3050; Wateke.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye malengo makubwa matatu tunayoyafanyia kazi kwenye kujenga biashara, yaani MFUMO, TIMU na WATEJA, lengo la TIMU ndiyo limekuwa gumu zaidi.
Kila ambaye ameshachukua hatua kwenye kujenga timu, amekutana na changamoto nyingi sana.
Changamoto ya kwanza ni kukosekana kwa watu sahihi ambao wanaweza kutekeleza majukumu yaliyopo.
Changamoto ya pili ni uzembe, uvivu na kutokupenda kujifunza kwa wale wachache wanaoonyesha dalili za kuweza kuwa sehemu ya timu.
Na changamoto ya tatu ni kutokukaa kwao kwa muda mrefu kwenye kazi pale wanapopewa nafasi.
Changamoto ya kwanza na ya pili hatutazizungumzia hapa, kwa hakika hatuhitaji hata kuzizungumzia, kwa sababu kama mtu hawezi kazi, ni mzembe, mvivu na hapendi kujifunza, huyo hapaswi hata kupewa nafasi.
Kama atapewa nafasi kwa sababu hakuna sahihi wanaopatikana kwa wakati huo na uhitaji upo, iwe ni kwa kushikiza tu, wasiwekewe matumaini makubwa.
Najua unaweza kuwa na matumaini kwamba mtu atabadilika, lakini usijiweke kwenye kuvunjika moyo.
Sasa tuje kwenye changamoto ya wale sahihi wanaopatikana kutokukaa kwenye nafasi zao kwa muda mrefu.
Hawa ni wale ambao angalau wana afadhali, wanaweza wasiwe kamilifu kama wanavyohitajika, lakini angalau wanajituma na wapo tayari kujifunza.
Lakini sasa, wakati wewe unategemea uwajenge kwa ajili ya muda mrefu, unakuja kugundua nao wanatafuta mahali pengine pazuri pa kwenda.
Hili ni jambo linaloumiza sana, wewe umeweka imani kwa mtu na umejitoa kumwendeleza ili awe bora na kufanya vizuri. Lakini yeye anakuwa anatafuta mahali pengine pazuri zaidi.
Hilo linaweza kukufanya uwaone ni wasaliti, ambao hawajajitoa kweli kwenye majukumu unayowapa.
Unaweza kutaka kuwaondoa kwenye kazi kwa sababu unaona hawawezi kudumu.
Lakini nataka nikuambie hupaswi kutaharuki kwa sababu ya hilo.
Kama mfanyakazi uliyekuwa unamtegemea umegundua anatafuta kazi mahali pengine, furahi.
Furahi kwa sababu anaamini anaweza kufanya zaidi ya majukumu ambayo umempa.
Angekuwa haamini anaweza zaidi, asingefikiria kingine nje ya kazi uliyompa.
Jambo jingine kubwa kabisa ni kuwa tu mkweli kwako.
Kama wewe ndiyo ungekuwa umeajiriwa kwa mtu mwenye biashara kama yako, anayeiendesha jinsi unavyoendesha biashara yako, ungekuwa tayari kuweka matumaini yako hapo kwa miaka 30 ijayo?
Yaani mtu anaendesha biashara bila ya mfumo wowote, maamuzi yote yanatoka kwenye kichwa chake, tena kwa kuchochewa na hisia na hakuna mpango wowote wa ukuaji unaofanyiwa kazi.
Je ungekaa kwa kujiamini kabisa kwamba hapo ndiyo umefika mwisho wa maisha yako?
Kama utakuwa mkweli, jibu ni hapana.
Na hapo sasa ndiyo nataka nikupe mpango ambao utakusaidia kuwabakisha wafanyakazi wazuri kwenye biashara yako kwa muda mrefu.
Mpango huo ni kuwateka.
Ninaposema uwateke simaanishi uwakamate na kuwafungia kwa nguvu kwenye biashara yako.
Badala yake uwawekee mtego ambao utawanasa na wasiwe tayari kuondoka hata pale wanapopata nafasi mahali pengine.
Njia ya uhakika ya kuwateka binadamu, ni kuwapa uhakika. Hakuna kitu ambacho watu wanakipenda kama uhakika.
Ndiyo maana watu huwa tayari kukaa kwenye kazi inayowalipa mshahara kidogo kuliko kwenda kufanya biashara yenye fursa ya kuwaingizia kipato kikubwa.
Mshahara, japo ni mdogo unakuwa wa uhakika kila mwezi, tofauti na faida ya biashara isiyokuwa ya uhakika.
Ili kuwateka wafanyakazi na kuweza kujenga timu imara ya kukuza biashara, wape uhakika kwenye maeneo haya matano.
1. Mshahara
Mshahara huwa ndiyo kitu cha kwanza kwa wengi kuangalia.
Na huu siyo lazima uwe mkubwa sana, lakini muhimu ni uwepo uhakika wa kuupata mshahara huo.
Kiasi chochote kile ambacho mmekubaliana, wape uhakika kwa kuwalipa mara zote kama mlivyokubaliana.
Walipe kwa ukamilifu na kwa wakati.
Hilo litawajengea utegemezi fulani.
Nasim Taleb amewahi kusema kuna vitu vitatu ambavyo vina uraibu mkali sana, ambavyo ni sukari, madawa ya kulevya na mshahara wa kila mwezi.
Watu wakishauzoea wanakuwa na uraibu nao na kutokutaka kuukosa.
2. Ndoto kubwa
Watu wengi hawana ndoto zozote kubwa kwenye maisha yao, wala hawaamini wanaweza kufanya makubwa.
Hivyo wanapopata mtu mwenye ndoto kubwa na ambazo zina matumaini ya kufikiwa, wanakuwa tayari kuambatana naye.
Ni muhimu kuwapa watu uhakika kwenye ndoto kubwa kwa kuzungumzia ndoto hiyo kila mara na kuwa na mkakati wa jinsi ya kuifikia.
Wafanye watu waone wana mchango mkubwa kwenye kufikia ndoto hiyo na watakuwa tayari kujitoa sana.
3. Mfumo
Hakuna kitu ambacho kinawavuruga watu kama kukosekana kwa utaratibu wa jinsi mambo yanavyopaswa kufanyika.
Hilo linawafanya washindwe kujua kama wanafanya kwa usahihi au la, kitu kinachowanyima kujiamini.
Uwepo wa mfumo unawapa watu uhakika wa jinsi mambo yanavyopaswa kufanyika.
4. Misingi
Ni muhimu sana kuwepo na misingi ambayo inasimamiwa kwenye biashara. Misingi hiyo ndiyo inayokuwa inawaongoza watu wote kwenye biashara na hakuna mtu yeyote anayekuwa juu ya misingi hiyo.
Hilo linawapa watu uhakika wa mambo kufanyika kwa usahihi na siyo kwa mihemko.
Misingi inapofuatwa, changamoto nyingi hukwepeka.
5. Jamii
Sisi binadamu ni viumbe wa kijamii na hivyo huwa tunapenda sana kuwa ndani ya kundi fulani.
Kwa kujenga jamii bora ya wale wanaofanya kazi kwenye biashara yako, kunawavutia watu kupenda kubaki ndani ya jamii hiyo.
Hilo linawafanya watu kuwa tayari kubaki kwa muda mrefu kwa sababu wanapenda kuwa ndani ya jamii husika.
Maeneo hayo matano yana nguvu ya kuwajengea wafanyakazi uhakika ambao unawafanya wakae kwenye biashara kwa muda mrefu.
Kazana kuyajenga mambo hayo kwa msimamo kwenye biashara yako ili uweze kujenga timu bora.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Wape watu uhakika.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ni kweli watu watakuwa tayari kukaa mahali ambapo wana maslahi ya uhakika,wanaiona ndoto kubwa,kuna mifumo mizuri,misingi inayosimamiwa na si maamuzi ya mtu kulala na kuamka lakini pia watu wanajaliana kama jamii.Haya yanafanya kazi kwa taasisi kubwa lakini pia kwa kwa biashara zetu ndogo.
LikeLike
Kabisa, tuyazingatie.
LikeLike
Huu ni ukweli mchungu kumeza. Inahitaji sana kujitoa na kuwa mkweli katika Kila hatua. Nimegundua bado ni mchanga sana kwenye eneo la kujenga mfumo na kushirikisha malengo makubwa niliyonayo Kwa watendaji yaani, wasakaji, wakamilishaji na wahudumiaji. Nitafanyia kazi hatua Kwa hatua.
Asante sana kocha Dr. Amani. Kweli umedhamiria kubadilisha maisha yetu tena kwa nidhamu kubwa sana.
LikeLike
Iko vizuri. Mimi nita ifanyia kazi
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ahsante sana kocha, nitawateka kwakuyazingatia maeneo hayo matano
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kwa kila mwenye maono ya kufika mbali, lazima ayazingatie haya mambo MATANO HAPA.
Hongera sana Kocha Dr Makirita Amani kwa kazi nzuri unayoendelea kuifanya.
LikeLike
Asante sana
LikeLike
Ninawapa wasaidizi wangu uhakika kwa kugusa maslahi yao ili wao waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kuiwezesha biashara kufikia malengo yake makubwa.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Wape watu uhakika ili uendelee kubaki nao kwa muda mrefu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Wape watu uhakika wa kile uchohaidi
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitawapa uhakika watu ili nikae nao kwa muda mrefu mpaka kufikia ndoto kubwa
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kuna vitu vitatu ambavyo vina Leta uraibu mkali sana vitu hivyo ni sukari, madawa ya kulevya na mshahara wa kila mwezi.
LikeLike
Uraibu ni mbaya.
LikeLike
Nitahakikisha nakamilisha uraibu wao. Mahabharata kwa wakati
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Sitaacha kuzitaja ndoto zangu na kuonyesha njia bora?ya kuzifikia ndòto hizo
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante tutawajengea uhakika ili wasiwe na wasi wasi
Wapate uhakika wa mshahara na kuwa na ndoto kubwa
Asante
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kumbe ndiyo maana wengi wanakaa mahali muda mrefu ni uhakika misingi mfumo namambo mengine ya msingi
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Njia ya uhakika ya kuwateka binadamu ni kuwapa uhakika.
Nitawapa uhakika.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Uhakika Wa mshahara ni mbinu Bora ya kuwateka, napambana kukuza mauzo Ili kutoa uhakika Wa mshahara kwa wakati , najenga mfumo imara kuepusha makosa mengi na kuwapa wafanyakazi kujiamini
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha,nitahakikisha nawateka wafanyakazi wangu kwenye maeneo haya matano;
1-Mshahara,uraibu huu huwa unawalevya sana,wanasema aheri mkate mwembamba mrefu,kuliko mnene mfupi.
2-Ndoto kubwa.
3-Mfumo.
4-Misingi na
5-Jamii.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nitahakikisha najari maslahi yao,ili niweze kuwateka,lakini pia wakiondoka nitachukukia ni sehemu ya wao nao kupambana.asante
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante kocha,nitajitahidi kujenga mambo yangu kwa msimamo ili na timu yangu iwe na uhakika wa kazi.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nini chakufanya ili wafanyakazi wakae muda mrefu bila ya kuondoka
LikeLike
Wape uhakika.
LikeLike
Ni kweli. Wanahitaji uhakika.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Uhakika ndiyo Kila kitu kwenye kuwateka wafanyakazi waweze kusalia kwenye biashara. Mtu akifahamu kwamba ana uhakika wa kupata mahitaji yake ya msingi ni rahisi sana kusalia kwenye biashara.
LikeLike
Hakik.
LikeLike
Hakika. Kuwepo kwa mfumo ni suluhisho la changamoto nyingi za kibiashara
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
ASANTEE KOCH A nitahakikisha mtumishi wangu anapata uhakika wa mambo haya mshara wake kwa wakati na uaminifu,kumshirikisha ndoto yangu kubwa NILIYONAYO,KUMWONesha mifumo ya uendeshwaji wa biashara hiyo,jAMII KWA KUSHIRIKIANA NAE KATIKA MAMBO YAKE KWA UPENDO
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ni ukweli kabisa usiyo pingika kuwapa watu mshashahara
kwa wakati kunafanya waweze kuona mtaani kulivyo na changamoto nyingi hivyo wanaona Bora wakae.
LikeLike
Kabisa, mshahara hata ukiwa mdogo, kiasi cha kupatikana kwa uhakika kinateka sana.
LikeLike
Watu wengi hawana ndoto kubwa wakipata uhakika wa mshahara wako tayari kuhudumu Kwa muda mrefu.
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike
-Mshahara
-Ndoto kubwa
-Mfumo
-Misingi
-Jamii
LikeLike
Muhimu kuyajengea uhakika.
LikeLike
nitajenga timu na kufuata misingi hio mitano ili niweze kukaa na wafanyakazi wamgu
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Njia ya uhakika ya kuwateka binadamu, ni kuwapa uhakika. Hakuna kitu ambacho watu wanakipenda kama uhakika.
Ahsante Kocha.
Nimekuelewa vizuri sana.
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Nilipomaliza kusoma hii makala (Uzi mkali sana) nilijilaumu kwanini sikuisoma mapema 😥
.
Lakini nakushukuru sana kocha Dr makirita Amani kwa sababu naenda kuandaa haya mambo matano kabla sijaanza safari yangu mpya ya kuajili. Na nitashirikisha kwako.
Ahsante sana🤝🤝
#NidhamUpendo.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante sana kocha hii imekaa vizuri nitawapa wasaidizi wangu mshahara ili wawe na uhakika wa mshahara kila mwezi na hii nikweli kwasababu msaidizi wangu msakaji akipiga ma simu akiona hapate oda yoyote huwa anaishia kukataa kwenda sambaza nakubaki nyumbani kwake kwasababu namulipa kwa commission pia kwasababu anajua asipouza hatapata hela kwa hiyo nitamuwekea uhakika wa mshahara
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mara zote nina wapa uhakika wafanya kazi wangu kwa kuwapa mishahara kwa wakati pia kuwapa zawadi kwa wale wanao fanya vizuri ktk kuketa matokeo kupitia kukaa ktk mchakato sahihi wa mauzo. Nina wateka kijichi kwa njia hiyo. Asante sana Kocha
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Mshahara wa uhakika na kwa wakati.
Ndoto kubwa.
Mfumo.
Misingi.
Jamii.
LikeLike
Tuzingatie haya.
LikeLike
Nikweli kocha maono makubwa yanawapa matumaini wasaidizi wetu hivyo kwenye vipindi vyetu vya asubuhi na timu yangu nitakuwa na na anza Kwa kuwakumbusha maono ya biashara inapotakiwa kufikia Kwa mda Gani tuwe tumefikia maono hayo
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Asante sana Kocha nitahakikisha nawapa watu uhakika kwenye ndoto zao.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kwa hakika mambo hayo yote matano ninakwenda Kuya zingatia ili kujenga timu ambayo nitakuwepo kwenye biashara kwa muda mrefu kwa kuhakikisha wafanyakazi wanapata mshahara kwa uhakika, Wanakuwa na Matumaini ya muendelezo wa biashara kutokana na maono na mipango mikubwa iliyopo kwenye biashara, uwepo wa mfumo kama itaratabiu wa utekelezaji wa majukumu mbalimbali, uwepo wa sheria na Miongozo kama misingi ya kufanya maamuzi na jamii thabiti iliyojengeka ambayo ipo tayari Kusaidiana na kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante Kocha kwa makala hii. Nitakwenda kuzingatia nguzo hizo tano za kuhakikisha nawateka wafanyakazi wangu.
Ndoto ya taasisi ilikuwa wazi kabisa waambatane nayo.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitaiishi misingi ifuatayo kuhakikisha nateka timu yangu
1.Mishahara ya uhakika
2.Ndoto kubwa
3.Mfumo
4.Jamii
5. Misingi
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante sana Kocha.
Hivi vitu vitano nitahakikisha navitoa Kwa wafanyakazi
LikeLike
Mshahara unateka upesi sana sana,tumia hii kuweza kuwateka kutimiza mambo yako.Lakini usikubali wewe kutumiwa na mshahara kufukia ndoto zako kubwa.Kuna mengi makubwa usipoweka umakini watakutwka kupitia mshahara.
Ahsante kocha
LikeLike
Huu ni ukweli mchungu kumeza. Inahitaji sana kujitoa na kuwa mkweli katika Kila hatua. Nimegundua bado ni mchanga sana kwenye eneo la kujenga mfumo na kushirikisha malengo makubwa niliyonayo Kwa watendaji yaani, wasakaji, wakamilishaji na wahudumiaji. Nitafanyia kazi hatua Kwa hatua.
Asante sana kocha Dr. Amani. Kweli umedhamiria kubadilisha maisha yetu tena kwa nidhamu kubwa sana.
LikeLike
Nikweli kabisa ukiwapa mshahara wao kwa wakati na ukawaelekeza kufuata taratibu hawawezi kuwa na wasiwasi
LikeLike
Mimi nimejiangalia mwenyewe na kwa haki bila upendel
eleo ninakili viwango vyangu vya kujenga MIFUMO imara na pia usimamizi imara Bado viko chini ya viwango
Hivyo ninapaswa kuongeza speed ya kujifunza endelevu
Kwa msimamo na kuyaweka ktk vitendo yote ninayotifu
nza ili kuweza kuwateka watu wavutiwe kufanya kazi na Mimi. Asante Sana kocha kwa Somo Bora kabisa .
LikeLike
Asante Kocha kwa makala hii! Hii siyo makala tu, bali ni mwongozo muhimu sana kwa sisi tunaojenga timu. Uhakika wa mshahara, ndoto kubwa, mfumo, misingi na jamii. Ninakwenda kufanyia kazi kwenye biashara zangu.
LikeLike
Wape watu uhakika.
1. Mshahara
2.Ndoto kubwa.
3. Mfumo
4.Jamiii
5. Msingi
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Wape watu uhakika katika vitu vifuatavyo
1. Mshahara
2.Ndoto kubwa.
3. Mfumo
4.Jamiii
5. Msingi
Hakika hii makala ni Msingi mkuu
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Haya umeandika Dr Amani hapa ni ukweli mtu,mimi ni shahidi wa hili kwa asilimia zote,biashara yangu ina kila changamoto na wakati mwingine inakosa hata bidhaa muhimu lakini kamwe na haitokuja kutokea ikafika tarehe ya kulipa mshahara nisilipe mshahara,kamwe sijawahi kuwauliza ndoto zao na kuwaambia namna gani biashara yangu ni mwanzo mzuri wa kuzifikia ndoto zao,kubwa zaidi jua liwake na mvua inyeshe haijawahi pita siku hesabu ya siku usika isifungwe na hilo limenifanya niwe na changamoto zingine lakini za wafanyakazi siyo sana. Asante sana kwa makala hii nzuri.
LikeLike
Asante sana Kelvin kwa kushirikisha ushuhuda wa jinsi umekuwa unatekeleza haya.
Endelea hivyo kwa msimamo, utakuja kujenga Business Empire kubwa sana kuwahi kutokea.
Kwa namna unavyopambana kibiashara licha ya magumu unayopitia, utakuja kufanya makubwa sana.
Kila la kheri.
LikeLike
Kumbe kama mimi mmiliki wa biashara nikawa sina ndoto kubwa na vijana wa kazi wakagundua kuwa biashara haina ndoto kubwa,, wanajiona hawapo mahali sahihi,?? Aisee ninahitaji sasa kuwashirikisha ndoto yangu kubwa pale ninapowaajiri ili waone wanakuja kujenga majina makubwa kwa kuikuza biashara yangu na sio kuja kulipwa mshahara tu.
LikeLike
Wakigundua hamna unakoenda wanakuwa wamejishikiza tu, wakipata pengine watakukimbia haraka sana.
Waimbie ndoto zako kubwa kila siku bila kuchoka, inawajengea imani kubwa.
LikeLike
Nashukuru sana kocha kwa makala hii ya kipekee. Ni kweli mambo haya matano ni muhimu nanyana nguvu, japo huenda ikawa sio rahisi kwenda nayi yote kwa pamoja. Kidogo kidogo ndio mwendo.
Kwenye mshahara hata kama sio kiwango alichohitaji lkn mlikubaliana kiasi fulani basi angalau anafundishwa jinsi ya kupata cha ziada mfano bonus za mauzo au kuwa na bidhaa ya pekee ambayo anaitendea kazi kwa jitihada za ziada na kile cha ziada kinakuwa ni kipato chake.
Lakini pia kuna vitu ambavyo vinaashiria na kumpa picha kubwa na ndoto kubwa mbeleni bila hata kuambiwa.
Mfano unapomshauri msaidizi kuwa na akaunti ya benki na sio akaunti tu bali unapomfunza jinsi ya kujiwekea akiba bila kuitunia kwa matumizi ya kawaida, anapata picha kubwa ya baadae, au unapomtaka awe na picha kubwa ya maisha yake miaka kumi ijayo ili wewe uweze kufanya kile unachoweza kuifanikisha basi anakua na picha kubwa na ndoto kubwa ya kazi anayoifabya sasa
LikeLike
Vizuri sana kwa nyongeza hii ya namna bora ya kuyafanyia kazi haya.
LikeLike
Ntapambana kujenga haya Mambo matano kwenye biashara yng ili iweze kustawi na wafanyakazi kukaa muda mrefu pamoja.
Asante kocha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Watu kwenye maisha wanakuwa watiifu Kwa sabadi Wana uhakikika
Asante
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Nitahakikisha nawapa uhakika wafanyakazi sahihi nitakaowapata katika maeneo haya matano ili kuwafanya waendelee kuwa sehemu ya timu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
”Kiasi chochote kile ambacho mmekubaliana, wape uhakika kwa kuwalipa mara zote kama mlivyokubaliana”
Asante sana Kocha, hapa nitapazingatia Sana.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike