3073; Faida, Hasara au Mshahara?
Rafiki yangu mpendwa,
Jim Rohn aliwahi kunukuliwa akisema; unalipwa kulingana na thamani unayoipeleka sokoni.
Hiyo ina maana kwamba kiasi cha fedha unachopata, kinategemea sana kile unachofanya na jinsi unavyofanya vitu hivyo.
Kanuni ya msingi ya uchumi pia inaeleza wazi juu ya mahitaji (demand) na upatikanaji (supply) wa kitu.
Kwamba kadiri kitu kinavyokuwa na upatikanaji mdogo, ndivyo uhitaji wake unakuwa mkubwa na hilo kupelekea kitu hicho kiuzwe zaidi.
Kwa upande wa pili, upatikanaji wa kitu unavyokuwa mkubwa, ndiyo uhitaji unakuwa mdogo na bei yake pia kushuka.
Kwa kuzingatia hayo mawili, kuna malipo ya aina tatu ambayo mtu unaweza kupata kutoka kwenye biashara yako.
Moja ni faida.
Unatengeneza faida kubwa pale uhitaji wa kile unachouza ni mkubwa kuliko upatikanaji. Kadiri kitu kinavyokuwa na uhaba, ndivyo wengi zaidi wanavyotaka kukipata na hilo kufanya bei yake izidi kupanda.
Ni kupitia bei kupanda ndiyo mtu anaweza kutengeneza faida kubwa sana.
Hatua ya kuchukua hapa ili utengeneze faida kubwa ni kuuza kitu ambacho kinapatikana kwako tu na siyo kwa wengine.
Kitu hicho kiwe kina thamani kubwa sana kwa watu kiasi cha wao kuona maisha yao hayajakamilika bila ya kuwa na kitu hicho.
Thamani inapokuwa kubwa na uhaba kuwepo, bei inakuwa kubwa sana na faids inakuwa nzuri.
Mbili ni mshahara.
Unapata mshahara pale upatikanaji na uhitaji vinapokuwa vinaendana. Yaani upatikanaji unakuwa sawa na uhitaji uliopo. Kwa usawa huo wa upatikanaji na uhitaji, bei haziwezi kuwa kubwa, zinabaki za kawaida tu kwa sababu hakuna uhaba mkubwa.
Hapo pia thamani inakuwa ya kawaida, ambayo watu wanaweza kuipata mahali pengine.
Watu wengi wapo kwenye kundi hili, wakifanya mambo ya kawaida na kupata kipato cha kawaida pia.
Licha ya kuweka juhudi kubwa, bado kipato chao kinabaki cha kawaida kwa sababu hakuna nguvu inayosukuma walipwe zaidi.
Hakuna thamani kubwa wanayotoa na wala hakuna uhaba wa kile wanachotoa.
Tatu ni hasara.
Hasara inapatikana pale upatikanaji wa kitu unakuwa mkubwa sana kuliko uhitaji uliopo. Hapo kitu kinakuwa kinapatikana kwa wingi, wakati hakuna wenye uhitaji na kitu hicho.
Na kwa kuwa kitu kinapatikana kwa wingi na watu hawana uhitaji nacho mkubwa, hawakithamini. Watu hawaweki thamani kubwa kwenye kitu ambacho wanajua wanaweza kukipata kwa urahisi.
Kwa kupatikana kwa wingi na thamani kuwa ndogo, bei ya kitu inakuwa ndogo sana kitu kinachozalisha hasara kubwa.
Kwa upatikanaji mkubwa na uhitaji mdogo, hasara inakuwa kubwa kiasi cha mtu kushindwa kuendesha biashara.
Hapo ndipo ushindani unapoua biashara nyingi, kwa watu kuiga kile kinachofanywa na wengine.
Kuondoka kwenye hali hii ya hasara ni kuhakikisha unageuza hali hizo mbili, kufanya upatikanaji wa kile unachouza wewe adimu, huku ukitengeneza uhitaji mkubwa kwa wateja wako.
Pia chochote unachouza, hakikisha ni cha thamani kubwa sana kwa wale unaowalenga.
Kwa thamani kubwa kubwa na upatikanaji wa uhaba, utaweza kuondoka kwenye hali ya kutengeneza hasara na kwenda kwenye hali ya kutengeneza faida.
Kikubwa sana ambacho tunapaswa kuondoka nacho hapa ni tunayo nguvu ya kuamua kiasi gani tulipwe kupitia biashara tunazofanya.
Nguvu hiyo inahusisha maeneo mawili, thamani na kanuni ya upatikanaji na uhitaji.
Kwenye thamani, uza kitu ambacho kina thamani kubwa kwa wale unaowalenga. Yaani kitu ambacho kinatatua matatizo waliyonayo na kutimiza mahitaji yao. Wape watu kitu ambacho maisha yao hayawezi kwenda bila kuwa nacho.
Kwenye kanuni ya upatikanaji na uhitaji, mara zote hakikisha unachouza kinapatikana kwako tu, huku uhitaji wake ukiwa mkubwa. Ni wajibu wako kuhakikisha kuna kitu ambacho wateja wanaweza kukipata kwako tu na hawawezi kukipata kwa wengine. Halafu kuwafanya wengi watake kupata kitu hicho kwako.
Hayo ni mambo ambayo yanawezekana kabisa, ila yanataka mtu uache kufanya mambo kwa mazoea.
Lazima uweke kazi hasa, ambayo moja kwa moja itaongeza thamani na kufanya watu wawe na uhitaji mkubwa nayo, wakati upatikanaji ni wa uhaba, maana ni kwako tu.
Weka kazi inayohitajika ili uweze kutengeneza faida kubwa sana.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kwenye kanuni na upatikanaji na uhitaji ni muhimu kuhakikisha kwamba kinachouzwa kinapatikana kwangu tu, huku uhitaji wake ukiwa mkubwa.
LikeLike
Ukiseti hilo vizuri, utajenga biashara kubwa sana.
LikeLike
Weka kazi inayohitajika sana ili uweze kutengeneza faida.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitatengeneza thaman ili kukipa thaman kile ninachofanya au ninachouza.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nitatoa thamani kubwa ili kufanya kile ninachotoa au kuuza kuwa na uhaba ili kutengeneza uhitaji mkubwa kwa watu.Kupitia hilo nitaweza kutengeneza kiasi kikubwa cha fedha.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nitazingatia hili niweke Kitu kinachohitajika kwa wengi na kiwe kinapatkana kwangu tu
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nitauza bidhaa zenye thamani kwa wale ninaowalenga. Asante kocha kwa somo hili.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Nahakikisha nitauza kitu ambacho kina thamani kubwa kwa wateja wangu.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kuweka kazi ni muhimu Sana Ili kuuza zaidi nakutengeneza faida
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ninayo nafasi ya kiwango cha kulipwa kulingana na thamani ninayoitoa
LikeLike
Vizuri, ifanyie kazi.
LikeLike
Tengeneza thamani kubwa kwa upatikanaji wa uhaba
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Jambo kuu la kujifunza ni kutoa thamani na kanuni ya upatikanaji na uhitaji wa kile ambacho ninakiuza ni jambo kubwa la msingi kuzingatia kwenye mauzo
LikeLike
Hakika
LikeLike
Thamani inakuwa kubwa kwa unachouza pale uhitaji wake unapokuwa mkubwa kuliko Wingi wa kitu hicho sokoni.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Inatupasa tuwe na upekee wa kutoa huduma bora sana kuliko washindani wetu, pia na kuwa na bidhaa zenye ubora na maslahi makubwa sana kwa wateja wetu.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Unalipwa kadiri ya thamani unayozalisha sokoni.
Bila thamani huwezi kulipwa vizuri.
Tutengeneze uhaba Ili kuweza kutawala soko na kupata faida.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Thamani kubwa inaunda uhaba na Kupelekea bei kubwa inayotengeneza faida nzuri.
LikeLike
Ndiyo hivyo.
LikeLike
Kikubwa sana ambacho tunapaswa kuondoka nacho hapa ni tunayo nguvu ya kuamua kiasi gani tulipwe kupitia biashara tunazofanya.
Nguvu hiyo inahusisha maeneo mawili, thamani na kanuni ya upatikanaji na uhitaji.
Asante sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kuuza kitu ambacho kinapatikana kwako tu na siyo kwa wengine! Hapa kunataka kazi ya ziada Kocha
LikeLike
Mafanikio yanataka kazi ya ziada, ingekuwa rahisi kila mtu angekuwa nayo.
LikeLike
“Weka kazi inayohitajika ili uweze kutengeneza faida kubwa sana.”
Ahsante sana Kocha.
Nitaweka kazi hasa.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Biashara inaweza kuwa Ile-Ile ila ukaongeza thamani na ubunifu na kuleta tija. Utapata mauzo na faida na biashara kuimarika.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Faida, Hasara au mshahara,nitaweka kazi mbele yenye kutoa thamani kubwa.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ndiyo maana fedha huwakilisha thamani, ili upate fedha nyingi sana ni lazima kwako kuwe na thamani nyingi sana.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha,Nitahakikisha ninatengeneza thamani kubwa ili niweze kupata faida.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Wape watu kitu ambacho maisha yao hayawezi kwenda bila kuwa nacho.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Unapata mshahara pale upatikanaji na uhitaji vinapokuwa vinaendana. Yaani upatikanaji unakuwa sawa na uhitaji uliopo. Kwa usawa huo wa upatikanaji na uhitaji, bei haziwezi kuwa kubwa, zinabaki za kawaida tu kwa sababu hakuna uhaba mkubwa.
LikeLike
Tukwepe huo mtego.
LikeLike
Kulipya kwako kunategemea thani unayotoa
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Unatengeneza faida kubwa pale uhitaji wa kile unachouza ni mkubwa kuliko upatikanaji wake.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ni wajibu wangu kuhakikisha kuna kitu ambacho wateja wanaweza kukipata kwangu tu na hawawezi kukipata kwa wengine. ✍️
LikeLike
Kabisa.
LikeLike