3041; Kazi yako kuu.
Rafiki yangu mpendwa,
Ni rahisi na watu wanapenda sana kujipa vyeo vikubwa kwenye biashara zao.
Kuna wanaojiita waanzilishi, wengine wamilili na wengine wakurugenzi wakuu wa biashara zao.
Vyeo hivyo vinaweza kuwa sahihi na vinavyomfanya mtu ajisikie sana vizuri, lakini ni vyeo ambavyo vinaweza visiwe na wajibu wa kutekeleza moja kwa moja kwenye biashara.
Mara nyingi hivyo ni vyeo vya heshima, ambavyo haviambatani moja kwa moja na majukumu ya kutekeleza kila siku kwenye biashara.
Ili biashara yako ifanikiwe, hasa kwenye hatua za mwanzo, ni muhimu uwe na cheo chenye majukumu ya moja kwa moja.
Cheo hicho muhimu unachopaswa kuwa nacho kwenye biashara yako ni kuuza. Bila ya kujali udogo au ukubwa wa biashara yako, wewe ndiye muuzaji namba moja kwenye biashara yako.
Tofauti yako wewe kwenye mauzo na timu yako ya mauzo ni upanda wa cheo husika.
Wakati timu yako ya mauzo ikikazana kuuza bidhaa au huruma zilizopo, wewe kama muuzaji mkuu, unauza zaidi ya hivyo.
Kwanza kabisa unawajibika kuiuza biashara yako kwa timu yako. Wafanyakazi wote unaowaajiri kwenye biashara yako, unapaswa kuhakikisha wanayaelewa maono ya biashara hiyo na kuyageuza kuwa sehemu ya maono yao binafsi.
Mafanikio yako ya kibiashara yanategemea sana jinsi timu yako inavyoikubali biashara na kujitoa kwao.
Hilo halitatokea kwa bahati, bali ni matokeo yanayotokana na mauzo endelevu unayoyafanya kwa timu yako.
Mbili unawajibika kuiuza biashara yako kwa wadau wengine mbalimbali. Hapa ni washirika ulionao kwenye biashara, wawekezaji ulionao au unaowawinda kuwapata na pia umma wote. Kadiri biashara inavyokuwa na sifa nzuri sokoni, ndivyo inavyowavutia watu wengi zaidi.
Hili pia ni matokeo ya kuweka kazi kubwa kwenye mauzo.
Tatu ni unawajibika kuiuza biashara yako kwa wateja wa biashara hiyo. Hapa siyo tu unauza sifa za biashara kwa wateja hao, bali unauza moja kwa moja bidhaa na huduma zilizopo kwenye biashara yako.
Ili kujitofautisha na timu yako ya mauzo, wewe utachagua kukazana kuwauzia wateja wachache wakubwa zaidi kwenye biashara yako.
Wateja hao wakubwa huwa inachukua muda kuwashawishi kununua, lakini pia wanawaheshimu sana waanzilishi wa biashara wanaojituma kila wakati.
Wafanyabiashara wengi wakishakuwa na timu huwa wanaona mauzo siyo wajibu wao mkubwa, hivyo kuacha kila kitu kwa timu.
Huwa wanakuja kushtuka biashara ikiwa imeshapata uharibifu mkubwa na mauzo yake kuathirika sana.
Wakati mwingine timu yako yako ya mauzo inaweza kukudanganya baadhi ya mambo, kama na wewe utakuwa muuzaji huwezi kudanganyika kirahisi.
Kaa kwenye mchakato kamili wa mauzo kwenye biashara yako na utaweza kuyaelewa mauzo na kuisukuma timu yako kufanya makubwa zaidi.
Bado utakuwa ni mwanzilishi, mmiliki na mkurugenzi mkuu wa biashara yako, lakini vyeo hivyo vinakuwa ni vya muda mfupi.
Wajibu wako mkuu na wa muda wote kwenye biashara ni mauzo, wewe ni muuzaji mkuu kwanza halafu mengine ndiyo yanafuata.
Wafanyabiashara wote wakubwa na walioweza kujenga biashara kubwa na zenye mafanikio ndivyo wamekuwa wanazichukulia biashara zao na kupambana sana kwenye kuziuza.
Kubali wewe ni muuzaji mkuu kwenye biashara yako.
Jijenge kuwa muuzaji bora kabisa kuwahi kutokea.
Hili litapelekea uweze kujenga biashara yenye mafanikio makubwa.
Kila mahali unapokuwa na kila kitu unachokuwa unafanya, kumbuka unakuwa unaiuza biashara yako. Hakikisha unakamilisha hilo kwa mafanikio makubwa sana.
Hustahili kuvaa vyeo vingine kwenye biashara yako kama cheo cha msingi kabisa ambacho ni MAUZO kinakushinda.
Uzuri ni huna haja ya kuhofia hilo, kwani tayari mchakato upo, ni wewe tu kuweza kuufuata kwa msimamo ili kupata matokeo bora.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Mimi ni muuzaji mkuu wa biashara yangu.Nitakaa kwenye mchakato wa mauzo hasa kwa wateja wote wakubwa wa biashara,timu na wadau wengine wa biashara.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Mimi kama mmliki wa biashara cheo changu ni kuhakikisha nakua muuzaji bora kuwahi kutokea ili niweze kuwaongoza na kuwasimamia wasaidizi wangu vizuri mana nitakua naelewa kwa uhakika kabisa kile ninachokisimamia kwa matendo na si kwa maneno tu.
Asante kocha.
LikeLike
Mimi ni muuzaji namba moja kwenye biashara yangu,
kuqnzia kusaka, kuhudumia na kukamilisha wateja wa biashara yangu,,, nitakuwa mfano kwa timu yangu.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante kocha,Inabidi niwemuuzaji bora kuwahi kutokea na namba moja kwenye biashara yangu.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Mimi ni muuzaji mkuu wa TLG kwa wafanyakazi, wadau na wateja
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Napaswa kuwa muuzaji mkuu kwenye biashara yangu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ili biashara ifanikiwe hasa siku za mwanzo inabidi uwe na cheo chenye majukumu ya Moja Kwa moja
Asante
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Cheo cha KWANZA cha kila mwenye biashara ni kuwa muuzaji mkuu.
Mimi ni muuzaji Mkuu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
mimi ni muuzaji bora kuwahi kutokea,
rejea kauli 10 chanya za kujiambai kila siku hapo ndo kuna vyeo vyako vyote vya msingi kabisa.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Pamoja na vyeo vingine nilivyonavyo, mimi nitabaki kuwa Muuzaji mkuu wa biashara yangu. Asante kocha kwa makala hii.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Cheo chenye maana kwenye biashara ni kuwa muuzaji bora wa kile unachouza kwa wengine na hasa wale wenzako wakubwa
LikeLike
Kweli.
LikeLike
Wakati mwingine timu yako yako ya mauzo inaweza kukudanganya baadhi ya mambo, kama na wewe utakuwa muuzaji huwezi kudanganyika kirahisi.
Kaa kwenye mchakato kamili wa mauzo kwenye biashara yako na utaweza kuyaelewa mauzo na kuisukuma timu yako kufanya makubwa zaidi.
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike
Mimi ndio napaswa kuwa muuzaji namba moja kwenye biashara yangu.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante sana kocha ni hakika
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Asante sana kocha ni hakika. Shukrani nyingi kwako
LikeLike
Kazi yangu kubwa ni kuuza,kazi yangu kubwa ni kuhakikisha naiuza biashara yangu, napenda kwa maarifa tunayopata kwenye kisima cha maarifa naimani nitafanikiwa
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Vyeo vingine ni ziada tuu, cheo changu kikubwa ni kuuza , kuwauzia wateja wakubwa Wa biashara,kuiuzia timu yangu maono makubwa ya biashara na kuuza bidhaa na huduma Kwa wateja wetu…
LikeLike
Uza. U.Z.A.
LikeLike
Mimi ndio muuzaji namba moja kwenye biashara yangu.
Nawajibika kuiuza biashara yangu kwa timu yangu, kwa wadau wengine mbali mbali na kwa wateja wa biashara yangu
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike