3052; Siyo unachotaka, bali unachotoa.
Rafiki yangu mpendwa,
Karibu kila mtu kwenye maisha anataka kupata mafanikio makubwa.
Lakini kwenye uhalisia ni watu wachache sana wanaopata mafanikio makubwa wanayoyataka.
Tafiti nyingi zimefanywa ili kujua nini kinawatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa.
Vitu vingi vya nje ambavyo wengi walidhani ndiyo vinawatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa, vimeonekana kutokuwa na mchango.
Mafanikio yameonekana kuwepo kwenye kila eneo na kwa kila aina ya watu.
Kwenye mazingira ya aina moja, kuna watu wanafanikiwa sana na kuna watu ambao wanashindwa.
Matokeo ya tafiti nyingi zilizofanywa kwenye eneo la mafanikio zinaonyesha tofauti za wanaofanikiwa na wanaoshindwa zinaanzia ndani ya mtu.
Maisha ni mwendelezo wa kutoa kafara.
Ili kupata kitu chochote kile unachotaka, lazima uwe tayari kutoa kitu fulani kinachohitajika sana.
Hivyo basi, inapokuja kwenye mafanikio, swali muhimu zaidi siyo nini unachotaka, bali nini upo tayari kutoa kafara ili kupata unachotaka.
Kujua unachotaka ni hatua ya kwanza, ambayo wengi wamekuwa wanaijua hatua hii, hata ambao hawafanikiwi.
Kujua kafara ya kutoa na kuwa tayari kuitoa kafara hiyo kwa jinsi inavyopaswa kutolewa ni hatua ya pili muhimu, ambayo wachache sana ndiyo wanaifanyia kazi.
Ni jambo la kushangaza sana jinsi ambavyo watu wengi wanavyotaka mafanikio kwenye maisha yao, lakini watu hao hao wakiwa hawapo tayari kubadilika.
Mafanikio pia huwa yanakuja kwa ngazi na awamu.
Mafanikio makubwa huwa hayaji yote kwa wakati mmoja, bali yanakuja hatua kwa hatua.
Yanakuja mafanikio kidogo kwanza, ukishaweza kuyakabili vizuri na kutoa zaidi kinachohitajika ndiyo unapanda ngazi kwenda kwenye mafanikio makubwa zaidi.
Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana baadhi ya watu huwa wanakwama kwenye hatua ndogo za mafanikio wanayokuwa wameyapata.
Yaani mafanikio kidogo ambayo mtu anakuwa ameyapata yanakuwa kikwazo kwake kupata mafanikio makubwa zaidi.
Kabla hujalaumu kukosa unachotaka, anza kwa kulaumu kushindwa kutoa kafara unazopadwa kutoa ili kupata unachotaka.
Kila kitu unachotaka, asili inaweza kukupa.
Lakini asili haitakupa tu kwa sababu unataka, bali itakupa kama utaionyesha kweli umedhamiria kukipata, kupitia kafara unazotoa.
Na ieleweke wazi kwamba ninaposema kafara hapa simaanishi kuwaumiza wengine kwa namna yoyote ile.
Bali namaanisha kutoa kitu ambacho kinakuumiza sana wewe binafsi.
Lazima uwe tayari kuachilia vile ulivyokamatia sana ndiyo uweze kufungua uwanja wa mafanikio.
Mafanikio yako makubwa unayoyataka yanapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza kabisa kwenye maisha yako.
Kama kuna kitu kingine chochote ambacho unakipa nafasi kuliko mafanikio unayoyataka, kitu hicho ndiyo kitakuwa kikwazo kikubwa sana kwako kuyapata mafanikio hayo.
Vikwazo vingi kwenye safari yako ya mafanikio vinaanzia ndani yako mwenyewe, kwenye vitu ambavyo tayari unavipenda sana.
Hivyo ndivyo unavyopaswa kuachana navyo ili ufungue milango ya mafanikio makubwa kwako.
Kwa lolote unalokwama kwenye maisha yako, jiulize ni kitu gani bado hujawa tayari kukiacha.
Ukijua na kuacha, mafanikio yatakuwa uhakika sana kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ni kitu gani ambacho bado sijawa tayari kukiacha.
LikeLike
Hapo ndipo penye mkwamo.
LikeLike
ahsante kocha, kweli mafanikio ni kupanda ngazi na ukipanda lift kama kupata bahati nasibu mara nyingi mafanikio hayo upotea haraka sana.
na kadri unavyoenda ngazi za juu ndio unapaswa kuongeza nidhamu. maana ukianguka unaumia kuliko aliyepo ngazi ya chini.
AHSANTE
LikeLike
Hakika, ukienda juu zaidi anguko pia linakuwa la kishindi kikubwa.
Nidhamu ni muhimu sana.
LikeLike
Kile ambacho nakipenda na nimekikumbatia ndio kikwazo kwangu kwa mafanikio.Lazima niwe tayari kukiachilia na kutoa kafara ili niweze kufanikiwa.
LikeLike
Hakika, unavyopenda vinakwamisha sana.
LikeLike
Asante sana
Kujua unachotaka.
Kafara
Hivi ni vitu viwili kwenye mafanikio yangu
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kafara ya kujitesa na kujiumiza Mimi binafsi hata kujinyima vitu ninavyovipenda sana ambavyo nimevishikilia na kuviacha imekuwa changamoto, Leo naamua kuviachilia Ili kupata mafanikio ninayoyataka
Asante Kocha
LikeLike
Lazima uwe tayari kuumia ili kupata unachotaka.
LikeLike
Nitayatoa kafara mambo yote ambayo hayana mchango kwenye safari yangu ya mafanikio ili kupata ninachokitaka
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitaviachiria vitu vyote nabaki na maisha ya kutafuta MAFANIKIO YANGU KAFARA NINAYOITO NI MARAFIKI VITU MBALIMBALI NA MTU ANAYENIKWAMISHA KATIKA KULETA CHANGAMOTO ZA KUNIKATISHA TAMAA MM LIAZIMA NIJITENGE NAE.
LikeLike
Kila la kheri katika kusimamia maamuzi haya.
LikeLike
Asante sana kocha, hakika kuna mengi ninapaswa kuyaacha, ili kuweza kutembea kwenye safari hii.
LikeLike
Vizuri na kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha,Mafanikio makubwa ninayoyataka ndo kipaombele cha kwanza kuliko vitu ninavyovipenda.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Siyo unachotaka,bali unachotoa, nahitaji kuacha vyote visivyohusiana na maarifa,kazi na biashara na kuweka kafara yangu kwa kujitoa zaidi na zaidi ili kuendelea kupambania mafanikio yangu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kweli ni muhimu Sana kuzingatia haya mambo mawili na kuyafanyia kazi Kwa uhakika mkubwa Sana . Na mafanikio utayaona.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Ili uweze kufanikiwa;
1. Jua unachotaka.
2. Toa kafara upate unachotaka.
3. Kuwa tayari Kuacha kile kinachokunyima mafanikio.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kutoa kafara ni jambo jema sana. Nilichojifunza ni kuwa mzigo wa mafanikio ni mzigo mzito usiohitaki kuchanganywa na mizigo mingine. Watu wengi wamebeba vinyingo na kulipa visasi hivyo kuwa na mizigo ambayo ni kikwazo kwao kufanikiwa. Fanya kafara ya kuwaondoa watu Kwenye moyo wako. Nawe utapata nafasi ya kuweka mabegi ya mafanikio.
LikeLike
Ahsante Sana kocha kwa huu Uzi mkali wa Leo.
📝 Hii point ya kujua ambacho bado sijawa tayari kukiacha Ili nifanikiwe ndo naenda hasa kukifanyia kazi kwa msimamo wote.
Ahsante sana🤝🤝
LikeLike
Vikwazo vingi vya mafanikio vitaanzia ndani yako mwenyewe
LikeLike
Kuna gharama kubwa ya kupata mafanikio makubwa ninayotaka, kutoa kafara ya kuacha kuwa kwenye comfort zone. Kujikita kwenye mchakato sahihi wa kufanyia kazi mafunzo yote tunayoyoapata kwenye huduma za Kisima cha maarifa, Chuo Cha mauzo na Bilionea mafunzoni. Asante sana Kocha
LikeLike
Vizuri sana, tukae kwenye mchakato.
LikeLike
Asante sana kocha lazima nitoe kafara kwakuachilia vile vitu ninavyo vipenda ili nipate ninacho taka
LikeLike
Hakika.
LikeLike
MAFANIKO NI KWA HAWAMU KWA HAWAMU NA KUPANDA KIDOGO KIDOGO.
KUTOA KAFARA KWA YALE UNAYOPENDA SANA ILI KUFUNGUA MILANGO ZAIDI,
SHUKRANI KOCHA.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Natakiwa kuwa tayari kutoa kafara inayoniumixa mm binafsi badala ya watu wengine ili nipate ninachokata, kafara hiyo inatakiwa niitoe kwa mwendelezo bila kuridhika au kuchoka
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kwa lolote unalokwama kwenye maisha yako, jiulize ni kitu gani bado hujawa tayari kukiacha.
Ukijua na kuacha, mafanikio yatakuwa uhakika sana kwako.
Asante sana
LikeLike
Hakuna mafanikio ya kweli bila kutoa kafara na kuelekeza kila kitu kwenye kile ulichochagua kikupeleke kwenye mafanikio hayo.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Karibu.
LikeLike
mafanikio ni zaidi ya vile wengi wanavyoangalia kwa nje kama njia ya kupima kufanikiwa,hii inapelekea wengi kukwama kupata zaidi kwa kukwamishwa na wanavyokua tayari wamepata.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Nimechagua kujitoa kafara mimi mwenyewe ili niweze kuyafikia mafanikio makubwa ninayoyataka kwenye maisha yangu.
Asante kocha
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Vikwazo vingi kwenye safari yako ya mafanikio vinaanzia ndani yako mwenyewe
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
Utapata chochote kama utakuwa tayari kuachia vile unavyotamani sana kuvikamatia
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Hakuna mafanikio pasipo kujitoa kafara ili uweze kuvuka ngazi moja kuelekea ngazi nyingine ya mafanikio
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
Mafanikio yangu yanaazia ndani yangu.
Ninajua hasa kile ninachokitaka na hicho ndicho ninacho
paswa kukipa kipaumbele Cha kwanza kila siku, chochote kingine mbali na hicho kitakuwa ni kikwazo kufikia mafanikio yangu.
Asante Sana kocha.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kutaka ni rahisi, kutaka kila mtu anataka,inapokuja kutoa ndiyo tunaanza kuachana,asante Kocha kwa kutukumbusha hili.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Asante Kocha. Hakika, lazima niwe tayari kuachilia vile nilivyokamatia sana ndiyo niweze kufungua uwanja wa mafanikio yangu.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ili nifaniliwe ni lazima niachie vile vitu ambavyo nimeshikamana navyo sana!
LikeLike
Hivyo ni kikwazo kikubwa.
LikeLike
Nimekubali kuacha kila kitu kwaajiri ya mafanikio makubwa ninayotataka
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kwa lolote ninalokwama kwenye maisha napaswa kujiuliza ni kitu gani sijawa tayari kuachilia. Asante sana Kocha.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Maisha ni Mwendelezo wa kutoa kafara,
Ili uweze kupata unachotaka lazima uwe tayari kutoa kitu fulan kinachohitajika sana.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitajitahidi kuviepuka vikwazo vyote vinavyonikwamisha katika safari yangu ya mafanikio na nitaendelea kutoa kafara yale yote ninayoyapenda. Asante sana kocha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
maisha ni muwendelezo wa kutoa kafara
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kuachana na vitu ambavyo tayari navipenda sana, na hapo ndipo ulipo ufunguo wa mafanikio yangu.
Asante sana Kocha
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kwa lolote unalokwama kwenye maisha yako, jiulize ni kitu gani bado hujawa tayari kukiacha.
Ukijua na kuacha, mafanikio yatakuwa uhakika sana kwako.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
lazima kuchukua hatua ndogondogo ili kupata mafanikio makubwa
LikeLike
Kweli
LikeLike