3017; Rudia rudia.
Rafiki yangu mpendwa,
Ni kanuni na sheria ya asili kwa vitu kujirudia rudia kwa muda mrefu bila kuchoka wala kukata tamaa.
Jua huchomoza na kutua kila siku, majira ya mwaka hujirudia kila mwaka.
Na hata kwa miili yetu, kula, kujisafisha na mengine muhimu huwa tunayarudia mara kwa mara.
Lakini sasa, cha kushangaza ni namna tunavyotegemea mambo mengine kwenye maisha yetu yatokee baada ya kufanya tu mara moja.
Tunataka kupata matokeo makubwa kwa kufanya kitu mara moja.
Na hilo halipo kabisa, kitu kinachopelekea watu wengi kukwama kupata kile wanachotaka.
Chochote kile unachosema au kufanya, unapaswa kukirudia rudia mara nyingi bila ya kuchoka.
Ni kupitia marudio yasiyo na ukomo ndiyo unakielewa kitu kwa undani na kuweza kukifanya kwa viwango vya juu kabisa.
Ushindi kwenye jambo lolote lile kwenye maisha yako hauanzii kwenye matokeo unayopata, bali unaanzia kwenye msimamo unaokuwa nao kwenye kurudia rudia kwa muda mrefu bila kuchoka.
Mara nyingi sana matokeo huonekana kuja yenyewe tena bila ya kuweka nguvu kubwa.
Lakini unapochunguza kwa kina, ndiyo unagundua nguvu kubwa ya kurudia rudia inayokuwa kwenye kila jambo.
Kama unataka kuhusianishwa na kitu, kiongelee na kukifanya mara kwa mara.
Kama unataka kujulikana kwa kitu fulani, kizungumzie na kukifanya kila siku.
Na kama unataka kuwa mtu pekee anayejulikana kwa kitu fulani, kizungumzie na kukifanya mara nyingi kwenye kila siku yako.
Tafuta ujumbe wako mkuu na mchakato unaoufuata ili kufika kule unakotaka kufika, kisha rudia mara kwa mara bila kuchoka.
Marudio yana nguvu kubwa ya kuleta matokeo yoyote makubwa ambayo mtu anayataka.
Lakini hayapaswi kuwa marudio ya mazoea, bali marudio ya kuboresha kulingana na matokeo yanayopatikana.
Hakuna mafanikio yanayotokana na kufanya kitu mara moja tu.
Huli mara moja ukashiba milele,
Huogi mara moja ukatakata milele.
Hayo ni mambo unayorudia kuyafanya kila siku bila kuchoka, kwa sababu ni muhimu.
Ili uweze kurudia rudia kitu mara kwa mara lazima ukipende na kukikubali sana.
Lazima kiwe ndiyo kipaumbele cha kwanza kwako, kama ilivyo pumzi.
Lazima uwe tayari kufanya bila kuhesabu umefanya mara ngapi.
Ni lazima uzame kwenye kitu na kitu hicho kiwe sehemu ya maisha yako ndiyo utaweza kukirudia rudia bila kuchoka.
Mara nyingi watu wanashindwa kwenye maisha siyo kwa kushindwa kufanya vitu fulani, bali kwa kushindwa kurudia rudia kufanya kwa wingi bila kuchoka.
Binadamu huwa tunachoshwa haraka na marudio ya vitu vilivyo muhimu, lakini huko ndipo penye nguvu ya kupata matokeo makubwa sana.
Mpango kamili wa mafanikio ni;.
Moja, kujua kwa hakika kile hasa unachotaka kupata.
Mbili kujua mchakato unaopaswa kuutumia kupata hicho unachotaka.
Na tatu kukaa kwenye mchakato huo kwa kurudia rudia bila kuchoka.
Kwa kila matokeo unayoyapata, yatathmini kisha boresha yale unayofanya na endelea kufanya bila kuchoka.
Ugumu wa mafanikio haupo kwenye vitu vikubwa unavyopaswa kufanya.
Bali upo kwenye marudio ya vitu unavyopaswa kuvifanya.
Kuwa tayari kurudia rudia kufanya bila kuchoka ili uweze kuyapata mafanikio unayoyataka.
Kadiri unavyojua hili, kulielewa na kulisimamia, ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi kubwa ya kufanikiwa.
Mpango mzima ni kurudia rudia kufanya mambo yote muhimu kwa mafanikio yako bila kuchoka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nitaendelea kurudia kufanya mambo yote yaliyo chanya Ili kupata matokeo tofauti.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ugumu wa mafanikio haupo kwenye kufanya upo kwenye kurudia rudia kufanya.Asante kocha
LikeLike
Watu huwa wanachoka haraka sana, na kupishana na mafanikio yao.
LikeLike
Ili niweze kupata mafanikio ninayoyataka kwenye maisha napaswa kurudia kufanya yale yaliyo sahihi bila kuchoka na bila kuacha.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kufanikiwa kwa mtu haiji kwa kufanya kwa siku moja ni kwa kurudia rudi na kuna mambo 3 ya muhimu hapa
1.jua kwa uhakika unachotaka
2.fanya kwa kufuata mchakato bila kuacha
3.jua kwa uhakika hatua unazopaswa kufuata
Kwa kanuni hiyo utapata matokeo
LikeLike
Ni kanuni ya uhakika.
LikeLike
Najua ninachotaka
Najua mchakato wa kufanya ili kupata ninachotaka
Naamua kurudia kwa msimamo ili kupata ninachotaka
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kweli tunapaswa kukaa kwenye mchakato kwa kuchukua hatua na kujirudiarudia bila kukata tamaa matokeo yatapatikana Asante
LikeLike
Hakika
LikeLike
Mpango mzima wa mafanikio ni kufanya kitu kwa kurudia mara nyingi zaidi bila kuchoka.
LikeLike
Kuchoka ni kuyakataa mafanikio.
LikeLike
Kweli kocha ushindi uko kwenye msimamo wa kufanya kwa kujirudia rudia
Asante Sana kocha
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Kurudia rudia ndio mpango mzima kwenye maisha
Asante
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kitu pekee ambacho nitafanyw kwa kurudia rudia ni kuweka Akiba
LikeLike
Kaa humo kwa msimamo.
LikeLike
Hakuna mafanikio yanayotokana na kufanya kitu mara moja tu.
Sala tunazosali na maandiko ya kiimani ni yale yale kila siku lakini tunayarudia Kila siku.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Umesema vyema kwenye sala, tunazirudua rudia bila kuchoka.
Hivyo ndivyo mafanikio pia yalivyo.
LikeLike
Nitarudia rudia kuhakikisha nafikia lengo langu
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Kurudia rudia ndiyo msingi Wa kufanikiwa…nitarudi rudia kukaa kwenye mchakato Hadi nipate matokeo
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitajitahidi kurudia mchakato wa BM kila siku bila kuacha mpaka nipate mafanikio.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Najua ninachokitafuta, nitafajya kwakurudia rudia mpaka nitakapofanikiwa
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Ili uweze kurudia rudia kitu mara kwa mara lazima ukipende na kukikubali sana.
Lazima kiwe ndiyo kipaumbele cha kwanza kwako, kama ilivyo pumzi.
Lazima uwe tayari kufanya bila kuhesabu umefanya mara ngapi.
Ni lazima uzame kwenye kitu na kitu hicho kiwe sehemu ya maisha yako ndiyo utaweza kukirudia rudia bila kuchoka.
Nimekuelewa vizuri sana Kocha.
Ahsante sana.
LikeLike
Ukishaanza kuhesabu tu, umeshapotea.
LikeLike
Mafanikio yapo katika kurudia rudi a bila kuchoka, kwa asili mambo makubwa huja kwa kurudia rudia, nitajikumbusha kila mara ya kwamba ushindi wangu Upo katika kurudia rudia yale ya msingi.
LikeLike
Ushindi upo kwenye kurudia rudia.
LikeLike
Ushindi katika Jambo lolote ktk Maisha hauanzii kwenye
Matokeo unayopata, Bali unaanzia kwenye msimamo wako unaokuwa nao kwenye kurudia rudia kwa muda
Mlefu bila kuchoka.
HAYO NI MANENO 24 TU.
yamebeba ujumbe mzito ambao ukiuishi utapata Mara zote matokeo yenye tija . Asante Sana.
LikeLike
Hakika, tukae humo.
LikeLike
Nitafuata mchakato kwa kurudia rudia kila mara bila ya kuchoka
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Narudia rudia kufanya kwa mchakato sahihi bila kuchoka
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mpango mzima ni kurudia,rudia,bila kuchoka nitajitahidi kufanya hivyo mara nyingi.
LikeLike
Usichoke.
LikeLike
Nakuwa tayari kurudiarudia kufanya bika kuchoka.
LikeLike
Safi.
LikeLike
Ushindi kwenye jambo lolote lile unaanzia kwenye msimamo unaokuwa nao kwenye kurudia rudia rudia kwa muda mrefu bila kuacha.
Asante
LikeLike
Tusichoke kurudia.
LikeLike