3046; Wapambanie kombe.
Rafiki yangu mpendwa,
Kadiri chochote kile unachofanya kinavyokuwa rahisi kupatikana, ndivyo wengine wanavyokidharau na kukipuuza.
Kama muda wako unapatikana kwa urahisi, watu watautumia hovyo kwa mambo yasiyokuwa na tija.
Watakuzamisha kwenye mambo ya hovyo, yanayokula muda wako na yasiyokuwa na tija yoyote kwenye yale unayofanya au unayotaka kufikia.
Kadhalika kadiri chochote unachouza kinavyokuwa rahisi kupatikana, yaani wateja unaowalenga wanaweza kukipata kwa wengine wengi na kwa urahisi, ndivyo wasivyokithamini kitu hicho.
Kwa kuwa wanajua wanaweza kukipata kwa wingi na urahisi muda wowote, hawasukumwi kwenda hatua ya ziada ili kukipata.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwa watu unaoshirikiana nao, hasa wafanyakazi unaowaajiri. Kadiri majukumu unayowapa yanavyokuwa rahisi, ndivyo wanavyoyafanya kwa mazoea na matokeo wanayozalishwa kuwa hafifu sana. Lakini majukumu unayowapa yanapokuwa yanawapa changamoto, ndivyo wanavyosukumwa kuwa bora na kuyafanya kwa viwango vya juu.
Kwa watu wote wanaohusika na wewe kwa namna yoyote ile, waweke kwenye hali ya kupambania kombe. Fanya kile wanachofanya kiwe na ugumu fulani ambao utawasukuma kwenda hatua ya ziada ili kuweza kukikamilisha kwa ubora wa hali ya juu.
Mara zote waweke watu kwenye hofu ya kupoteza kile wanachopata kwako, hilo linawafanya wakithamini na kukipambania.
Tamaa ya kupata pia ni njia yenye nguvu ya kuwasukuma watu kupambania kombe, lakini peke yake haina nguvu kama hofu ya kupoteza.
Msingi mkuu wa uchumi ni kanuni ya mahitaji (demand) na upatikanaji (supply). Kitu kinapokuwa na mahitaji makubwa na upatikanaji wake kuwa mdogo ndivyo kinavyokuwa na thamani kubwa zaidi.
Hii pia tunaweza kuichukua kama moja ya kanuni kuu za maisha.
Cheza vizuri karata zako za kuhitajika kwa kile unachotoa (demand) na upatikanaji wake (supply).
Hakikisha kwa namna yoyote ile, uhitaji ni mkubwa kuliko upatikanaji ulivyo.
Hilo linatosha kukuza sana thamani ya chochote ulichonacho na kujiweka kwenye nafasi ya kupata matokeo bora zaidi.
Hii dhana tuliyojifunza hapa inahitaji umakini na ujasiri wa hali ya juu katika kutekeleza.
Wengi huona kurahisisha mambo na kutoa kwa wingi ndiyo itawapa uhakika wa kuwapata wanaowalenga.
Ni kweli kwa kutokuweka vikwazo vyovyote utawapata walio wengi, lakini pia wengi wa hao utakaokuwa umewapata, hawatakuwa watu sahihi kwako.
Unapochukua hatua kwenye dhana hii ya kuwafanya watu wapambanie kombe, utaona kama unapoteza, hasa mwanzoni. Na hilo ni kweli kwa sababu kuna wengi ambao siyo sahihi ulikuwa nao.
Ni lazima uwaondoe hao kwanza ili kupata bafasi ya wale walio sahihi na bora.
Kwenye huu msimu wa HAPANA ambao tupo, sema hapana kwa yote yaliyo chini ya viwango unavyokuwa umejiwekea.
Usihofie kukosa unachotaka kupata, changa vizuri karata zako za mahitaji na upatikanaji ili kuwapa watu msukumo wa kuweka juhudi ili wapate yale unayoyatoa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nitasema hapana yale yotenyakiyochini ya viwango
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Unapatikana wa kitu unapokuwa adimu ndivyo thamani yake inavyokuwa kubwa
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Tamaa ya kupata ni njia kuu ya watu kupambania Kombe
LikeLike
Kabisa, tuwape kitu cha kupambania kupata.
LikeLike
Lazima kuwa tayari muda wote kama unapambania kombe
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante kocha,nitaweka juhudi na nguvu kubwa kwa kusema hapana mara zote.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asili ya binadamu ni ushindani, HIVYO unapokuwa unawapa watu kitu wakipambanie ndiyo wanakua na msukumo mkubwa wa kujituma kupata kile wanachotaka.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hapana kwa yote Yaliyo chini ya viwango vyangu nilivyojiwekea
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kwenye huu msimu wa HAPANA ambao tupo, sema hapana kwa yote yaliyo chini ya viwango unavyokuwa umejiwekea.
Asante sana
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Viwango vya juu vinahusika
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kuanzia sasa Nitasema hapana kwa yote yaliyo chini ya viwango ninavyokuwa nimejiwekea.🙏🙏
LikeLike
Simamia hilo.
LikeLike
Nitachanga vizuri karata zangu ili demand ili kubwa kuliko supply
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kusema hapana kwa yote yaliyo chini ya viwango nilivyojiwekea.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kusema Hapana kwa wote waliochini ya Viwango na kuwapa ushindani wapambanie Kombe wanaoweza.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kitu nilichojifunza kwenye Makala ya leo ni,
Kama Ukiwaweka watu kwenye hofu ya kupoteza kile wanachopata watakiona kitu hicho kuwa cha thamani kwao na kukipambania.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitaendelea kusema HAPANA kwa yote yaliyochini ya viwango nilivyojiwekea.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nimekumbuka nilipokuwa Arusha nafanya filed mdada Mmoja alikuwa anapenda sana kutumia hili neno. Tunapambania kombe
Nitaendelea kupandisha viwango vyangu. Na wore ninaojihusisha nitahakikisha wanafanya KAZI Kwa viwango
LikeLike
Lazima wapambanie kombe.
LikeLike
Mara zote waweke watu kwenye hofu ya kupoteza kile wanachopata kwako, hilo linawafanya wakithamini na kukipambania.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Mara zote naweka viwango vya juu na kuhakikisha wote ninaojihusisha nao wanafanya kwa viwango au juu ya viwango.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Naongeza thamani ili kuongeza hofu ya kupoteza Kwa kila ninaejihusisha nae.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Adimu ni kitu cha heshima sana,mazoea huzaa dharau na kuooteza thaman
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ukitoa thamni kubwa utapata wenye kuipna hiyo thamini na watakulipa ghali na kuwa adimu ndiyo thamani yako pia inakua kubwa
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kuyapata mambo kwangu itakuwa si jambo rahisi maana rahisi haina thamani au ina thamani ndogo sana.
LikeLike
Hakika.
LikeLike