3062; Hakuna mjadala.
Rafiki yangu mpendwa,
Fikiria kuna kitu muhimu sana ambacho unataka kununua.
Unaongea na muuzaji wa kitu hicho na anakupa bei.
Mnajadiliana kwenye bei na kufikia muafaka kati yako na muuzaji.
Unaondoka kwenda kuchukua fedha za kulipia kama mlivyokubaliana.
Unarudi ukiwa na kiasi cha fedha kilichokamilika kulingana na makubaliano.
Lakini muuzaji anakuambia hataweza kukuuzia kwa bei hiyo mliyokubaliana, maana amegundua amekupa kwa bei ya chini sana.
Wewe unakitaka sana kitu hicho, ni muhimu mno kwako.
Hivyo mnajadiliana bei mpya ya kukipata.
Unatoka tena mwenda kuongeza fedha.
Unarudi kwa ajili ya kumamilisha mauzo.
Lakini tena muuzaji anakuambia hataweza kukuuzia kwa bei hiyo, ni ndogo sana.
Mpaka hatua hiyo utakuwa tayari utakuwa umepatwa na hasira.
Utaona muuzaji amekosa umakini au hayupo tayari kuuza kile anachouza.
Mwisho kabisa utaamua kuachana naye na kwenda kununua kwa mtu mwingine ambaye amejipanga vizuri.
Utakuwa na haki kabisa ya kumshangaa muuzaji anayebadilika kila wakati, lakini mbona huwa hujishangai wewe mwenyewe?
Kwa sababu tabia aliyokuonyesha muuzaji ya kubadilika badilika kwenye makubaliano, umekuwa unaifanya kwenye maisha yako mwenyewe.
Unaweza kukataa na kujiambia wewe siyo kigeu geu.
Lakini twende tena kwenye mfano ili tuelewane vizuri.
Mara ngapi umejiwekea mpango wa kukamilisha jukumu fulani na kuliwekea kabisa muda wa kulikamilisha.
Lakini wakati wa kukamilisha jukumu hilo unapofika, unabadilika.
Unafungua tena upya mjadala wa iwapo ufanye au usifanye kitu hicho.
Unapoteza muda na nguvu zako nyingi kwenye mijadala isiyo na mwisho.
Kitu pekee ambacho hupati ni matokeo uliyotegemea kwa kufanya kitu hicho.
Hivyo ndivyo umekuwa unaenda kwenye sehemu maeneo mbalimbali ya maisha yako, unapanga vitu vya kufanya, lakini wakati wa kuvifanya unapofika, badala ya kufanya, unafungua upya mjadala.
Ili uweze kufanikiwa, unahitaji kuwa na uwajibikaji wa hali ya juu sana.
Unapopanga kitu cha kufanya, wakati unapofika unapaswa kufanya na siyo kufungua upya mjadala.
Umeshajadiliana na wewe mwenyewe wakati wa kupanga, inapofika wakati wa kutekeleza, tekeleza kama ulivyopanga.
Kamwe usiendekeze mijadala mipya kwenye mipango ambayo tayari umeshaiweka na kukubaliana nayo.
Mara zote fuata mpango wako kama ulivyouweka.
Hata kama unaona kuna maboresho ya kufanya, tekeleza kwanza kama ulivyopanga na utarekebisha baada ya kuwa umeshafanya.
Kuna sababu kwa nini ulipanga jinsi ambavyo umepanga.
Mara nyingi wakati wa kupanga unakuwa na utulivu na akili yako inafikiri vizuri.
Lakini wakati wa utekelezaji unakosa utulivu na hisia zinatawala zaidi akili yako.
Kwa hisia ni rahisi kubadili maamuzi ya awali, lakini mara zote mabadiliko hayo yanakuwa siyo sahihi.
Ukishaweka mipango, kinachofuata ni kuitekeleza kama ulivyopanga.
Hakuna kufanya mabadiliko yoyote kabla hujaanza kufanya.
Heshimu mipango unayojiwekea wewe mwenyewe, utajiheshimu na kuweza kuzalisha matokeo mazuri na makubwa.
Kubadili mipango kila mara, hasa wakati wa utekelezaji ni aina nyingine ya uvivu na uzembe ambayo inakukwamisha sana kupiga hatua.
Panga na kufanya kama ulivyopanga.
Usiruhusu mianya ya kufungua upya mjadala kwenye jambo ambalo umeshaliamulia.
Hata kama unaona maamuzi uliyoweka yana makosa, anza kutekeleza kwanza kabla hujabadili makosa hayo.
Ni muhimu sana ujenge kwanza nidhamu ya kufanya kama ulivyopanga, kwani hiyo itakuwezesha kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Ukishaamua, tekeleza kama ulivyoamua.
Usikubali kufungua tena mjadala na wewe mwenyewe juu ya maamuzi hayo.
Hisia zako zina nguvu kubwa ya kukudanganya, hasa inapofika wakati wa kuchukua hatua.
Usiendekeze mijadala, kuwa mtu wa kuchukua hatua.
Hata kama utakosea, ni bora ukosee kwa kufanya kuliko kuendelea na mijadala isiyo na ukomo.
Matokeo yanazalishwa kwa kufanya na siyo kwa mijadala.
Kuwa mfanyaji mzuri na utaweza kupiga hatua kubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Matokeo yanazalishwa kwa kufanya na sio kwa mijadala.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Msimamo na Nidhamu ya kufanya nilivyopanga ndiyo msingi mkuu Wa kufanikiwa.
Nitafanya kila ninachopanga na siyo kuruhusu mijadala.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante kocha,nikishapanga kitu lazima nitekeleze kuliko kubadilisha maamuzi,na nikiweza kufanya vizuri ndo nitaweza kupiga hatua.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nikishapanga nitafanya matokeo yatajitokeza mbele,sitoahirisha kuanza kufanya nilichopanga maadam hakinigharimu uhai
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Hizi kurasa hizi zimebeba mambo uhalisia asee dah changamoto zetu zingi huku
LikeLike
Tuchukue hatua.
LikeLike
Moja ya mambo yaliyonirudisha nyuma ni kuirudiarudia kupanga tena. Kuanzia Sasa kile ninachokipanga nakifanya kwanza. Kama Kuna mabadiliko yatafuata baadae. Asante sana Kocha Kwa elimi hii ya Leo.
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike
Ukishaweka mipango, kinachofuata ni kuitekeleza kama ulivyopanga.
Asante sana
LikeLike
Kabisa, mjadala unafungwa.
LikeLike
Mafanikio makubwa yatatokana na mimi kujijengea nidhamu ya kufanya kama nilivyopanga na si vinginevyo. Asante Kocha.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Hata kama unaona maamuzi uliyoweka yana makosa, anza kutekeleza kwanza kabla hujabadili makosa hayo.
Asante sana Kocha.
LikeLike
Kabisa, ni rahisi sana kujidanganya ili usifanye.
LikeLike
Asante kocha, kwa kushindwa kuwa mfanyaji ndiyo kumepelekea kuwa hivi nilivyo sasa ninakwenda kuwa mfanyaji bora wa yale tunayokubaliana
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha , makala imenilenga Mimi. Nitajisukuma Sana kuiishi . Ninakili kabisa ili nifanikiwe ninapaswa niwe na uwajibikaji wa Hali ya juu Sana . Ninapokuwa ninapanga akili huwa na utulivu. Wakati wa kutekeleza hisia huigia na hudanganya Sana. Ili niepuke kuahilisha
Ninapaswa kufanya Kama nilivyopanga.
SHUKLANI SANA KOCHA
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitafanya kama nilivyopanga kufanya.
Sitobadili maamuzi nuliyopanga kwenye mwendo wa kufanya
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Panga na kufanya kama ulivyopanga usighairishe.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Sitakua kigeugeu tena yaani nikiweka mpango kinachofuata nikuitekeleza Asante sana kocha
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
NIkipanga kitu unapofika muda wa kutekeleza nitatekeleza kama nilivyopanga bila kuruhusu sababu zozote…..
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ahsnate sana kocha, nitatekeleza yote niiiyoyapanga bila mjadala
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mijadala kweli haifai ni bors kufany kwanza then ukosee kuliko kujadiliana na kutokufanya
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nikweli Mjadara wa maboresho ya mpango ufanywe wakati wa kupanga na wakati wa kutekeleza acha kazi ichukue nafasi yake.
Asante.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Mimi ni Mtu wa kufanya na Sio Miti wa mijada.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kilicho pangwa kifuatwe kama kilivyo pangwa ili kujenga nidhamu kali.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Matokeo yanazalishwa kwa kufanya na siyo kwa mijadala.
Kuwa mfanyaji mzuri na utaweza kupiga hatua kubwa.
Asante sana
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
nitaendelea na msima wangu niliouweka mwanzo bila ya kubdili maamuzi
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Nazalisha matokeo kwa kufanya na siyo kwa mjadala.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha kwa somo hili. Nitajitahidi kufanya kama nilivyopanga.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kubadili mipango kila mara, hasa wakati wa utekelezaji ni aina nyingine ya uvivu na uzembe ambayo inakukwamisha sana kupiga hatua.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
NUK _Nidhamu, Uadilifu na kujituma nitatembea humo kwa kufanya nilichokipanga.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike