada ili uweze kupata kile unachotaka.
Ahsante sana Kocha.
LikeLike
Nitahakikisha ninaenda hatua zaidi ninapotaka kupata ninachokitaka. Najua wazi Dunia haina ukomo na mie sikati tamaa kuufikia Ubilionea wangu 2030.
LikeLike
Ukomo ni kama kona ukifika mwisho wa kona ni mwanzo wa kona nyingine hivyo twende hadi mwisho ili tuanze mwanzo wa hiyo kona nyinvine hiyo ndiyo njia pekee ukitatua tatizo unaanza kutafuta tatizo lingine
LikeLike
chochote nakitaka kipo ndani yangu sio nje
nashukuru kocha kwa hilo naendelea kujitafuta mpaka nipate ninachotaka.
LikeLike